Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

Wanawake mna viherehere kuamini tu jambo usilokuwa na uhakika nalo kabla haujajiridhisha.Inaonekana una kiburi pia maana badala ungemtafuta uzungumze naye kuujua ukweli bado ukaamua kukaa kimya.Kiukweli umemuudhi sana mwenza wako kwanza kwa kutomuamini.Msamaha wako labda Mungu tu asaidie
 
Mimi ningekuwa huyo mchumba wako, ningekusamehe. Ila nisingekuoa tena huna sifa za kuwa mke Bora. Huna adabu, huna busara, huna hekima, unapenda umbea na majungu, huna uvumilivu.

Hata ukiolewa kwa tabia uliyoweza kuionesha mbele ya ndugu zake, hasa wazazi, hata ndoani mkiwa wenyewe unaweza kuirudia kwa kupenda na kuyaamini maneno ya uzushi na umbea.
Mbaya zaidi tayari amesharuka ruka sana ujanani mpaka na mtoto juu amepata (single mother)
 
Jamani mambo zenu, Niko katika wakati mgumu
Mimi ni binti wa miaka 29 kwa sasa, nimempata mwanaume ambaye tulipanga mengi sana hadi kupanga jinsi ya kufunga ndoa,

Mwaka fulani niliingia kwenye mahusiano na kijana mmoja toka Mbeya, ila kwa sasa anaishi Afrika ya Kusini kwa shughuli zake ,
Tulikubaliana kuanza kutambulishana kwao, na kwetu

Nakumbuka alinilipia nauli ya ndege nikaenda kwao kutambulishwa nikamshukuru Mungu kwamba nimepata mme sasa,

Tumeendelea na utaratibu na mshenga akatumwa kwetu kusema, baada ya kuondoka nikamweleza mama kuwa kijana sawa ananipenda ila hapendi jambo fulan ambalo kwa ukweli sitalisema hapa, mama akasema kama ndo hivo sitak habari zako za kuolewa,

Ikabidi mchakato uendelee kawaida, wakaleta kishika uchumba mama akawa hataki kushiriki hata kidogo, anasusa, sasa shangazi yangu akaniambia kwamba kwakuwa huna baba naomba ili suala tuwashirikishe baba wadogo na wajomba tuendelee na nchakato,

Baada ya muda tukapanga wataletaje mahari na siku ya send off tukaipanga,

Sasa kabla ya send off siku moja kabla tukapata habari kupitia kwa mjomba kwamba Mwanaume anayeenda kunioa kumbe ana mke mi naenda kuwa mke wa pili, taarifa hii ikawachanganya wote hata wajomba wakasema ngoja wajiweke pembeni, maandalizi ya send off yakavurugika wakati huo wakwe wakiwa njiani kuhudhuria sherehe hiyo , walikodi Costa na magari kadhaa kutoka mbeya hadi Ngara,

Wakanikimbia ndugu zangu wote nami nikachanganyikiwa kwa hasira sikutokea kwenye send off na maandalizi ikawa hasara, wakapiga simu nikazima nilikuwa na hasira sana,

Baadaye nikawasha simu nikakuta mama mkwe mtarajiwa amenitumia meseji kwamba "Sikutegemea kama ungetufanyia haya, sisi tunajiandaa kesho tunarudi lakini baki na amani"

Niliumia sana Akaendelea kunitumia meseji za machungu nikijua naye anajua kuwa Mwanae ana mke na mama huyu tumeongea kila siku niliumia,

Sasa yule mchumba wangu akawa ananitafta sipokei nikamwambia sina Muda mchafu wa kuolewa na wewe, hapo sikumwambia kwanini nimebadili mawazo,

Sasa nakumbuka siku kadhaa baadae naitwa nyumbani kwamba kuna kikao,

Kumbe kuna taarifa kwamba yule kijana hakuwa ameoa ila alichumbia sehemu akalipa mahari ila kumbe hakuoa,

