Right Way In Light
JF-Expert Member
- Jul 27, 2024
- 1,322
- 3,461
- Thread starter
- #101
Ni kwel usemacho mkuuKikubwa kubaliana na hali mpokee mtoto anayekuja.shangaa huyo akawafaa uzeeni make hakuna ajuaye ya mbeleni
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kwel usemacho mkuuKikubwa kubaliana na hali mpokee mtoto anayekuja.shangaa huyo akawafaa uzeeni make hakuna ajuaye ya mbeleni
Yaan mkuu hii ishu yako ni kama yetu, hata mimi nilivurugwa kiasi cha kumuuliza hivyo wife like "au kuna mistake umefanya huko ndio maana unalia" hapa sasa nikachochea motoHaya mambo haya mimi kalenda ilinisaliti mpaka mr akaanza kusema au umenibambikizia,kwanza mtoto alikuwa bado mdogo sana jamaa alipanic akasema tuitoe,mi nikamwambia sina mpango huo hata sir God hawezi kunielewa,badae akarudi kwenye mstari mambo yakawa sawa tu.
Sawa sawa chief..kumbe hii ni experience ya watu wengi kidogo kwenye ndoa!!.. napata mwangaza sasa, na ninashukuru wadau kuniweka wazi maana inanitia moyoNakazia hapa.
Nyie hamkupanga lakini Mungu alipanga kua huyo mtoto lazima azaliwe wakati huo.
Nakumbuka mimi na wife tulipitia stress kidogo baada ya mimba ya mtoto wa pili kuingia wakati wa kwanza bado hajakua vizuri.
Tuliamua kutomwaga damu, isitoshe watoto ni zawadi, tukakubaliana nalo, na Mungu mwema safari ya miezi tisa tumeimaliza.
Hakikisha unakua karibu na mke wako, muonyeshe upendo mkubwa sana.
Mwongozo wako pia muhimu mkuu!.
Inabidi muwe strong nyie bora mkubwa,mimi ndo kwanza alikuwa na miezi sita,nilipambana mtoto nikamnyonyesha huku na mimba yangu karibia najifungua ndo namuachisha baada ya kujifungua unasahau.Yaan mkuu hii ishu yako ni kama yetu, hata mimi nilivurugwa kiasi cha kumuuliza hivyo wife like "au kuna mistake umefanya huko ndio maana unalia" hapa sasa nikachochea moto
Dada angu kweli wewe ulipambana, mtoto wa miezi 6 naamin kabisa haikua rahisi.Inabidi muwe strong nyie bora mkubwa,mimi ndo kwanza alikuwa na miezi sita,nilipambana mtoto nikamnyonyesha huku na mimba yangu karibia najifungua ndo namuachisha baada ya kujifungua unasahau.
Mungu alikupa mwanaume uwezo wa kumjaza mimba mwanamke hata ukiwa na miaka 90, lakini mwanamke 40 tu kupata mimba ni mbinde.Ushauri.
Mmoja au wote mfunge kizazi, au wife atumie zile njia za kuzuia uzazi.
Hebu naomba uni PMWakuu heshima kwenu.
Polen na hongereni kwa majukumu yenu ya kila siku.
Niko kwenye hali fulani ya mkanganyiko kidogo. Nasema kidogo kwasababu ni kama niko njia panda japo kuna njia ambayo kwa mujibu wa misingi ya imani na utamaduni na maadili yangu najua nitaiendea njia hiyo japo naona ni ngumu sana ndio lengo la kusogea kwenu nipate mawili matatu.
Mimi ni mwanaume. Umri wangu ni 35 years. Nina mke yeye ni 36 years na Mungu katubariki kuwa na watoto wa 4 mpaka sasa hivi katika kipindi chote cha miaka 14 toka tujuane na mpaka kufunga ndoa. Tuna miaka 10 toka siku tufunge ndoa rasmi.
Mwanangu wa kwanza ana 13years yuko form 1, wapil yuko class 3, wa 3 yuko class 1 na wa 4 ana mwaka mmoja na miez kama 9 sasa. Katika hawa woote watoto wanne, ni mmoja tu wa kiume wa tatu kuzaliwa alieko clasa 1.
Sasa hapa juz kati tumekuja kufaham kuwa wife kanasa mimba tena. Ni baada mwezi kupita bila kuona kawaida ya kike ya kila mwezi na tukaamua kufanya vipimo tukagundua imoo.
Shida sio mtoto, shida ni mipango. Sikua na mpango wa kuzaa baada ya kufunga miaka 35 ya umri.
Hii imenifanya kuwa na reaction tofaut katika mapokeo ya taarifa ya ugen huu.
Na suala hil hata kwa wife pia lilimtoa machozi. Kiukwel hii taarifa ilitupa shock na imezua mgogoro mkubwa na wife, amenishushia lawama sana hasa kwakua nilipopata majibu haya sikuchukua hatua ya kum comfort. Nafikir ni kwakua hata mimi ilinichanganya. Amekua akinishutumu sana japo najua hii yote yaweza kuwa ni shock ya tukio ambalo hakuna aliyetegemea.
