Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

Huu uzi niliuona toka jana ila sikutaka kuufungua. Kila nikipita nauona unatrend hivyo nimeona acha na mimi niufungue nione kuna nini. Ninachoweza kuchangia ni hiki "Mleta mada wewe ni fala na katiri sana, hustahili kuishi kwenye jamii ya watu waliostaarabika, na ndio maana aliyekuzalisha alikuacha".
 
Send off ilikuwa tarehe 10 taarifa zinatoka tarehe 8 wakati wameanza safari tarehe 7 Kutoka mbeya, nilimtext mvulana kuwa wasitishe wakati huo wameshafika Kahama,

Suala ambalo mama na mimi tulitofautiana ni baada ya kumweleza mchumba wangu kwamba nina mtoto akasema mi ndo naoa kwakuwa nimekukubali ukiwa na mtoto hakuna shida ila akaomba mtoto atamlea na kumsomesha na ameshamlipia ada ya primary one ya mwaka mzima niwe mkweli, ila akanisihi nisiwajulishe kwao kama mi nina mtoto, hapo ndio mama akakazania kwamba lazima wajue, nikamsihi mama kwamba anayenioa kashamkubali mtoto na anamhudumia ila kwao wataleta mapingamizi nikiwaambia muda huu, hivyo kasema tutawaambia mbeleni, mziki ukaanzia hapo mama akajitoa
Hufai kuwa mke wewe,unamaamuzi ya papara ,nadhani Mungu kamuepusha jamaa na majanga makubwa dhidi yako,unakataa kuolewa na mtu mwenye mke huku ukiwa huna ushahidi kuwa ana mke au laah,huku wewe ushahidi upo wazi kuwa una mtoto.

Tena kwa ubaya zaidi hutaki wakwe zako wajue kuwa ushawahi zaa,hujui kuwa hili litaleta baraa katika familia ya Mme pindi wakijua kuwa ulishawahi zalishwa.

Mwisho nakushauri uachane na kijana Wa watu,tafuta mtu Wa saizi yako,tambua pia ukweni hawana imani na wewe tena vyovyote iwavyo kamwe hawawezi kukuamini na kukuona wewe mtu Wa thamani kwa haya uliyofanya.
 
Naona umeamua kuja kuthibitisha hapa sababu ya kuzalishwa na kuachwa. Kwa namna yoyote ile huyo jamaa hatakiwi kukukubali tena. Pole sana
 
Mungu akupige laana we dada yaani uvimbe hata jipu katkati ya matak* Jinga sana we dada alafu unataka ushairiwe nini sasa...
 
Usithubutu kuolewa nae kwanza kwa mwanaume timamu hawezi kukuoa tena..

Kaombe msamaha familia yao endelea na maisha yako..

Nahisi km jini mkata kamba aliwapitia hivi
 
Kwanini mlivyopata habari jamaa kaoa hamkuwaambia wahusika ili wasitishe safari? Wewe na ukoo wako mnatabia mbaya

naunga hoja mkono mlishindwa vip kutoa taarifa kwa wahusika hasira hasara dada umevuna ulichopanda
 
Ulivyopata habari tu kama kaoa ama la ungemface kumuuliza, upumbavu ni wako...
ashafeli kuwa mke bila kuingia kwenye ndoa sikulaumu ila umewapa watu kuyapokea yao hvi unafikri kijan watu alipitia wakat gani embu jiulize.......
 
Waelezee ukweli wakwe zako kwanini ulikimbia, sababu za wewe kukimbia zinaeleweka, kuoa au kuolewa siku hiz ni bahati, kajaribu bahati yako ndoa ni kujipanga coz waliopo kwenye ndoa wanatamani kutoka
Angewaambia tatizo kuliko kuwaacha kwenye mataa

Wanyakyusa hatupendi dharau

Asijisumbue
 
Na kama mjomba ndio alifanya hayo lazima yametoka kwa mama asiyeitaka ndoa
 
Hufai kuwa mke wewe,unamaamuzi ya papara ,nadhani Mungu kamuepusha jamaa na majanga makubwa dhidi yako,unakataa kuolewa na mtu mwenye mke huku ukiwa huna ushahidi kuwa ana mke au laah,huku wewe ushahidi upo wazi kuwa una mtoto.

Tena kwa ubaya zaidi hutaki wakwe zako wajue kuwa ushawahi zaa,hujui kuwa hili litaleta baraa katika familia ya Mme pindi wakijua kuwa ulishawahi zalishwa.

Mwisho nakushauri uachane na kijana Wa watu,tafuta mtu Wa saizi yako,tambua pia ukweni hawana imani na wewe tena vyovyote iwavyo kamwe hawawezi kukuamini na kukuona wewe mtu Wa thamani kwa haya uliyofanya.
Sijui wanawake wamekaririshwa na nani hii aina ya wivu. Wewe una mtoto ambaye hukuzaa na huyo mume mtarajiwa. Kwa upendo wake akaamua kukupokea wewe na mwanao na alijua kabisa hapa sio hadhi yake. Wewe kusikia tu ana mke tena bila uthibitisho unamblock na hasara ya maandalizi kwa upande wa mume mtarajiwa. Wamechangishana weee ila ukaona ni jambo dogo tu usimtafute na kujidhihirishia. Wallah ningekuwa mimi huyo mwanaume eti unakuja kuniomba msamaha ungeangukia kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi. Kuna watu wana maudhi hata unajiuliza walizaliwa kwa ajili gani. By the way baba wa mtoto ulimpa taarifa kuwa unaolewa?
 
