Naomba ushauri, ninunue pikipiki au nifungue library ya kuingiza movie katika flash? (nina Tsh. milioni 1. 2)

Ushauri wowote ambao hauhusiani na pikipiki nenda nao achana na mawazo ya pikipiki ata kama kuna watu unawajua wanafaidika achana na hayo mawazo yani usiwaze kuhusu pikipiki.
 
Nenda kwa makampuni kama "watu";
Chukua pikipiki used na weka deposit 200,000 au kutegemeana na ubora wa pikipiki husika.
Marejesho kila siku hayazidi 6,000.
Tafuta maeneo yenye muingiliano mzuri, tafuta kijiwe(wanalipia vijiwe hadi 500,000).
Ingia road mwenyewe upambane.
Funga zipu.
Usitumie mihadarati.
Usitumie kilevi.

Nakuhakikishia baada ya muda utayaona matunda yake.

Pesa itakayokuwa imebaki fanya mambo mengine(umesema una 1.2m mkononi).
 
Pikipiki kama huendeshi mwenyewe achana nayo, its wastage of money.
 
hujachelewa boss
 
ndio boss
 
Ushauri wowote ambao hauhusiani na pikipiki nenda nao achana na mawazo ya pikipiki ata kama kuna watu unawajua wanafaidika achana na hayo mawazo yani usiwaze kuhusu pikipiki.
Naomba unipe ufafanuzi juu ya risk ya pikipiki boss
 
asante mkuu
 
Sina uzoefu na libraly pia sina uzoefu na boda hila ni bora ufungue libraly upate eneo sahihi la biashara pia itajenga heshima una amka asubh unaenda ofisini mwako kuliko boda asa dar unatakiwa uwe makini sana ukijipanga vizur kuanzisha libry ni chaguo zuri lakini sehemu ya uswahilin au njian
 
NAKUSHAURI FUNGUA LIBRARY.
Ni nzuri kama ukipata ambayo inauzwa ingawa bei yake itakuwa 1.3m mpaka 1.5m
endapao ukianzisha ya kwako kuna gharama zifuatazo:
a) kioo 24 inch 140000 b) cpu koa 5 240000 c) external 12TB 360000.
d) speaker airliang 450
000.
e)meza ,kiti,makasha, na kulipa kodi tufanye 300000.=149,000/=
la kuzingatia jitahidi uwe na vioo viwili kwa ajili ya uharaka wa kazi.
 
ENEO NA MAPATO.

ENEO

Eneo ni zuri kama utakuwa pembezoni mwa mji,na hii ni kwa sababu huko ushindani unakuwa ni mdogo pia mama wa nyumbani ni wengi.

MAPATO.
Hapo itategemea kwanza uaminifu wa mfanya kazi ,si ajabu kwa siku ukatapa kama elfu14 hadi 16.

GHARAMA ZA UENDESHAJI

Umeme elfu 28 kwa mwezi

Kodi elfu 30 kwa mwezi.

Hela ya kununua muvi kwa maagenti elfu7 hadi 15 kwa wiki.

Mfanya kazi elfu 50 kwa mwezi.=168,000/=

Chakula cha mfanyakazi hapo wewe ndio utampangia kutokana na eneo husika.

Unashauriwa umtafute kijana ambae anaish kwao kiufupi asiwe na majukumu ya kifamilia.

Ukiwa pazuri na kuitunza vizuri ,kupata laki mbili kwa mwezi ni kawaida.
 
Njoo pm nikupe madini kama utachagua ishu za library...

Ukija uwe na pesa ya maji
 
Uuuuuuuuu hatareeee hatareeee thanaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…