Naomba ushauri, ninunue pikipiki au nifungue library ya kuingiza movie katika flash? (nina Tsh. milioni 1. 2)

Acha kumuingiza Chaka mwenzio, library ya muziki inalipa sana uswahilini
 
Wana Jukwaa,

Ubungo au Keko kuna pikipiki used aina ya Boxer au TVS. Lakini pia nina wazo la kufungua maktaba (library). Je, kati ya biashara hizo mbili, ipi itanipa kipato cha uhakika kwa mtaji wa takribani milioni 1.2?

Asanteni.
Sijajua machine ya kunyoa ni bei Gani ila ungetafuta frame kubwa uweke desktop au laptop ya kuweka muvi na uwe na kijana wa kunyoa ambaye kutokana na mwanzo mgumu labda mtalipana kwa kichwa... Mfano: kunyoa kama ni 1,000# unampa labda 400 wewe 600# kwa namna utakavyoona inafaa.
 
Ushauri wangu fungua library ya kisasa, movie zako ziwe na ubora wa kutosha, achana na mamb ya cd, Sasa hiv watu wanaweka movie kwenye flash, tumia social media km inst na whtsp kujitangaza, unaweka movie mpya ambazo zimetoka.

Wakat unapiga hyo kazi uwe unatafuta lain za m pesa, t pesa, Airtel money, nk. Kwahyo badae utaongeza huduma ya kutoa na kuweka pesa.

Kama ni kweli wewe ni mpambanaji basi itafika muda utaitanua huduma kwa kuuza vitu km flash, charger za simu, nk..
 
Wana Jukwaa,

Ubungo au Keko kuna pikipiki used aina ya Boxer au TVS. Lakini pia nina wazo la kufungua maktaba (library). Je, kati ya biashara hizo mbili, ipi itanipa kipato cha uhakika kwa mtaji wa takribani milioni 1.2?

Asanteni.
Nakushauri uchukue hiyo 1.2M ukalipe ada usome VETA ili akili ikae sawa kwanza. Mambo mengine baadae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…