Habari zilisononesha sana

Nikaenda kwa askofu mmoja akanishauri

1.Ama tuombe radhi kwao kuendelea na mchakato

2.Ama tuwape kishika uchumba chao maana mahari alikuwa bado angetoa siku ya send off asubuhi yake,

Naomba ushauri wenu plz

Nimeikosea Sana familia ile, pia hasira baada ya kupungua natamani niolewe naye japo nashindwa naanzaje
Duuuh kwahiyo ulichukua maamuzi ya kishenzi bila hata ya kumuuliza muhusika Kama ni kwel au uongo ?
Pole aisee ,ukisikia jambo jifunze tabia ya kutafuta ukwel kabla ya kuchukua hatua,
Hapo chamsingi endelea kupiga round kitaa unaweza bahatika kupata mwingine , Ila huyo Wa sasa jaribu tu kumsahau ,maana sijui ni Mani atakuja kuwaweka sawa hao wakwe zako
 
Ukimuomba msamaha akakusamehe...chunga sana! Huyo jamaa atakuja kukulipizia tukio zito zaidi ya hili la kusumbua wazazi wake na kumtia aibu bila sababu.

Mambo ya kiswahili hayo...kama umesikia issue kwanini usimuulize na umshirikishe maamuzi yako ili ajue la kufanya.

Hili umelikoroga, linywe tu
 
Anajifikiria mwenyewe huyu dada alisahau jamaa kakubali kuwa mume wa pili.
Nyongeza kidogo tu kuwasaidia single mazaz

1. Tambua mtoto/watoto ni kielelezo cha maisha yako ya ufuska kabla ya ndoa. Ni alama ya wazi kwamba umechakachuliwa peku na ukaridhika na kutoa yai, ukashika mimba na kuzaa.

2. Jambo hilo ni habari mbaya kwa mwanaume anayekuoa. Asingependa uwe hivyo. Linamsikitisha na itafaa ufanye kila juhudi asahau.

3. Namna nzuri ya kumsahaulisha ni kutomuweka karibu mtoto wako na mume huyo maana kila amuonapo mtoto mumeo atakumbuka habari mbaya kwamba ulishachojolewa mavazi yote na mwanaume mwengine aliyemuwahi, yeye anakula makombo. Mtoto ni kikwazo, akae mbali na mume wako. Mpeleke kwa bibi yake.

4. Usilazimishe mumeo aone suala la wewe kuwa na mtoto sio issue, NI ISSUE tena nzito.
 
Eti jamaa alishaanza hadi kumsomeshea mtoto, sijui naye ni bwege nazi gani tu... bora amedhalilishiwa ndugu zake huenda akazinduka!
Wahuni wamepiga mie nije kusomesha mtoto si uzuzu huu!!?? Bora nitafte dem Love Connect kuliko kuoa hawa "single problem"
 
Wewe ulienda kuchepuka siku ya send off na lijamaa likakushushia dozi hadi ukapitiwa ukalala, kuja kushtuka send off imevurugika. Hapa umeleta drama.
Ushauri:- achana na mambo ya ndoa , tuwekee namba yako hapa na sisi tuonje ulichonacho.
 
Jamani mambo zenu, Niko katika wakati mgumu
Mimi ni binti wa miaka 29 kwa sasa, nimempata mwanaume ambaye tulipanga mengi sana hadi kupanga jinsi ya kufunga ndoa,

Mwaka fulani niliingia kwenye mahusiano na kijana mmoja toka Mbeya, ila kwa sasa anaishi Afrika ya Kusini kwa shughuli zake ,
Tulikubaliana kuanza kutambulishana kwao, na kwetu

Nakumbuka alinilipia nauli ya ndege nikaenda kwao kutambulishwa nikamshukuru Mungu kwamba nimepata mme sasa,

Tumeendelea na utaratibu na mshenga akatumwa kwetu kusema, baada ya kuondoka nikamweleza mama kuwa kijana sawa ananipenda ila hapendi jambo fulan ambalo kwa ukweli sitalisema hapa, mama akasema kama ndo hivo sitak habari zako za kuolewa,

