Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

We meanamke ni mjinga kiasi cha kutosheleza yani una mtoto alafu uanataka kijana wa watu ye akuoe asiwe hata alikua na mtu wake ulizani angekua anakusubiri weee tu,umesikia maneno tu umeharibu kila kitu hufai kuwa mke hata kidogo una hasira za ajabu ,huna busara,hata elimu yako nahisi hujaelimika ,

Kijana wawatu kajitoa kweli kweli nanukienda ukawasimulia uo ujinga wako eti umeskia kaoa sijui nini na nini sahau ndoa apo,yeameridhia we unaleta ushubwada ,utamtesa kaka wa watu bure
 
Maelezo yooote sioni kama wewe na huyo mwanaume kama mtajenga ndoa nzuri na ya maelewano.

Kwa umri wangu wa kuishi, kila ndoa niloona ni mfano bora kwangu inamawasiliano mazuri ya wanandoa, nnachoona kwenu wote mnacheza na jukwaa.
 
Ni Jambo zuri kuomba msamaha. Ila msamaha utoke ndani ya moyo wako. Usirudishe kishika uchumba.
Kawaambie pia kuwa una mtoto. Nakutakia safari njema
 
Nenda kaombe msamaha, ikiwezekana wape kishika uchumba chao yaishe.

Utapata msamaha wao utaishi kwa Amani na nakusubiria mume mwingine akija itakua sawa kuliko huyo.

Mpaka sasa ndugu wa mumeo kwa uliyoyatenda hawatakua na Amani na ww ata wakisamehe wapo watakao Kia nakinyongo bado na itapelekea mara zote kukitokea jambo watasimama upande wa kijana wao na ww utaona wanakuonea ila ni sababu ulishawawekea mindset ya kutokukuamini tayari

Jitahidi kumuomba Mungu akupe uamuzi sahihi zaidi
 
Ndo maana una miaka 29 na hujaolewa sababu hufai kuwa mke

Wewe na familia yako wote ni wazinguaji
 
Singo maza huo ujasiri uliutoa wapi!? Mtu keshamlipia mwanao na kakubali kumhudumia kama wake, possibly na kwenu alikuwa anawahudumia, huo ujasiri wa kuchagua ulichokichagua kwa hatua za mwisho uliutolea wapi hata kama nduguzo walijiweka kando nawe!? Mazafaka
 
mi sikuurumii maana kwa maamuzi yako ya kukurupuka hufai kuwa mke, plain truth

somo. Usihukumu kwa hatari ya Upande mmoja.
Ila kishingo Upande Polee sana, neema ya Mungu ikufunika
 
Miaka 29 ulinayo unafanya mambo bila kuangalia side effects sasa ukimkosa huyo mwanaume basi tena. Utajiingiza kuwa single mother mtarajiwa Kwa Hali inavyoonekana utakuepo single mother mtarajiwa
 
We mkorofi sana hufai hata kidogo.Kwani kuwa mke wa sita nini yani unasumbua wazee wa watu toka uyole hadi ngara halafu unawasusia kwani wao ndo walikuwa wanakuoa?Anyway em niambie ulifanikiwa kwenda,ulisamehewa?Umeolewa?Pole sana ila maisha yana mitihani sana.Usikurupukie kuolewa for the sake of.tafuta akupendaye umpende
 
Kijana yule namjua kiundani ni mpole mno ana Busara sana, najua ataweza kunisamehe ila sijajua namuanzaje na naianzaje familia yake
Usijidanganye kabisa.

SIKUSAMEHI HATA KIDOGO.
Nikikusamehe utanisumbua sana mbele ya safari.

We endelea na mambo yako tu.
 
Achana na hiyo ndoa, huko mbele mtavurugana sana, mama yako yupo sahihi, hata kama ukiomba msamaha mkaoana hamtakuwa na amani kwenye ndoa yenu.
Usilazimishe mambo
 
Inaonekana mama yake yupo sahihi anamjua mwanaye vema ndiyo maana katia ngumu, jua mama anapoint kwanini wafiche mtoto wa huyu binti kwa wazazi wa mwanaume hapo mama kaona mbali.
 
Kyusa haturembi,hatua hiyo iliyofikiwa ushukuru sana, ukaleta nyodo
Watu wanaendelea mbele tu,bahati yako umetoka Ngara huko ungekua jirani kishika uchumba tungekifata na mngetupa live.
Nenda huko ukaone namaanisha nini.
Otherwise nakushauri rudisha kwa tigopesa hela ya watu kama kuyajenga na kikolo anza upya ila hatakuamini tena.
Usiende
Alamsiki.
 
Unamwita mchumba wako mvulana. Yani unconsciously humchukulii kama mwanaume bali mvulana. Inakuwaje hajang'amua hili? Ana mushkeli.

Ndoa ni muunganiko wa familia, sio ninyi wawili tu. Hamuishi kwenye kisiwa. Ukweni wanatakiwa wajue kama una mtoto hata kama hawatakubaliana nalo. Halitawazuia kufunga ndoa. Mvulana wako anaonekana hana msimamo ni mtu wa kupelekeshwa ndio sababu hata anawaogopa ndugu zake.

Ulipanic kusikia kuwa ana mke na hukujua, mpaka kwa hasira ukasusa kwenda kwenye sendoff yako. Imagine panic ya wakwe kujua kwamba una mtoto na umewaficha.
 
Eti jamaa alishaanza hadi kumsomeshea mtoto, sijui naye ni bwege nazi gani tu... bora amedhalilishiwa ndugu zake huenda akazinduka!
Mpaka mchumba wake anamuita mvulana ... Imeniuma mno!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…