Ni jambo jema kuomba msamaha.Nadhani wewe stiki na option one ya kuwambia kwamba unaomba msamaha kwa usumbufu na hasara uliowasababishia na pili unarudisha kishika uchumba.Wakikipokea hicho kishika uchumba hoja yako namba mbili inakufa outomatically.kwamba hawana haja na wewe ten.ila wakikataa kikupokea basi ujumbe ni kwamba uchumba wako bado upo upo.So wewe washukuru na ondoka zako.Wao watapanga lini wanakuja kumalizia process zilizobaki.Wewe uwe tayari.Kama nilivyoeleza awali kupitia Uzi ambao niliuweka week hii
Nimeamua kuwaambia ukoo wangu, Kuanzia Mama sina Baba R.I.P
Mashangazi, Baba Mdogo na wajomba nia yangu ya dhati kuiomba msamaha familia ya ambaye alikuwa mchumba wangu,
Naenda kuomba msamaha nikitegemea maswali magumu,
Naenda Kuomba msamaha nikijua maumivu na uchungu hata hasara waliyopata kutoka Mbeya hadi Ngara,
Hatua ya Kwanza
Nimeamua niangalie upepo ndani ya familia yangu, idadi ya wanaonisapot,
Niangalie mtazamo wao juu ya kwanini nasukumwa kuomba msamaha,
Tatu naangalia dhamira yangu na msukumo wa moyo wa dhati,
Nne Nimeamua kuwashirikisha ndugu na kuwaambia sitaenda moja kwa moja kwa wakwe ila ntaenda kwa mshenga
Tutaenda timu ya watu 7 watu wazima sita na mimi nikiwa wa saba, katika timu hiyo mama aneendelea kugoma kutoshiriki, Nimepata shangazi mama mdogo na baba mkubwa,na wengine
Tutaelekea kwa mshenga kuomba radhi, na kueleza sababu za kutokuwapo kwenye send off alafu tumuombe atuombee msamaha,
Baada ya wao kujua tunaomba msamaha kup kwa mshenga
Nimeandaa kishika uchumba walicholipa na nimeandaa wazee 5 na wanisindikize Mbeya kutoka Ngara kwenda kuomba msamaha na pia kabla ya kufika kwenye familia ya wakwe, tutapitia kwenye parokia iliyokaribu kumuona kiongozi wa dini atupe mwongozo na kumuomba atupe ushirikiano kufika kule, pia tutaomba aambatane na wazee wa heshima wa Kanisa, hii nitaifanya tu hata wasipotoa jibu pitia kwa Mshenga
Nikifika nitakuwa na maombi mawili
1.Kuomba kusamehewa na kurudisha kishika uchumba chao
Ama
2.Kuomba kusamehewa na kuendelea na mchakato wa harusi kama watakua bado hawajapata mtu.
Naombenii mawazo yenu mengine pia
asante
Mwisho usisahu kuwaambia pia una mtoto.ili usije tena kuwa na kitu kingine cha kuwaomba msamaha hapo badaye