Naomba ushauri wa biashara ya malori

Ahsante Mkuu, kama gari yangu binafsi nimekata comprehensive nikijua manufaa yake basi bila shaka hii gari ya biashara itafuata mkumbo huo. Ahsante kwa kunikumbusha.
 
Mkuu nimeulizia HOWO na FAW mpya kabisa. Naona zimesimama sana bei. Hapo kwenye trailers sasa nimekuelewa vema. Ahsante
 
Volvo na MAN sio gari za kichina Mkuu.
 
Mkuu mm Sina utaalamu Sana wa hayo magari japo na watu wangu wengi wanayo Kuna mmoja alinunua horse pekee Ila trailer akakodisha Ila safari zake nyingi Ni za trip town Hapa Hapa Ila chakushauri tafute Gari nzuri na imara japo ulivosema Gari hii Ni ya kwanza BC uhakikishe Una Nunua yenye hali nzuri Sana na tafuta dereva mwaminifu mzuri sio haya janja janja Mara aibe mafuta na spare zingne, ikiwezkana funga camera kabsa Kama wanavofanya superdoll, siku zote kwenye hizi biashara hakikisha Una Kama 1-5mil hio weka pembeni kwaajili ya emergency na let's say kwa siku umelaza 300k faida BC nusu weka kwa ajili ya Gari matengenezo n.k all in all nakutakia mafanikio mema
 
Ahsante sana Mkuu, nimepokea vema ushauri wako
 
Hizo pia ni gari za Europe
Hata mimi naunga mkono chukua scania used europe 124 na trela ya kukodi kwanza usome game maana una uhakika wa mizigo.
Ila inata mda wa kifuatilia Sana Ili wengine wasitajirike badala yako.
Kata bima kubwa,
Biashara zote ni changamoto mafanikio ni kutokata tamaa
 
Achana na hiyo biashara!
Kama utaziweza hizi changamoto try!
1-Ale dereva!
2-Ale msaidizi!
3-Ile gari!
4-Ile serekali!
5-Ale dalali!
6-Ale Trafic
Kitakacho fika kwako sound!....

Wekeza kwenye kilimo cha Kitaalamu!
Heheee..umeanza vzr ila uliposema kilimo nimeshituka.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nilikuwa mbishi kwenye biashara hiyo hadi niliitwa betri na vijana!
Kilichotokea magari yalipo haribika walaji woote wakasepa na kuniacha na magari yangu mabovu kunguru wanayanyea[emoji24]
[emoji24][emoji24]
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…