Ikabidi mchakato uendelee kawaida, wakaleta kishika uchumba mama akawa hataki kushiriki hata kidogo, anasusa, sasa shangazi yangu akaniambia kwamba kwakuwa huna baba naomba ili suala tuwashirikishe baba wadogo na wajomba tuendelee na nchakato,

Baada ya muda tukapanga wataletaje mahari na siku ya send off tukaipanga,

Sasa kabla ya send off siku moja kabla tukapata habari kupitia kwa mjomba kwamba Mwanaume anayeenda kunioa kumbe ana mke mi naenda kuwa mke wa pili, taarifa hii ikawachanganya wote hata wajomba wakasema ngoja wajiweke pembeni, maandalizi ya send off yakavurugika wakati huo wakwe wakiwa njiani kuhudhuria sherehe hiyo , walikodi Costa na magari kadhaa kutoka mbeya hadi Ngara,

Wakanikimbia ndugu zangu wote nami nikachanganyikiwa kwa hasira sikutokea kwenye send off na maandalizi ikawa hasara, wakapiga simu nikazima nilikuwa na hasira sana,

Baadaye nikawasha simu nikakuta mama mkwe mtarajiwa amenitumia meseji kwamba "Sikutegemea kama ungetufanyia haya, sisi tunajiandaa kesho tunarudi lakini baki na amani"

Niliumia sana Akaendelea kunitumia meseji za machungu nikijua naye anajua kuwa Mwanae ana mke na mama huyu tumeongea kila siku niliumia,

Sasa yule mchumba wangu akawa ananitafta sipokei nikamwambia sina Muda mchafu wa kuolewa na wewe, hapo sikumwambia kwanini nimebadili mawazo,

Sasa nakumbuka siku kadhaa baadae naitwa nyumbani kwamba kuna kikao,

Kumbe kuna taarifa kwamba yule kijana hakuwa ameoa ila alichumbia sehemu akalipa mahari ila kumbe hakuoa,

Habari zilisononesha sana

Nikaenda kwa askofu mmoja akanishauri

1.Ama tuombe radhi kwao kuendelea na mchakato

2.Ama tuwape kishika uchumba chao maana mahari alikuwa bado angetoa siku ya send off asubuhi yake,

Naomba ushauri wenu plz

Nimeikosea Sana familia ile, pia hasira baada ya kupungua natamani niolewe naye japo nashindwa naanzaje
Omba msamaha na rudisha kishika uchumba, hamtakuwa na amani kamwe kama mtaendeleza mahusiano.
Mawasiliano ni muhimu sana katika mahusiano, wewe unahasira, unazira, wakati mwenzako hata hajui sababu, na wewe unaona ni sawa?
 
Mwabamke mjinga huvunja nyumba kwa mikono yake mwenyewe,,
Shukuru hata umepanda ndege ,endelea kuwasimulia nduguzo ujinga mlioudanya bila tafakuri ya yoyote
 
Kuna watu huwa wanasema kuwa Single Mothers mna matatizo sana.

1. Umepata taarifa kuwa jamaa ana mke, kwa nini usitafute ushahidi kwa Kumuuliza mhusika?

2. Ndoa haikufai maana kama unaamua kwa kusikia utaenda kuleta matatizo zaidi kwenye ndoa.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwa namna ya maelezo yako ni wazi kuwa
1. Familia yako ina matatizo ya kufikiri na kuamua mambo
2. Wewe mwenyewe una matatizo ya kufikiri na kuamua mambo.

Kwa sasa utulie ili kulea mtoto, hilo lishapita maana ndugu wa Dismas wameshajua kuwa una mtoto.

