Naomba ushauri wako juu ya kipi nifanye kwa hiki kilichotukumba kwenye ndoa

Naomba ushauri wako juu ya kipi nifanye kwa hiki kilichotukumba kwenye ndoa

Pia, unaweza amua kutumia condom. Hakikisha unakuwa na box kabisa chumbani, sio kununua rejereja.
Kondom hapana, nafikiri nitafunga mimi uzazi.
SWali moja. Ukifunga uzazi unakua hushushi mzigo ule kwenye mambo yetu yale au inakuaje yan?? Na haina atharinyoyote kwa mwanaume ku enjoy sex akifunga uzazi??
 
Wakuu heshima kwenu.
Polen na hongereni kwa majukumu yenu ya kila siku.

Niko kwenye hali fulani ya mkanganyiko kidogo. Nasema kidogo kwasababu ni kama niko njia panda japo kuna njia ambayo kwa mujibu wa misingi ya imani na utamaduni na maadili yangu najua nitaiendea njia hiyo japo naona ni ngumu sana ndio lengo la kusogea kwenu nipate mawili matatu.

Mimi ni mwanaume. Umri wangu ni 35 years.
Nina mke yeye ni 36 years na Mungu katubariki kuwa na watoto wa 4 mpaka sasa hivi katika kipindi chote cha miaka 14 toka tujuane na mpaka kufunga ndoa. Tuna miaka 10 toka siku tufunge ndoa rasmi.

Mwanangu wa kwanza ana 13years yuko form 1, wapil yuko class 3 , wa 3 yuko class 1 na wa 4 ana mwaka mmoja na miez kama 9 sasa.
Katika hawa woote watoto wanne, ni mmoja tu wa kiume wa tatu kuzaliwa alieko clasa 1.

Sasa hapa juz kati tumekuja kufaham kuwa wife kanasa mimba tena. Ni baada mwezi kupita bila kuona kawaida ya kike ya kila mwezi na tukaamua kufanya vipimo tukagundua imoo.

Shida sio mtoto, shida ni mipango. Sikua na mpango wa kuzaa baada ya kufunga miaka 35 ya umri.
Hii imenifanya kuwa na reaction tofaut katika mapokeo ya taarifa ya ugen huu. Na suala hil hata kwa wife pia lilimtoa machozi. Kiukwel hii taarifa ilitupa shock na imezua mgogoro mkubwa na wife, amenishushia lawama sana hasa kwakua nilipopata majibu haya sikuchukua hatua ya kum comfort. Nafikir ni kwakua hata mimi ilinichanganya. Amekua akinishutumu sana japo najua hii yote yaweza kuwa ni shock ya tukio ambalo hakuna aliyetegemea..

Kwa imani yangu, nimekua nikimuomba Mungu anipe amani na uamuzi sahihi na pia utayari wa kupokea suala hilibkwa mikono miwili. Anisaidie kusiwe na athari yoyote kiroho kwa mtoto kwa jiona kama hatuko tayari kumpokea. Namuomba sana Mungu anisaidie na aingilie kati, pia amsaidie wife aweze kukubaliana na hili, naelewa sana jinsi ambavyo inam frustrate pengine kila anapofikiri kuanza safar ndefu ya miezi 9 yenye kila aina ya vikwazo kiafya na kihisia.

Naelewa ni namna gani huwa inatu consume kusubiri mtoto kuzaliwa na majibu ya maombi yetu kuwa mtoto azaliwe salama mwenye afya njema bila kasoro. Haya yote tunayajua kwa watoto hawa wa 4 tuliojaaliwa.

Sasa sisi tukawa tunahesabu mambo haya tumekwisha yamaliza na hatuta rudi tena huko zaid ya kukaa na kulea watoto na kuwaandalia future yao.

Wakuu nachanganyikiwa japo nimeanza kukubaliana na hili.
Naomba ushauri wenu na kutiwa moyo.

Nafikiri baada ya hili kupita kama Mungu akitujaalia kumaliza mwendo salama, mmoja wetu atapaswa kufunga uzazi, hakuna namna.

Ahsanten na karibun kwa ushauri.
Siku njema
Bado cjaona sababu za moja kwa moja ya kujipa presha wala kulaumiana kwasabu ulipo mwagia ndani ulitegemea nni mkuuu limesha tokea kama kuitoa hiyo mimba hamko tayari kubalini matokeo and move one binafsi naona ni jambo la kawaida bado haijabeba uzito wa kukupa stress……… ni seme tu hilo ni jambo la kumshukuru MUNGU na mkatoe sadaka ya shukrani jumapili
 
Bado cjaona sababu za moja kwa moja ya kujipa presha wala kulaumiana kwasabu ulipo mwagia ndani ulitegemea nni mkuuu limesha tokea kama kuitoa hiyo mimba hamko tayari kubalini matokeo and move one binafsi naona ni jambo la kawaida bado haijabeba uzito wa kukupa stress……… ni seme tu hilo ni jambo la kumshukuru MUNGU na mkatoe sadaka ya shukrani jumapili
Sawa kiongozi wangu, nafikiri nimekuelewa.
 
