Naomba ushauri wa biashara ya malori

Kwema mkuu,hongera kwa jitihada,,kwa kua tayar una ka mtaji kadogo,jaribu kuagiza horse ya mtumba thn tafuta taratibu za kukod trailer,ukishafanikiwa kuusoma mchezo utaona mwenyewe kwamba nikikopa ela ya trailer ntaweza kurejesha?

Trailer ya double inapenda kwa sabab kwenye mizani haizidi mzigo,zile single zinasumbua sana kwenye mizani achana na story za vijiweni

Angalia hata mabus mengi wanayafunga terias nyuma siyo fashen n sabab ya mizan mkuu

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Umemshauri vyema lakin kwenye trailer ya kukodi hapana, faida ya gari ikienda na kurudi mara nyingi inakuwa $300 mpaka $500 , sasa Kama umekodi trailer maana yake faida inakuwa inaenda kwa trailer , kibaya zaidi contract ikiisha urudishe trailer Kama ukivyoichukua wakati kuchakaa kwake ndo kufanya kazi kwake:

Ni kama mwenye nyumba akwambie ukitaka kuhama paka rangi nyumba yangu ( haiwezekani)

Kama hauna trailer ya kwako mwenyewe, usinunue horse, kuwa na uhakika wa trailer kwanza ndo ununue horse: vinginevyo utakikuta unahudumia trailer harafu horse yako inakosa msaada
 
Kuna tajiri mmoja aliadithia kipande Cha maisha yake.

Alikuwa anasafiri sana Kuna siku alipanda Basi akaona Basi linajaa mpaka kutapika na huko njian abiria n wengi alivyorud tuu Ile safari akaenda kununua Basi 2 mpya akaziweka barabarani kilichofuata hapo anasema hatokuja kukisahau.

Anasema kwanza aligombana na matajiri wenzake bila sababu za msingi, aligombana na madereva na makondakta mwisho alkua anaishi na stress kila wakati ikabid auze zile basi ili awe na Amani.

Hii inamaana kuwa Biashara ya Gari unahitaji usimamizi mkubwa sana napia maneno ni mengi pia uhasama n mkubwa hvyo unahitajika 100% kwenye usimamizi tofauti na hapo uliowaajiri watajenga na kununua fuso huku wewe nje kukiwa na screpa za giabox, engine mpaka chassis na matairi vipara ukiwa umeyapanga nje kwako ukiamini utayauza.
 
Nipo kwenye mchakato wa kuomba mkopo wa Bajaj, Ila IPO siku ntaomba ushauri Kama huu!!!

Mkuu nakuunga mkono!! Mungu akutangulie
Ushauri wangu!!
Jitahidi Sana kuweka bima ya jadi kwenye gari yako!
75% ya ajali za barabarani zinasababishwa na masuala ya ushirikina...
Ni Hilo tu
 
Ukisha nunua naomba kazi ya uajent kwa mpaka wa kasumulu mkuu.
 
Anzia EFTA unalipa 30% ya gharama ya chombo alafu mnakubaliana kila mwezi utapeleka ngap ukimaliza wanakupa kadi yako kumbuka unatakiwa pia ulipe insurance kubwa kwa manufaa yenu wote hasa EFTA
 
Anzia EFTA unalipa 30% ya gharama ya chombo alafu mnakubaliana kila mwezi utapeleka ngap ukimaliza wanakupa kadi yako kumbuka unatakiwa pia ulipe insurance kubwa kwa manufaa yenu wote hasa EFTA
Efta ndo nn mkuu nifahamishe
 
Nimetoa ushauri tu! Na ww nakushauri umtie moyo kwa hilo fundisho ulilo niandikia mimi!
 
Nilikuwa mbishi kwenye biashara hiyo hadi niliitwa betri na vijana!
Kilichotokea magari yalipo haribika walaji woote wakasepa na kuniacha na magari yangu mabovu kunguru wanayanyea[emoji24]
[emoji24][emoji24]
Yaliharibika nini kisichotengenezeka?

Inawezekanaje magari yote yaharibike kwa pamoja kiasi cha kushindwa kutatulika?

Inawezekana wewe ni wale wanaolimbikiza magonjwa mpaka gari igome kwenda ndiyo muanze kuunga unga..
 
Daah[emoji2][emoji2]
 
Yaliharibika nini kisichotengenezeka?

Inawezekanaje magari yote yaharibike kwa pamoja kiasi cha kushindwa kutatulika?

Inawezekana wewe ni wale wanaolimbikiza magonjwa mpaka gari igome kwenda ndiyo muanze kuunga unga..
Ndio imesha wezekana!
Beyond economic repair...
 
Hahaha umenikumbusha miaka ya nyuma nilikuwa nakodi fuso za jamaa flani kubebea mizigo yangu.

Aisee tajiri wa hizo gari anafuatilia na ni mkali mpaka madereva wanaomba Mungu gari isiharibike.
Tanzania kuna utamaduni kuwa tajiri hapaswi kutembea na gari lake muda wote! Tajiri yoyote anayeonekana kutembea na gari lake eg basi la abiria anachukiwa na kutukanwa sana. Kwa nini?
 
Nimeamua kwenye trailer hapo nianze na ya kukodi nione kwanza pesa inavyoingia. Ahsante Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…