Pole sana.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Jamani mambo zenu, Niko katika wakati mgumu
Mimi ni binti wa miaka 29 kwa sasa, nimempata mwanaume ambaye tulipanga mengi sana hadi kupanga jinsi ya kufunga ndoa,

Mwaka fulani niliingia kwenye mahusiano na kijana mmoja toka Mbeya, ila kwa sasa anaishi Afrika ya Kusini kwa shughuli zake ,
Tulikubaliana kuanza kutambulishana kwao, na kwetu

Nakumbuka alinilipia nauli ya ndege nikaenda kwao kutambulishwa nikamshukuru Mungu kwamba nimepata mme sasa,

Tumeendelea na utaratibu na mshenga akatumwa kwetu kusema, baada ya kuondoka nikamweleza mama kuwa kijana sawa ananipenda ila hapendi jambo fulan ambalo kwa ukweli sitalisema hapa, mama akasema kama ndo hivo sitak habari zako za kuolewa,

Ikabidi mchakato uendelee kawaida, wakaleta kishika uchumba mama akawa hataki kushiriki hata kidogo, anasusa, sasa shangazi yangu akaniambia kwamba kwakuwa huna baba naomba ili suala tuwashirikishe baba wadogo na wajomba tuendelee na nchakato,

Baada ya muda tukapanga wataletaje mahari na siku ya send off tukaipanga,

Sasa kabla ya send off siku moja kabla tukapata habari kupitia kwa mjomba kwamba Mwanaume anayeenda kunioa kumbe ana mke mi naenda kuwa mke wa pili, taarifa hii ikawachanganya wote hata wajomba wakasema ngoja wajiweke pembeni, maandalizi ya send off yakavurugika wakati huo wakwe wakiwa njiani kuhudhuria sherehe hiyo , walikodi Costa na magari kadhaa kutoka mbeya hadi Ngara,

Wakanikimbia ndugu zangu wote nami nikachanganyikiwa kwa hasira sikutokea kwenye send off na maandalizi ikawa hasara, wakapiga simu nikazima nilikuwa na hasira sana,

Baadaye nikawasha simu nikakuta mama mkwe mtarajiwa amenitumia meseji kwamba "Sikutegemea kama ungetufanyia haya, sisi tunajiandaa kesho tunarudi lakini baki na amani"

Niliumia sana Akaendelea kunitumia meseji za machungu nikijua naye anajua kuwa Mwanae ana mke na mama huyu tumeongea kila siku niliumia,

Sasa yule mchumba wangu akawa ananitafta sipokei nikamwambia sina Muda mchafu wa kuolewa na wewe, hapo sikumwambia kwanini nimebadili mawazo,

Sasa nakumbuka siku kadhaa baadae naitwa nyumbani kwamba kuna kikao,

Kumbe kuna taarifa kwamba yule kijana hakuwa ameoa ila alichumbia sehemu akalipa mahari ila kumbe hakuoa,

Habari zilisononesha sana

Nikaenda kwa askofu mmoja akanishauri

1.Ama tuombe radhi kwao kuendelea na mchakato

2.Ama tuwape kishika uchumba chao maana mahari alikuwa bado angetoa siku ya send off asubuhi yake,

Naomba ushauri wenu plz

Nimeikosea Sana familia ile, pia hasira baada ya kupungua natamani niolewe naye japo nashindwa naanzaje
The worst thing ever katika maisha ni kupewa taarifa na kurukia kwenye conclusion.

Unamuhukumu mtu bila hata kumuuliza yeye mwenyewe? Surely?

Me sijui hata nikushauri nini.
 
Kwanini mlivyopata habari jamaa kaoa hamkuwaambia wahusika ili wasitishe safari? Wewe na ukoo wako mnatabia mbaya
Tena siyo kidogo. Yaani tabia mbaya mno. Unapata taarifa za mtu unakimbilia kufanya maamuzi?

Bila hata kuwashirikisha wahusika?
 
Mbeya mpaka Ngara.. mnaroho mbaya sana ninyi.. haswa wewe no utu.. eti ukaolewe huko tena.. subiri mume mwingine.. ukienda kujisukuma huko usirudi kutusumulia humu majanga yake.. kumbuka Mjomba alikusaidia wewe na Mama yako mfikie lengo la kutotaka kuolewa naye.. utafikiri hakuwa mume mtarajiwa.. hukuongea nae kujua ukweli.. humupendi huyo mwanamume.. usimusingizie Mjomba wako na wengine.. tatizo ni wewe
 
Back
Top Bottom