Naomba ushauri, ninunue pikipiki au nifungue library ya kuingiza movie katika flash? (nina Tsh. milioni 1. 2)

Naomba ushauri, ninunue pikipiki au nifungue library ya kuingiza movie katika flash? (nina Tsh. milioni 1. 2)

Mtu kaomba kujua kati ya pikpik au library we unaleta biashara nyingine ya machuma chuma ebu kua serious acha ujuaji
Nunua welding machine angle grinder na drill ufungue goli uwe unachomelea riziki utapata mkuu
 
Tafuta eneo lenye mzunguko mzuri, Anza biashara ya nafaka Mchele, Unga, maharagwe, dagaa mafuta! Hapo uhakika kabisa pesa yako.
2. Eneo lenye mzunguko wa watu andaa jiko lako safiii unachoma mishkaki, nyama choma miksa na soseji na ndizi chapu kwa haraka utakuja kunishukuru.
3. Kama sio bishoo nunua jiko la ges maalum kwaajir ya chapati, uwe na Meza moja viti 4 kuanzia unapika supu ya kuku na chapati asubuh na jion.
4. Ukipata mdada mtafutaji mwenye hasira anayejua kupika vitumbua dili nae awe anapika asubuh na jion pamoja na maziwa! "simple Sana kwa mtaji mdogo.
5. Usipokuwa mvivu na bishoo tafuta shule 2 dili na vishet vya 100 kwa watoto, kwa siku unauhakika wa kukata mifuko 2 ya ngano na unauhakika wakuingiza 30000/50000 kwa siku kulingana na idadi na ubora wa vishet vyako,, ni swala la kuwa na hasira na usiliazi. Achana na mapikipiki uwe mlemavu, uibiwe, uzurumiwe, ukamatwe, iharibike ni umasikini mtupuuuuu. Hrf ondoa mawazo ya kitoto mtu ambaye yupo serious kabisa unawaza library ya kuingiza nyimbo? Are serious? Fanya vitu ambavyo kwa age yako hawawez kufanya na unapiga pesa! Usimaindi mkuuu nakupa uhalisia ulivyo
Watu kama nyie mnakera ..alf mnajidai wajuaji kumbe hakuna kitu ,,biashara unazomshauri na library anayotaka kufungua unaona vinaendana ?
1.mtu anafanya kitu anachopenda ndio ataeza kukisimamia vizur alaf vitu anavotka haviitaji usimamizi mkubwa Wala havichukui mda wake mwingi kuvifatilia hii inamfanya afanye hata kazi zingine
Pili library hupat hasara movie hata uwarushie watu 100 haiaribiki na unaweza uza hata movie za mwaka 1990 ila kitumbua Cha juzi huezi muuzie mteja
 
Nina uzoefu juu Hilo mkuu, nilimpa kijana boda yangu akaendesha wiki 2 tu akaipiga chini,hizo gharama siyo poa kaka..taa kubwa, dashboard,foot rest, na hapo Hela aliyoleta Kwa wiki 2 haitoshi kununua hivyo vyote
Hawa vijana wa siku hizi wanachukulia maisha poa sana
 
Chukua pikipiki na ukomae nayo wewe mwenyewe.

Ukiwa na nidhamu na kazi yako pamoja na nidhamu ya pesa utafanya la maana zaidi.

Kufungua library ni kutengeneza kijiwe cha kupigia soga tu.
Umemaliza kila kitu.
 
Sijajua machine ya kunyoa ni bei Gani ila ungetafuta frame kubwa uweke desktop au laptop ya kuweka muvi na uwe na kijana wa kunyoa ambaye kutokana na mwanzo mgumu labda mtalipana kwa kichwa... Mfano: kunyoa kama ni 1,000# unampa labda 400 wewe 600# kwa namna utakavyoona inafaa.
Ushauri mzuri huu.
 
Nunua pikipiki. Hii ina uhakika wa kupata pesa kuliko Library. Kwa technolojia ya sasa watu wanapata movies na music kwa urahisi mitandaoni kuliko kwenda Library.

