Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

Kama nilivyoeleza awali kupitia Uzi ambao niliuweka week hii



Nimeamua kuwaambia ukoo wangu, Kuanzia Mama sina Baba R.I.P
Mashangazi, Baba Mdogo na wajomba nia yangu ya dhati kuiomba msamaha familia ya ambaye alikuwa mchumba wangu,

Naenda kuomba msamaha nikitegemea maswali magumu,

Naenda Kuomba msamaha nikijua maumivu na uchungu hata hasara waliyopata kutoka Mbeya hadi Ngara,

Hatua ya Kwanza
Nimeamua niangalie upepo ndani ya familia yangu, idadi ya wanaonisapot,

Niangalie mtazamo wao juu ya kwanini nasukumwa kuomba msamaha,

Tatu naangalia dhamira yangu na msukumo wa moyo wa dhati,

Nne Nimeamua kuwashirikisha ndugu na kuwaambia sitaenda moja kwa moja kwa wakwe ila ntaenda kwa mshenga

Tutaenda timu ya watu 7 watu wazima sita na mimi nikiwa wa saba, katika timu hiyo mama aneendelea kugoma kutoshiriki, Nimepata shangazi mama mdogo na baba mkubwa,na wengine

Tutaelekea kwa mshenga kuomba radhi, na kueleza sababu za kutokuwapo kwenye send off alafu tumuombe atuombee msamaha,

Baada ya wao kujua tunaomba msamaha kup kwa mshenga

Nimeandaa kishika uchumba walicholipa na nimeandaa wazee 5 na wanisindikize Mbeya kutoka Ngara kwenda kuomba msamaha na pia kabla ya kufika kwenye familia ya wakwe, tutapitia kwenye parokia iliyokaribu kumuona kiongozi wa dini atupe mwongozo na kumuomba atupe ushirikiano kufika kule, pia tutaomba aambatane na wazee wa heshima wa Kanisa, hii nitaifanya tu hata wasipotoa jibu pitia kwa Mshenga

Nikifika nitakuwa na maombi mawili

1.Kuomba kusamehewa na kurudisha kishika uchumba chao

Ama

2.Kuomba kusamehewa na kuendelea na mchakato wa harusi kama watakua bado hawajapata mtu.

Naombenii mawazo yenu mengine pia

asante
Ni jambo jema kuomba msamaha.Nadhani wewe stiki na option one ya kuwambia kwamba unaomba msamaha kwa usumbufu na hasara uliowasababishia na pili unarudisha kishika uchumba.Wakikipokea hicho kishika uchumba hoja yako namba mbili inakufa outomatically.kwamba hawana haja na wewe ten.ila wakikataa kikupokea basi ujumbe ni kwamba uchumba wako bado upo upo.So wewe washukuru na ondoka zako.Wao watapanga lini wanakuja kumalizia process zilizobaki.Wewe uwe tayari.

Mwisho usisahu kuwaambia pia una mtoto.ili usije tena kuwa na kitu kingine cha kuwaomba msamaha hapo badaye
 
Asante lakin hilo la Katoto nitalitafakari zaidi
Yaani unaolewa bila jamaa kujua kuwa una mtoto? Inavyoonekana wewe unaitaka ndoa pekee na wala haujampenda huyo jamaa , kama unataka kuwa huru ni bora ukamwambia ukweli maana akija kugundua ndani ya ndoa ataomba ushauri kwa wazee wake halafu unajua nibi kitatokea?

Kwanza jua hakuna mzazi anapenda mwanaye aoe single mother na ukijumlisha na kosa la kwanza kutumia hisia zaidi badala ya logic(sikulaumu ni wanawake wote huwa mnatenda kabla ya kufikiri) utaondoka kwenye hiyo ndo kwa aibu trust me.

Edit:
Wakati nasoma comment sikujua kwamba jamaa anajua kuwa una mtoto , ndo maaana nika comment mwanzo.
Ila hii haibadilishi mantiki kwamba hakuna mzazi anapenda mwanaye aoe single mother ila kama unataka ufanye maamuzi yaliyo na tija ni bora kuwataarifu hao wazazi wake amini nakuambia uongo haudumu .

Na kwasababu umeshafanya tukio la kwanza watakuwa makini sana na ww na ikatokea wakahisi hata kidogo amini hiyi ndoa utaiona chungu.
 
