Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

Wanawake wengi huwa hawajipi nafasi kuchunguza yale wayasikiayo.. hukurupuka. Ila unapaswa kuongea na muhusika mkuu ambaye ni mchumba wako huyo mkishayaweka sawa ndipo unaweza panga safari hiyo tarajiwa..
 
Namba mbili kwanzaaa.... Hilo la kurudisha kishika uchumba mpaka waombe wao

Sent from my 5023F using JamiiForums mobile app
 
Lipa gharama zote ulizowasababishia pamoja na kishika uchumba. Binafsi hutakiwi kusamehewa. Wanawake kama ninyi ndio mnasababisha wanaume wafe kwa stress za mapenzi. Unajua maumivu kiasi gani ulimsababishia huyo jamaa?
 
Duh...dunia, duara!

Omba msamaha usio na masharti.....utapata amani. I.e. Usiweke tegemeo la kuendelea na mchakano wa ndoa kama sababu ya kuomba radhi. Kama unaamini ulikosea, omba radhi tu bila kujali kama utaolewa nae ama la.
 
Hii CHAI ila kwa mtindo wa Series S01E2.
 
Next time kama ukiolewa epuka majungu, sio kila unaloambiwa uliamini bila kumsikiliza muhusika

nilitaka kusema ivyo ivyo, umbea utakupeleka wapi dadangu unaona ulivyokucost ? next time punguza ujuaji na uwe na subira...wanawake kila anaemletea habari huwa wanamsikiliza kama vile zile habari za ukweli zote daaah huwa siwaelewi kwakweli
 
Dada you must be very desperate to get married. Wazo na tendo la kuomba msamaha ni nzuri sana. Do not expect to be trusted by either your boy friend or your in-laws. Omba msamaha na tafuta maisha elsewhere. Kufanya kosa siyo kosa ila kurudia ni kosa. Jipange upya my dearest single mum😭😭😭😭
 
Umeamua vyema, na nakupongeza kwa hilo ila suala la kutaka mchakato kuendelea hilo waachie wao waliseme.

Kazi yako kwa sasa ni kuomba msamaha tu.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
We chenga sanaa...

Mwanaume kama mimi nakusamehe ila ndoa hamna apo.
Labda kama jamaa naye awe chenga au umemzidi kipato au baadhi ya vitu otherwise you two have zero compactibility.

Na kama yeye ndo kakuzidi alafu awe hana mtoto na yeye!! am sorry my sister.
 
Ni Jambo la busara sana, ila mama yako mmh sisemi neno
 
singo maza mkurupukaji, hupaswi kuolewa, rudisha hela ya watu kwa TigoPesa
 
Huo ndio utu! Tujifunze kutokana na makosa, natumaini umejifunza kuwa mawasiliano katika uhusiano wowote ni muhimu.
Nimependa umekuwa na wazo kama nililotoa kwenye bandiko lako la awali, kuwa omba msamaha na rudisha kishika uchumba.
 
Ni vizuri kuomba msamaha Ila sidhni kama litakuwa Jambo jema kuolewa tena apoo maana sioni Amani ikiwa kwenye maisha yenu ya mbeleni ata kama ndoa itafungwa omba msamaha Rudisha pesa Yao angalia mbele labda wao ndyo wang'ang'anize mwanao akuowe tena Ila option iwe kwenda kuomba msamaha na kurudisha kishika uchumbw chao
 
[emoji23]mbongo anakushauri na dongo juu,,,feminist to be.
 
Sipati Jambo Kama hili linskotokea umemchukua Bi mkubwa , Mama wadogo, wakubwa, shangazi, dada umewalundika kwenye coaster mpaka Ngara mda huo ushaingia gharama za kufa mtu..

Then wanafika Ngara simu zote hazipatikan, wanakuuliza huna jibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…