Corosive
JF-Expert Member
- Oct 16, 2020
- 1,460
- 2,908
Kwema mkuu,hongera kwa jitihada,,kwa kua tayar una ka mtaji kadogo,jaribu kuagiza horse ya mtumba thn tafuta taratibu za kukod trailer,ukishafanikiwa kuusoma mchezo utaona mwenyewe kwamba nikikopa ela ya trailer ntaweza kurejesha?Wakuu nawasalimu kwa Jina la JMT.
Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza. Nimekuja humu ndani kupata ushauri wa Biashara ya Malori haya ya kubeba mizigo iwe ya Local ama Transit.
Kutokana na Connection nilizonazo nadhani suala zima la kupata Mizigo ya Kusafirisha halitokuwa la kuumiza kichwa.
Changamoto inayonikabili ni funding pamoja na aina ya truck ambayo inapaswa ni nunue.
Kabla ya kuja humu ndani nilishaomba ushauri kwa watu kadhaa ambao wapo kwenye hii industry na wamenijuza truck nzuri ya kununua ni Mtumba SCANIA 124 420 iliyotumika Europe. Hawakunishauri kabisa kununua Truck Mpya ama Refurbished za Mchina, DAF na Volvo wakaniambia zitanitesa maana ndio kwanza naingia kwenye game. Hata nilipouliza SCANIA zilizotumika south Africa wakaniambia ni bora nichukue za europe zinakuwa bado zipo Bora na hazijatembea sana kwenye rough road kwa hizo za SOUTH japo hizo za south walikiri kwa gharama ya manunuzi zipo chini kiasi.
FUNDING
Kama nilivyoeleza awali mimi ni new comer kwenye hii industry hivyo nategemea kujichanga kama 50-60Mil then the rest nichukue mkopo maana nakopesheka vizuri sana. Baada ya kufanya window shopping nimegundua horse scania mtumba inaweza kunicost kati ya 75Mil - 85Mil hapa nitapata gari nzuri tu, Trailer nimeshauri kununua ya Mkononi ambayo imetumika hapa nchini ambapo zina range 25Mil - 30Mil kutokana na hali yake. Nimejaribu kuulizia. Mpya lakini naona bei imechangamka sana USD 28,500.00 flatbed Double tire
TECHNICAL
Nimeshauriwa hapo kwenye trailer kununua super single kwa maana inabeba Mzigo Mkubwa kulinganisha na trailer yenye double tire.
Kwenye Horse kama nilivyoeleza awali nimeshauriwa SCANIA 6x2 124L 420 Mtumba kutoka EUROPE
BUDGET
Ukiangalia makisio ya gharama zote Horse na Trailer budget yake inacheka kati ya 100Mil - 115Mil. 60% Nategemea kuitoa Mfukoni na 40% nichukue Mkopo. Nategemea kulipa Mkopo kwa kutumia Mshahara wangu pamoja na Mapato yatakayokuwa yanapatikana baada ya Truck kuanza kuoperate. Nimekuja kuomba ushauri kwa yeyote mwenye kuielewa biashara hii kwa undani, nimeweka mchanganuo wote hapa ili niweze kupata ushauri mzuri kulingana na information nilizopokea pamoja na uwezo wangu wa kifedha. Nategemea kuna wajuzi wengi humu na nitambulia ushauri mzuri katika kukamilisha hili. Ahsanteni na niwakaribishe kwa Ushauri. Kejeli na dharau hapa si mahala pake.
Trailer ya double inapenda kwa sabab kwenye mizani haizidi mzigo,zile single zinasumbua sana kwenye mizani achana na story za vijiweni
Angalia hata mabus mengi wanayafunga terias nyuma siyo fashen n sabab ya mizan mkuu
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app