Naomba ushauri nimekwama kimapenzi, niufuate moyo wangu au akili?

Badili kwanza jina ujiite Hanifer Mjinga ili nami niweze kuchangia.
 
Nimerudi niemchoka, najihisi kuchanganyikiwa kwani anataka kunioa ila sioni kama nitakua na furaha.
anataka kukuoa au unataka kujiozesha kwake kwa nguvu?

Inaonyesha dhahiri hakutaki lakini unajipendekeza kwani asingekufanyia jeuri hiyo ya kukwambia umlipie na mwanamke wake halafu na wewe kama zuzu ukalipia gharama hizo.

Dunia hii haishi maajabu. Mama jiondoe mapema sana huyo siyo mume hata kidogo. Ungekuwa mwanangu ningekuchapa viboko kabisa kwa hiyo dharau anayokufanyia.

Samahani kwa maneno makali lakini una elimu kubwa ila hujitambui.
 
Pole Sana daktari, hisia ziko juu Sana kwako na zimeelekeza conscious mind Yako kutokubali uhalisia wa mambo (kuona hata alifanyalo lisikupoteze kwenye mapenzi) lakini, Kwa afya Yako ya akili pamoja na mstakabali wa maisha Yako kwakweli acha naye jifunze kuacha mtu aende after 21 days utakua mtu mpya kabisa na utaangalia nyuma na utakuja kugundua kuwa umepitia kwenye mambo magumu Sana na pia utakuja kugundua kuwa ulizipa hisia zikuongoze kuliko fikra/akili.
Nawasilisha
 
Wewe sio DR ni kichaa upo milembe umeiba simu ya mganga mfawizi wa hospital ya dodoma.
 
Acheni kungangania wanaume mahandsome
 
Kama si chai, basi umejikorogea sumu hatari sana na ukaanza kuinywa.
Anyway! Ukiolewa na kumzalia angalau watoto 2, akianza kukuzaba makofi usije kutuletea machozi humu
 
Pole!!

Acha ujinga

Ndoa ni zaidi ya hisia hizo!!


Tafuta mtu mwenye kazi inayoeleleweka mwenye tabia njema akuoe!!

Usimfiche mwambie tu unataka uolewe nae!!
 
Tupa hilo zigo bovu[emoji57]subiria atakae kupenda na kukupa tulizo la moyo.
Achana na mwanaume asiyekupenda atakutesa mpaka utaona rangi zote.


Jipige kifua sema mimi ni mtumwa kipofu.
 
Hello JF, nina miaka 27, sijaolewa bado ila nina mchumba na kashajitambulisha kwetu. Mimi nafanya kazi kwenye NGO ya kimataifa (ni daktari kitaaluma) nina kipato kizuri


Tafadhali sana acha kufananisha mchumba na vitu vya hovyoo.
 
Huu uongo ni kwa faida ya nani?
 
Hii bahati ni Tanzania hii hii au ni wapi..tuwekane sawa..!
 
Dada hujaolewa unamasikitiko namna hii ukiolewa unahisi utapata furaha, achana na huyo mtu hakufai.
 
Sjui unahitaji kithibitisho gani kuwa huyo sio sahihi kwako??haya kila la kheri lkn watu hubadilika
 
Hakuna mwanamke wa dizaini iiii toka duniaaa kuuumbwaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Yani nimepata hasira sana,unawezaje kulea gume gume Hilo??ahh,yani umlipie mwanaume pesa alale na mwanamke mwingine?? Really?? Huu ni upumbavu na sio upendo,ni ujinga uliokithiri,mwanaume kama hakupendi hata umfanyie Nini,atakuina boya tu,acha kupoteza muda na pesa zako bure,sio lazima kuwa na mwanaume,muombe Mungu atakupa wa kwako wa kufanana naye,pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…