Naomba ushauri wa gari gani zuri la kutembelea lisilozidi Sh. milioni 10

Naomba ushauri wa gari gani zuri la kutembelea lisilozidi Sh. milioni 10

Joined
Sep 10, 2019
Posts
72
Reaction score
74
Habari wadau,

Nimejichanga kwa kipindi kirefu sasa nimeamua kutafuta kigari cha kutembelea cha kutosha familia ya watu 5 (me, ke& watoto 3) kisichozidi 10m.

Binafsi sijui kuendesha gari na hata sina uzoefu na vyombo vya moto kwa sababu hata pkpk sijawahi miliki.

Naombeni ushauri wa aina ya gari inayoweza kunifaa ambayo nitaweza safir nayo toka Shy to Njombe bila wasiwasi.

NB: Isiwe imetumika zaidi ya 150,000 KM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
20200426_101650.jpg
 
Kwa bajet hiyo cheza kwenye gari ndogo za kawaida.. IST, raum, probox and the like. Upate ilioko katika hali nzuri ili isikusumbue kama ulivyosema huna uzoefu na magari. Ukipata iliyochoka utashinda gereji na mafundi watakutoa jasho
 
kamwene vanyalukolo


Hongera kwa kujichanga, maana huwa ni zoezi zoto la kujinyima sana pongezi sana.

Kwa sababu hujawahi kumiliki gari, kwa namna yeyote nadhani hauna experience nzuri na magari.
Hivyo, unahitaji kupata, si gari tu bali gari bora. Gari ambayo haitokusumbua na pia yenye ulaji mzuri wa mafuta.

Naomba nikushauri juu ya Toyota Corolla Spacio, hii ndio gari ambayo haitoweza kukusumbua, kwa maana upatikanaji wake wa vipuri pamoja na hata utengemezaji wake, mafundi wengi wanaumudu. Uzuri zaidi ina ulaji mdogo wa mafuta, na inaweza kusafiri umbali mrefu zaidi hata ya huo uliotaja. Zaidi sana hata shambani, na kwenye barabara za vumbi pia ina himili.

Naomba ubonyeze maandishi haya hapa Used 2005 TOYOTA COROLLA SPACIO X G EDITION/CBA-NZE121N for Sale BG872260 - BE FORWARD kuona picha zoote za gari yako.

Details kwa ufupi ;

2005 Toyota Corolla Spacio
Engine size : 1,490 cc
Milleage : 47,016km (imetembea 47,016km tu)
Utumiaji wake wa mafuta : Inakwenda wastani wa kilometa kumi na tano kwa litre (15km/L)

UKWELI WA HALI HALISI ;

Niukweli kwamba, kwa gari kama hii, 10mil max, haitoshi , hii inatosha kuagiza nakuifikisha hadi bandari ya Dar es salaam tu, lakini hauwezi kulipia ushuru.

Kuna huduma ambayo inakufaa, huduma yenyewe ni kwamba ; Kuna utaratibu wa kumlipia mtu ushuru ikiwa anahitaji gari fulani, ila budget yake inakua haitoshi.. hivyo kama ukipenda nitakupa mtu ambaye mtaandikishiana maandishi ya makubaliano kisheria, na mwanasheria ataya sign.

Kisha malipo ya uagizaji yatafanywa jule japan.
Baada ya malipo ya uagizaji kule japan.
Gari yako itasafirishwa, ikishafika Bandari ya Dar es salaam, mtu huyu ambaye mliandikishisna tokea mwanzo, atailipia ushuru na gharama zote za bandari hadi kulitoa bandarini.

Baada ya hapo, anakukabidhi gari lako, na kisha baadaya mwezi unaanza marejesho yako kama mkataba wako na yeye utakavyokua unaelezea.

Ahsante!
BG872260_372d4a.JPG.jpg
BG872260_15bcf8.JPG.jpg
BG872260_04c294.JPG.jpg
BG872260_15628d.JPG.jpg
BG872260_7579d9.JPG.jpg
BG872260_90b379.JPG.jpg
BG872260_80bc54.JPG.jpg
BG872260_43c0c4.JPG.jpg
BG872260_2ef17a.JPG.jpg
BG872260_c49deb.JPG.jpg
BG872260_f9ef8e.jpeg
BG872260_1bf3b2.jpeg
 
Back
Top Bottom