Ushauri wangu nunua pikipiki mkuu. Kikubwa uwe na nidhamu barabarani na nidhamu ya pesa.
Kama yupo Mbeya atapiga hela,Isanga,Mama John,Karibia sehemu nyingi niliona hiki kitu na kina watu kwa jioni.
Kuna watu wachache sana wanajua habari za netflx,Torrents..
 
Acha kumuingiza Chaka mwenzio, library ya muziki inalipa sana uswahilini
Nimetoa reference,nilikuwa Mbeya nimeona sana hiki kitu.
Kuna ofsi nilienda kubwa tu,wafanyakazi wanasimulia Squid game na mpaka wanapoenda kuichukua😀😀
Nikasema nisiwe mmbeya kusema kuna netflx nitakata ugali wa mtu.
Mdada amekusanya flash huyo kaenda kwa Library😀😀😀
 
ikitokea umenunua pikipiki jiepushe na wake za watu, matumizi ya madawa ya kulevya na kusafirisha magendo
 
Kwa maktaba hela haitatosha kwa sababu itakubidi ununue kompyuta na fremu ya biashara vitagharimu zaidi ya hiyo 1.2m
 
Wengi mnashaurinlakinibhamjawwhi kufanya hizo kazi NI kwa kuangalia nnje tu...Kama umri unaruhusu fungua movie libray...unamda wa kuziangalia na kujua wahusika watoto watoto ndio wanajua Kama Kuna biashara Kama hio mi nilikuwa sijui naonaga tu vyumba vimejaa cd...mpaka mmoja wao alipokuja kuomba ushauri na kujifunza Adobe ndio nikamdodosa na kwenda kwenye ofisi yake anapoga kazi...na haiztaki location ya usoni sana kwenye makazi ya wamama wanaoshinda nyumbani Kuna movie kibao wanazifuatilia naingizo yake NI Kama kupiga photocopy tu..movie moja Mia mbili Hadi Mia tana unategemea imetoka lini na inahitajika kivip...wanauza soft copy...hii biashara nilishawahi kufanya enzi hizo tunaburn CD music na kurusha kwenye simu...we ni kuwa na umeme tu...kazi imeisha kitoto Toto unaweza maana MTU anakuja anakuimbia au kuniambia kipande inabidi ujue anataka Nini...boda sijawahio kufanya kwa kweli na naziogopa
 
Pikipiki inalipa ila usimamizi wa karibu muhimu sana. Mimi nilinunua nikampa mtu kwa mkataba.
Alikuwa analipa vizuri tu mpaka nikashawishika kununua ya pili.
Dahh! Miezi miwili Nyuma dogo akaanza sarakasi za kijinga nikamfuatilia nikagundua alishaanza kunywa pombe Hadi akawa anashindwa kulipa pesa.

Niliamua kuchukua Pikipiki na kuuza kabisa maana Mimi situmii.

Ukitaka ule loss nunua Pikipiki mpya halafu tukutane na dereva mpuuzi utajuta.
Maisha ni uangalifu na kupanga mikakati thabiti.

Mimi nakushauri hivi;
Kama dereva ni "wewe mwenyewe" basi nunua Pikipiki kama sivyo utapoteza pesa.
 
Kwani kabla hajaipata hiyo hela alikuwa anaishije mkuu? Ni uhakika huo ni mtaji wake siyo hana hela ya kujikimu kama ni hivyo hata kwenye boda aombee mema asipate changamoto yoyote......
Ni mkazi wa mjini daslam, ina maana hapo kabla alikua anapiga mishe zake hapo mjini, kumpeleka huko ndichi hizo mishe atapigaje na inabidi asimamie shamba ambalo kwa miezi kadhaa hana hakika kama atapata kitu
 
Sijui nimechelewa, ila Sikiliza, Fungua wakala, hata kabanda, alafu tenga 250,000 kanunue charge , sijui earphone zile vijaze na makava. Achana na Cd na hiyo boda.
Upatu ujao ndio weka CD, uwe unawekea watu miziki na Printer. Hutolala njaa.
Au fungua kabisa saloon ya kiume.
Saloon ya kiume tayari boss
 
Back
Top Bottom