kamwene vanyalukolo
Hongera kwa kujichanga, maana huwa ni zoezi zoto la kujinyima sana pongezi sana.
Kwa sababu hujawahi kumiliki gari, kwa namna yeyote nadhani hauna experience nzuri na magari.
Hivyo, unahitaji kupata, si gari tu bali gari bora. Gari ambayo haitokusumbua na pia yenye ulaji mzuri wa mafuta.
Naomba nikushauri juu ya Toyota Corolla Spacio, hii ndio gari ambayo haitoweza kukusumbua, kwa maana upatikanaji wake wa vipuri pamoja na hata utengemezaji wake, mafundi wengi wanaumudu. Uzuri zaidi ina ulaji mdogo wa mafuta, na inaweza kusafiri umbali mrefu zaidi hata ya huo uliotaja. Zaidi sana hata shambani, na kwenye barabara za vumbi pia ina himili.
Naomba ubonyeze maandishi haya hapa
Used 2005 TOYOTA COROLLA SPACIO X G EDITION/CBA-NZE121N for Sale BG872260 - BE FORWARD kuona picha zoote za gari yako.
Details kwa ufupi ;
2005 Toyota Corolla Spacio
Engine size : 1,490 cc
Milleage : 47,016km (imetembea 47,016km tu)
Utumiaji wake wa mafuta : Inakwenda wastani wa kilometa kumi na tano kwa litre (15km/L)
UKWELI WA HALI HALISI ;
Niukweli kwamba, kwa gari kama hii, 10mil max, haitoshi , hii inatosha kuagiza nakuifikisha hadi bandari ya Dar es salaam tu, lakini hauwezi kulipia ushuru.
Kuna huduma ambayo inakufaa, huduma yenyewe ni kwamba ; Kuna utaratibu wa kumlipia mtu ushuru ikiwa anahitaji gari fulani, ila budget yake inakua haitoshi.. hivyo kama ukipenda nitakupa mtu ambaye mtaandikishiana maandishi ya makubaliano kisheria, na mwanasheria ataya sign.
Kisha malipo ya uagizaji yatafanywa jule japan.
Baada ya malipo ya uagizaji kule japan.
Gari yako itasafirishwa, ikishafika Bandari ya Dar es salaam, mtu huyu ambaye mliandikishisna tokea mwanzo, atailipia ushuru na gharama zote za bandari hadi kulitoa bandarini.
Baada ya hapo, anakukabidhi gari lako, na kisha baadaya mwezi unaanza marejesho yako kama mkataba wako na yeye utakavyokua unaelezea.
Ahsante!