Chendembe
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 444
- 488
Salaaam.
Nimekuwa na changamoto katika maisha yangu na familia yangu.
1. Nilikuwa nimeowa mke wa kwanza 1996 na kubahati kuishi kwa miaka 9 ivi na kupata watoto 3. Lakini, ikaja changamoto mke akawa ananishutumu kuwa nawatuma watu wamzalilishe, akawa anakosa amani aliamini kuwa nawatuma watu wamchungulie Hadi chooni/bafuni na hata tunapolala. Nikamuacha kwa kuamini alikuwa analengo lake. Lakini baada ya kuachiwa Hali yake ikawa mbaya zaidi na kuwa mtu aliechanganyikiwa.
2. Nikaowa Tena 2003, lakini baada ya miaka Kama Saba Hali ya yule mke wa kwanza ikajitokeza kwa huyu na kupelekea kukosa Furaha ya ndoa. Amekuwa anasikia na kusema Mambo ambayo wengine tunashangaa tu na ngumu kuamini. Anaweza kuwa ndani lakini akakuambia watu wanamzomea au wanamtuka nje bila wengine kusikia
Mbaya zaidi kunasiku akaamka na kuniambia kuwa ameota kuwa na jitu kubwa na lilimwambia yeye ni mkubwa na aniambie nimwaache. Baada ya mwezi, anadai kuachwa. Naogopa kumwacha kwakuhofia lile la mke wa awali.
3. Wakati napambana na Hilo, mwaka juzi mtotowangu alitoka nyumbani nilikozaliwa na kuanguka na pikipiki na lakini hakuumia sehemu yoyote ile lakini alisema alishangaaa tu ameanguka na hakuwa anajielewa na kujikuta tu anaburuza pikipiki kwa mda mrefu na baada ya kupata fahamu akawasha na kurudi nyumbani anakoishi. Toka siku hiyo akawa anaongea Mambo ambayo ni ngumu kuelewa, atoki ndani mchana na kuchukia kuwa karibu na watu.
Naomba Allah akuongoze kunishauri Hilo maana linanikosesha amani. Naomba saana kwa Allah Ila nakosa maarifa ya kutafakari ndoto zangu.