Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

Kama nilivyoeleza awali kupitia Uzi ambao niliuweka week hii


Nimeamua kuwaambia ukoo wangu, Kuanzia Mama sina Baba R.I.P
Mashangazi, Baba Mdogo na wajomba nia yangu ya dhati kuiomba msamaha familia ya ambaye alikuwa mchumba wangu,

Naenda kuomba msamaha nikitegemea maswali magumu,

Naenda Kuomba msamaha nikijua maumivu na uchungu hata hasara waliyopata kutoka Mbeya hadi Ngara,

Hatua ya Kwanza
Nimeamua niangalie upepo ndani ya familia yangu, idadi ya wanaonisapot,

Niangalie mtazamo wao juu ya kwanini nasukumwa kuomba msamaha,

Tatu naangalia dhamira yangu na msukumo wa moyo wa dhati,

Nne Nimeamua kuwashirikisha ndugu na kuwaambia sitaenda moja kwa moja kwa wakwe ila ntaenda kwa mshenga

Tutaenda timu ya watu 7 watu wazima sita na mimi nikiwa wa saba, katika timu hiyo mama aneendelea kugoma kutoshiriki, Nimepata shangazi mama mdogo na baba mkubwa,na wengine

Tutaelekea kwa mshenga kuomba radhi, na kueleza sababu za kutokuwapo kwenye send off alafu tumuombe atuombee msamaha,

Baada ya wao kujua tunaomba msamaha kup kwa mshenga

Nimeandaa kishika uchumba walicholipa na nimeandaa wazee 5 na wanisindikize Mbeya kutoka Ngara kwenda kuomba msamaha na pia kabla ya kufika kwenye familia ya wakwe, tutapitia kwenye parokia iliyokaribu kumuona kiongozi wa dini atupe mwongozo na kumuomba atupe ushirikiano kufika kule, pia tutaomba aambatane na wazee wa heshima wa Kanisa, hii nitaifanya tu hata wasipotoa jibu pitia kwa Mshenga

Nikifika nitakuwa na maombi mawili

1.Kuomba kusamehewa na kurudisha kishika uchumba chao

Ama

2.Kuomba kusamehewa na kuendelea na mchakato wa harusi kama watakua bado hawajapata mtu.

Naombenii mawazo yenu mengine pia

asante
 
Jambo zuri sanaa....

Uzuri umetambua kosa lako lakini usisahau sababu iliyokupelekea kufanya kosa.....

Naamini watakusamehe Ila hawatokusahau,na itapendeza kama utawaweka wazi kwamba una katoto Ili uko mbeleni usijeleta balaa jengine.
 
Ni Uamuzi wa Busara kuomba msamaha ila zingatia maswali yafuatayo
1.Kwanini hukutoa nafasi ya Kuwasikiliza juu ya majungu uliyoambiwa na ukatimka?

2.Je Dhamira yako ni kuomba msamaha kweli au ni kwakuwa unataka kuolewa hapo

3.Vipi wakipokea kishika uchumba wakasema tutakujibu, alafu ukasikia kaoa mwingine?

Naona kwanza ungeanza kujua Mwanaume wako Ana mtazamo gani na je anakubali haya?

Britannica
 
Pole kwa yote, kila lakheri uendelee kuleta mrejesho hapa ili uzidi kupata ushauri.
 
Kama atakuwa hanitaki Tena sina Budi kukubaliana na yanayoendelea
 
Dada yangu nakushauri rudisha kishika uchumba cha watu na vitu unavyokumbuka kwa ni moto na vinafunga milango ya baraka hata kama we ni mzuri kiasi gani
Ndio maana kanisa limekushauri hivyo
Vya kuolewa huko hapana kwa furaha ya baadaye
 
Kwan wee ni MUHAYA ???.

Sijaona mantiki yako ya kwenda ukweni kuomba msamaha ukiwa na machaguzi mawili

Et naomba nisameheni , kama mtapenda kunisamehe ili tuendelee na ndoa, au mnisamehe ila niwarudishie kishika uchumba chenu...

Hii inaonyesha ,Bado huna Dhati thabiti ya kuomba msamaha na kile kikichofanya usitokee ndicho kinaendelea kukuweka njia panda kama katoto (kitindamimba ) ka shetani .


Ushauri wangu...


Nenda kwa kusudio la kumuomba msamaha mchumba wako ,asamehe yalotokea muendelee na mchakato.

Ili yeye na wakwao ndio wabaki wenye kuamua !!!!.




Nmefarijika tu kujua wee ni binti wa miaka 29 . .... Umebakiza miaka 2-3 , nawee uaanze kujiita Feminist!!!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…