Yani wewe single maza afu unauchukia uke wenza.... Mungu anakuona ujue.

Ila Mungu hamtupi mja wake,hakuna kinachotokea kwa bahat mbaya....uyo jamaa ashukuru sana.
 
Jamani mambo zenu, Niko katika wakati mgumu
Mimi ni binti wa miaka 29 kwa sasa, nimempata mwanaume ambaye tulipanga mengi sana hadi kupanga jinsi ya kufunga ndoa,

Mwaka fulani niliingia kwenye mahusiano na kijana mmoja toka Mbeya, ila kwa sasa anaishi Afrika ya Kusini kwa shughuli zake ,
Tulikubaliana kuanza kutambulishana kwao, na kwetu

Nakumbuka alinilipia nauli ya ndege nikaenda kwao kutambulishwa nikamshukuru Mungu kwamba nimepata mme sasa,

Tumeendelea na utaratibu na mshenga akatumwa kwetu kusema, baada ya kuondoka nikamweleza mama kuwa kijana sawa ananipenda ila hapendi jambo fulan ambalo kwa ukweli sitalisema hapa, mama akasema kama ndo hivo sitak habari zako za kuolewa,

Ikabidi mchakato uendelee kawaida, wakaleta kishika uchumba mama akawa hataki kushiriki hata kidogo, anasusa, sasa shangazi yangu akaniambia kwamba kwakuwa huna baba naomba ili suala tuwashirikishe baba wadogo na wajomba tuendelee na nchakato,

Baada ya muda tukapanga wataletaje mahari na siku ya send off tukaipanga,

Sasa kabla ya send off siku moja kabla tukapata habari kupitia kwa mjomba kwamba Mwanaume anayeenda kunioa kumbe ana mke mi naenda kuwa mke wa pili, taarifa hii ikawachanganya wote hata wajomba wakasema ngoja wajiweke pembeni, maandalizi ya send off yakavurugika wakati huo wakwe wakiwa njiani kuhudhuria sherehe hiyo , walikodi Costa na magari kadhaa kutoka mbeya hadi Ngara,

Wakanikimbia ndugu zangu wote nami nikachanganyikiwa kwa hasira sikutokea kwenye send off na maandalizi ikawa hasara, wakapiga simu nikazima nilikuwa na hasira sana,

Baadaye nikawasha simu nikakuta mama mkwe mtarajiwa amenitumia meseji kwamba "Sikutegemea kama ungetufanyia haya, sisi tunajiandaa kesho tunarudi lakini baki na amani"

Niliumia sana Akaendelea kunitumia meseji za machungu nikijua naye anajua kuwa Mwanae ana mke na mama huyu tumeongea kila siku niliumia,

Sasa yule mchumba wangu akawa ananitafta sipokei nikamwambia sina Muda mchafu wa kuolewa na wewe, hapo sikumwambia kwanini nimebadili mawazo,

Sasa nakumbuka siku kadhaa baadae naitwa nyumbani kwamba kuna kikao,

Kumbe kuna taarifa kwamba yule kijana hakuwa ameoa ila alichumbia sehemu akalipa mahari ila kumbe hakuoa,

Habari zilisononesha sana

Nikaenda kwa askofu mmoja akanishauri

1.Ama tuombe radhi kwao kuendelea na mchakato

2.Ama tuwape kishika uchumba chao maana mahari alikuwa bado angetoa siku ya send off asubuhi yake,

Naomba ushauri wenu plz

Nimeikosea Sana familia ile, pia hasira baada ya kupungua natamani niolewe naye japo nashindwa naanzaje
Mpaka hapo wewe jiandae kuwa single mother tu, sahau habari za ndoa,maana kwa ulichowafanyia ndugu zangu has ka nakwambia maumivu yao utayabeba mpaka unazeeka!

Ila pole kwa kufanyia kazi habari za kuambiwa bila kufanya uchunguzi binafsi

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
Send off ilikuwa tarehe 10 taarifa zinatoka tarehe 8 wakati wameanza safari tarehe 7 Kutoka mbeya, nilimtext mvulana kuwa wasitishe wakati huo wameshafika Kahama,

Suala ambalo mama na mimi tulitofautiana ni baada ya kumweleza mchumba wangu kwamba nina mtoto akasema mi ndo naoa kwakuwa nimekukubali ukiwa na mtoto hakuna shida ila akaomba mtoto atamlea na kumsomesha na ameshamlipia ada ya primary one ya mwaka mzima niwe mkweli, ila akanisihi nisiwajulishe kwao kama mi nina mtoto, hapo ndio mama akakazania kwamba lazima wajue, nikamsihi mama kwamba anayenioa kashamkubali mtoto na anamhudumia ila kwao wataleta mapingamizi nikiwaambia muda huu, hivyo kasema tutawaambia mbeleni, mziki ukaanzia hapo mama akajitoa
Mama yako anaona mbali Kuna kitu kikubwa Sana hapo umeepushiwa bila kujua just move on haikua riziki yako!!
 
Wa kwanza kulaumiwa ni wewe wa pili ni ndugu zako hamkuwa na umoja ili kumaliza jambo lenu
 
Back
Top Bottom