Mimi nachokushauri move on na maisha yako, hao wakwe watakuwa wajinga sana kukupokea tena ukaolewe na mtoto wako.

Kwa sasa kinachokusumbua ni stress na frustration wala sio msamaha.
Ushaharibu kubaliana na ukweli and move on usiende kusumbua watu.
 
Mimi nachokushauri move on na maisha yako, hao wakwe watakuwa wajinga sana kukupokea tena ukaolewe na mtoto wako.

Kwa sasa kinachokusumbua ni stress na frustration wala sio msamaha.
Ushaharibu kubaliana na ukweli and move on usiende kusumbua watu.
Si Vibaya Kujaribu, hata wasiporuhusu kuolewa cha muhim Uhuru na amani
 
Fuata ushauri wa mama yako hao wengine ni wapitaji mambo yakikuharibikia huko ni mama pekee wa kuchukuliana nawe.
 
mimi nikikaa kwenye nafasi ya huyo mumeo, nitakusamehe lakini siwezi kuendelea na mwanamke ambae anakurupuka kama wewe kwa maneno ya "uzushi"....hata kama kuna ukwel ndani yake, bado ulipaswa kumsikiliza utetezi wake.... rudisha hela ya watu kwa tigo pesa, tuma sms ya msamaha usisumbue watu na kuharibu nauli, usisahau ya kutolea[emoji4]
 
Kwann usiendelee na maisha yako aisee.

Imetokea yametokea basi, mambo ya kurudi nyuma ya nini.

Vitu vingi na mambo mengi hutokea kwasababu maalum ambazo ni fumbo na muda mwingi huwezi kujua.

Inawezekana usitishwaji wa hiyo safari yenu ya ndoa ilikua na kusudio la kificho, labda ungemsababishia matatizo huyo muoaji, au angekuasababishia shida ambazo baadae ungejutia zaidi kuwepo ndoani.

Inatakiwa kukubaliana na matokeo, usitake kuforce mambo.
 
Kama Kawaambia atakuwa kanirahisishia
Nimekufananisha na mzee mmoja ambae tulikua tunashea mradi mmoja wa maji kwa hiari sasa baadae alivyokuja kupata maji ya serikali nikamuuliza mzee VP kuhusu kufuatilia maji kwenye mradi wetu wa hiari! Akanijibu hayo maji nikiyapata ni sawa nikiyakosa ni sawa,majibu ambayo yalitokana uwepo wa mradi B (serikali),sasa kwa hii situation yako nadhani ulikuwa na Mr.A na sasa una Mr.B kwaiyo huna cha kupoteza
 
Kama Kawaambia atakuwa kanirahisishia
Acha kuamini kwenye kurahisishiwa
Makosa ya awali ya kuwakataa alafu wajue una mtoto tena mlipanga iwe siri hii itazidisha chuki yao kwako. Na hata kijana wao akikubali wao wataamini kuna cha ziada kwako sio bure (ushirikina). Lengo la kurudisha hiyo kishika uchumba iwe tu ni kuomba msamaha mengine yakufuate usiyatafute.
 
mimi nikikaa kwenye nafasi ya huyo mumeo, nitakusamehe lakini siwezi kuendelea na mwanamke ambae anakurupuka kama wewe kwa maneno ya "uzushi"....hata kama kuna ukwel ndani yake, bado ulipaswa kumsikiliza utetezi wake.... rudisha hela ya watu kwa tigo pesa, tuma sms ya msamaha usisumbue watu na kuharibu nauli, usisahau ya kutolea[emoji4]
[emoji23][emoji28] Danh! Asisahau na ya kutolea au sio
 
Ngoja nipite kimya nisikoment chochote maana ingekuwa ndo mimi umenifanyia hivyo halafu leo hii ghafla uje kuomba msamaha nakutoa nduki na hao wazee wako( huwa sisamehe wanawake niliwahi kumsamehe msariti mmoja ilinikosti sana!
 
Hatukutaki usijeee.....tutakupiga bureee.we rudisha kishika uchumba Cha ndugu yetu.hi ndoa haikupangwa na mungu inaweza ikawa mbele Ni hatari zaidi
 
Back
Top Bottom