Kondom hapana, nafikiri nitafunga mimi uzazi.
SWali moja. Ukifunga uzazi unakua hushushi mzigo ule kwenye mambo yetu yale au inakuaje yan?? Na haina atharinyoyote kwa mwanaume ku enjoy sex akifunga uzazi??
Mzigo unakula kama kawaida, una ejakulate shahawa tu mbegu hazitoki.
Zinabaki kwenye mbupu na baada ya muda zinachukuliwa na mwili kwa matumizi mengine.
 
Hayo yalishanipata mimi kwa mtoto wa mwisho na tukakaa chini na mke wangu na kukubaliana na hali. kwanza nilifikiri jinsi ya kumlea Mungu akanionyesha kuwa yeye ndiye anatulisha. La pili nikamwambia Mungu anipe mvulana maana nilikuwa na wasichana wawili na kijana mmoja na nikampa Jina la kiume. Kweli alizaliwa mtoto wa kiume. Mungu akamjalia akili na akawa anasomeshwa kwa scholarship kuanzia form six mpaka degree na amekuwa baraka kwetu sana. Ninakushauri kaa na mke wako mjue kwamba is a blessing to you na atakuja kuwa faraja kwenu.
 
Ahahahahah... mkuu kwa namna nyingine umefanya nicheke. Ila usemayo ni sahihi.

Niseme tu, suala la wife kutokuabali hili kirahisi ndio linanipa hofu nafikiri. Namuelewa though kwann yuko hiv. Ninkitu kigumu sana uzazi
Mtoe out halafu msifu Kwa kufyatua hao wnne alionao na huyo atafyatua tu!!

Sisi me ni shock obsorber sio stress inducers!!

Tangu mwanzo ungeua wasiwasi wake angekua fine!!

Mtoe out kabisa halafu msifu aachane na stress!
 
Poleni na hongera pia,
Lea mimba mpaka mkeo ajifungue,
Mmepanga yenu Mungu nae kapanga ya kwake,
Mshukuru Mungu na fungueni mioyo yenu mumtolee huyo malaika Roho ya kukataliwa,
Nenda kampe faraja mke wako,
Unachanganyikiwa na kupata sonona wakati mzigo ni wako.
Be a man,
Be responsible 💪
 
watu wazima wawili wasio na akili wamekutana, ina mana mkeo ameshindwa kutumia uzazi wa mpango? mlivyomwagiana ndani mlijua mtavuna mapera? ole wenu mkaitoe, sasa mliwapangaje watoto mkashindwa kupangilia kwa hapa? haya bahat ishakua imetokea mimba imo wajibikeni nyote, msiwaze sjui itakuaje ushatokea hio komaeni
 
Shida sio mtoto, shida ni mipango. Sikua na mpango wa kuzaa baada ya kufunga miaka 35 ya umri.
Hii imenifanya kuwa na reaction tofaut katika mapokeo ya taarifa ya ugen huu.
Ulitakiwa kuomba tukutengenezee ratiba ya tendo mapema, kwa hapo ulipofika sidhani kama kuna point of return any more
 
USHAURI.
Kaa na wife vzr onyesha furaha kama ni mtu wa dini Anza kumpa matumaini na Imani hata kama ni kubumba.

Mwambie kwako wewe unafuraha sana kuwa na mtoto mwingine wa5 hivyo Mungu ndiye alipanga iwe hivyo.

Kwa Wakati huu Sasa onyesha uzezeta kuliko kipindi cheto za mimba zilizo pita.

Ingia jikoni pika, kateembeen pamoja hata kama huna Hela tokaen mjini mkadhurule huko maporini.

Jifanye hiyo mimba imerudisha mapenzi yenu upyaaa muda mwingine mvamie osha vyombo,

Mkuu sikufundishi yte hayo ni baadhi tu na ukizingatia wanaume Huwa hatushindi nyumbani Kwa sababu ya majukumu hivyo muda ukiwa upo fanya haya.

Naongea Hivi nilimshauri jamaa yangu baada ya mke wake kunywa dawa mara1 aitoe na haikutoka Ile mimba ndo akanishirilisha Mimi.

Jibu langu nilimwambia WEWE NI MWANAUME MPUMBAVU SIKU ZOTE SIKUJUA KAMA NINA RAFIKI MPUMBAVU KIASI HIKI!!

Nikampa mfano vipi mkeo akifa anatoa hiyo mimba? Hasara itakuwa kwake au kwako?

Nikampa hizo nondo mara kadhaa nikawa namuazima gari angu kipindi hiko akale Bata nae. Now mtoto anamiaka2 mzuri mchangamfu sana nilimuita jina BAHATI (Good luck) Hadi Leo.

Ni ushauri tu ukiamua uuchambie yote sawa tu
 
Back
Top Bottom