Naomba ushauri wa biashara ya malori

Naomba ushauri wa biashara ya malori

"Kila unachokiona mbele yako kilishawahi kuwa kwenye truck"

Umeamua vyema kuwaza biashara hii.

Niongeze kidogo

Kuliko kununua gari used budget yako inatosha kuwapa TATA wakakupa gari mpya kwa 35m na trailer ukiunga unga utapata kwa 30m double tyres.

Super single ina changamoto nyingi sana kuliko unavyoweza kudhan!
Transcargo, Dangote hawana trailer za super single.

Ukiamua kuchukua gari used jitahidi kuipitia kila sehemu ikiingia barabaran usipate changamoto. Maghari yanayotoka Poland usichukue mengi yametumika sana.

Gari kutoka South Africa ukipata muungwana akakurekebishia kabla ya kulisafirisha ni gari bora kuliko mtumba wa Uingereza.

Ukiamua kuchukua Uingereza hakikisha MOT iko active hii gar imejaribiwa kwao na inafanya kazi katika barabara za Uk.
Scani 124 420, kuwa makina kuanzia 2002 hadi 2004 nying ni HPI ama red dot zinasumbua sana katika mazingira yetu.
6x2 chagua tag axle yaan teriaz nyuma ili uweze kubeba mzigo mkubwa.

Biashara ni nzuri ngumu, jitahidi ujibanze kwenye kampuni yenye kazi za uhakika. Kazi za dalali zitakufanya uchukie kazi.

Usimamizi jitahid mda mwigini uone gari nanufanye service.

Hayo machache kwa nilivyojionea barabaran.
Mkuu hapo kwenye TATA umewaza kuhusu Spare maana sijaziona nyingi hizo gari mtaani.
 
Tafuta Howo mpya gharama za uendeshaji ni ndogo kuliko European trucks. Biashara ikikuwa ndio uende huko kwa European trucks. Trailer la double tyres ndio linabeba mzigo zaidi kutokana na sheria mpya za Tanroads(mizani) ...hawataki singles kwente barabara zao hivyo wamepunguza uzito unaoruhusiwa kwenye axles za single tyres.
 
Yote 9. Usisahau COMPRENSIVE INSURANCE. From day 1.
Mie ilinunua truck and trailer mwaka 2005. Nikakata third party nikisema likirudi safari ndio nikate compressive. Likaanguka trip ya kwanza pale mteremko wa TUKUYU. Sijawahi kunyanyuka tena kibiashara.
Au lile lililoanguka WAMI lilikuwa trip ya kwanza bila insurance.
 
Tafuta Howo mpya gharama za uendeshaji ni ndogo kuliko European trucks. Biashara ikikuwa ndio uende huko kwa European trucks. Trailer la double tyres ndio linabeba mzigo zaidi kutokana na sheria mpya za Tanroads(mizani) ...hawataki singles kwente barabara zao hivyo wamepunguza uzito unaoruhusiwa kwenye axles za single tyres.
Umemshauri vizuri ndio maana mm nimemwambia ukitaka kuingia kwenye hizo mishe za scania angalau uingize laki5 kwa siku nazani hajaelewa namaanisha nini atapoingia atajua,
Kwann matajiri wengi wanadaka michina kama,volvo,man,howo,faw,nk sio kwamba scania hawazipend ishu uendeshaji wake ni gharama sana hasa ikipata hitilafu ila ni za kudumu mwenye nina scania 4 na howo5,lakini pind ikiharibika scania unakuta umedunduliza mtaji wa, kwenye howo tatu kutengeneza scania moja japo ukitengeza ni mkataba ila nataka nizitoe nidake faw
 
Jomba zingine hizi ukiziitaji njoo pm tukae chini nikuachie
29137c77232703d71c2bf7c864bbf5b1b0d8a737.jpg
7c2c55102ac1ab61cef95c8a098acf83f5e16350.jpg
dacbe0a411807353931056d1e6dc6f764e6026e8.jpg
 
124 , 420 mwaka 1999 hadi 2001 cummis engine , utafurahi, unaweza jaribu na V8 164 ama R500 kwa kazi za kiume zina fanya vyema sana.
Samahani Mkuu, cummis ni nini?

Halafu hiyo R500 unayomshauri jamaa hazifiki hata tano nchi nzima!

Superstar & world oil ni miongoni mwa wenye mbavu za kununua hii gari lakini hawana..

Muache jamaa atulize roho yake kwenye 124!!
 
Samahani Mkuu, cummis ni nini?

Halafu hiyo R500 unayomshauri jamaa hazifiki hata tano nchi nzima!

Superstar & world oil ni miongoni mwa wenye mbavu za kununua hii gari lakini hawana..

Muache jamaa atulize roho yake kwenye 124!!
Nimemaanisha Cummins,
 
Kwamba huzioni au ? Labda mkoa ulipo Ila zipo nyingi sana ila mtaji uwe kuanzia m17 hivi sio laki tano tu hadi m4 kwa siku unalaza kutegemea umechanga vip karata zako
Tudokeze mkuu , unaweza saidia mtu akanyanyuka
 
Kabla hajaingia huko hakikisha una njia zingine zinazo kuingizia mapato japo kima cha chini uingize laki5 kwa siku tofauti na hapo endelea kujiwekeza,sikukatishi tamaa ila naielewa vizuri hiyi biashara mwaka wa tano sasa ukiweza hilo karibu ni bonge la biashara
Laki 5 kwa siku ni 15 kwa mwezi. Hiyo sio kipato cha chini
 
Kwamba huzioni au ? Labda mkoa ulipo Ila zipo nyingi sana ila mtaji uwe kuanzia m17 hivi sio laki tano tu hadi m4 kwa siku unalaza kutegemea umechanga vip karata zako
Mkuu,
Mtaji wa milioni 17 halafu uingize milioni 4 kwa siku! Hiyo ni asilimia 25 ya mtaji unaingiza kwa siku….be serious!
 
Broo umemshauri vzr San huyu jamaa asije pata pressure buree Niko ktk magari ya mtu tunapanga kuyapiga minada yote , scani mende Bei iko poakama utaziitaji ukachongee body POA tu Ila Ni risk bussines ever
Ungemuwekea hapa hizo risks ili nayeye ajipime
 
Back
Top Bottom