Kwa imani yangu, nimekua nikimuomba Mungu anipe amani na uamuzi sahihi na pia utayari wa kupokea suala hilibkwa mikono miwili. Anisaidie kusiwe na athari yoyote kiroho kwa mtoto kwa jiona kama hatuko tayari kumpokea. Namuomba sana Mungu anisaidie na aingilie kati, pia amsaidie wife aweze kukubaliana na hili, naelewa sana jinsi ambavyo inam frustrate pengine kila anapofikiri kuanza safar ndefu ya miezi 9 yenye kila aina ya vikwazo kiafya na kihisia.
Naelewa ni namna gani huwa inatu consume kusubiri mtoto kuzaliwa na majibu ya maombi yetu kuwa mtoto azaliwe salama mwenye afya njema bila kasoro. Haya yote tunayajua kwa watoto hawa wa 4 tuliojaaliwa.
Sasa sisi tukawa tunahesabu mambo haya tumekwisha yamaliza na hatuta rudi tena huko zaid ya kukaa na kulea watoto na kuwaandalia future yao.
Wakuu nachanganyikiwa japo nimeanza kukubaliana na hili.
Naomba ushauri wenu na kutiwa moyo.
Nafikiri baada ya hili kupita kama Mungu akitujaalia kumaliza mwendo salama, mmoja wetu atapaswa kufunga uzazi, hakuna namna.
Ahsanten na karibun kwa ushauri.
Siku njema
Ni kweli kila mtu anaongea lake ila unapotezea,alafu nyie umri wenu bado mdogo mi mtoto wa kwanza nilipata nikiwa na miaka 31Dada angu kweli wewe ulipambana, mtoto wa miezi 6 naamin kabisa haikua rahisi.
Hapo huwa tunaumizwa na mitazamobya watu, kwamba watatuonaje hawa? Kwamba tunapemda sanaaa mpaka hatuzingatii masuala ya msingi?
HApo nimekuelewa vyema mkuu. Ahsante sana.Ni kweli kila mtu anaongea lake ila unapotezea,alafu nyie umri wenu bado mdogo mi mtoto wa kwanza nilipata nikiwa na miaka 31
Mkuu i really appreciate your sharing. Thanks alotKilichokukuta wewe ni kama ambacho kilinikuta mimi miaka 4 iliyopita. Mimi na mke wangu tumejaaliwa watoto 4 kwa sasa.
Plan ya kwanza ilikuwa tuwe na watoto wawili tu. Ila kwa bahati wote wawili walikuja wa kiume. Tukakubaliana tujaribu mara moja ya mwisho napo pia akapatikana wa kiume.
Tuliamua rasmi kuwa kuzaa basi tena. Mke wangu aliweka kitanzi lakini kikawa na madhara makubwa kwake kiafya, akaweka kijiti halkadhalika ikawa na matatizo, akaishia kwenye vidonge vya majira.
Kuna kipindi alipata blood infection kupelekea kutumia antibiotics ambazo kitaalam inasadikika huudhofisha nguvu ya vidonge vya majira. Baada ya muda ikawa hajielewi ikabidi kupima ujauzito na kukuta imo.
Hicho kipindi kilikuwa ni kigumu mno maana iilikuwa kipindi cha Covid, kipato kilitetereka na bado ujauzito umekuja.
Mungu anisamehe, nilimwambia mke wangu atoe ujauzito na mpaka kumfanyia booking ya abortion. Mwanzo alikubali lakini dakika ya mwisho kabisa akabadili mawazo yake na kukataa kabisa kutoa ile mimba. Hii ilileta mtafaruku mkubwa mno baina yetu katika ndoa. Kipindi chote cha mwanzo cha ujauzito hatukuwa sawa mpaka nililipoamua kukubaliana tu na hali halisi.
Baada ya miezi tisa mke wangu alijifungua mtoto wa kike. Mtoto ambae nilikuwa nikitamani kumpata kwa miaka.
mingi. Nafsi ilinisuta na wakati mwingine inanisuta mpaka leo.
Binadamu ni wazuri katika kupanga ya kwetu huku tukisahau kuna mamlaka yenye nguvu zaidi yetu na kila kitu hutokea kwa matakwa yake.
Binti yangu alizaliwa July, 2020, January 2021 mke wangu alipata message instagram toka kwa ad agency kupitia kwenye account ambayo alimfungulia mtoto kama wafanyavyo ma mama wengi. Walitaka kutumia picha za mwanangu kwenye matangazo ya vitu vya watoto.
Mwanzo nilidhani utani lakini baada ya kuangalia account ya huyo mtu ya instagram nikagundua ni ya kweli kutoka Kenya. Process iliyofuatwa ilikuwa ni mkataba wa miaka miwili ambao uliisha January 2023. Malipo hayakuwa makubwa sana ila kwa kipindi hicho ilitusaidia mno kusogeza maisha mbele.
Inawezekana mwanao asije kupata mikataba ya kazi akizaliwa tu kama wangu lakini kila jambo hutokea kwa sababu zake. Mpe moyo mke wako na chukulia kuwa huo ujauzito ni kama baraka kwenu. Mipango ya Mungu daima huwa haina dosari japo kama wanadamu huwa hatuoni mpaka jambo jema litokee mbeleni.
Kila heri mkuu.
Kwakua ndoa sina tatizo nayo kabisa hivyo sikuona haja ya kukusumbueni.Mbona ulipokuwa unataka kufunga ndoa hukutuomba tukushauri
Thanks mkuuNyuzi zinazoweza kukpmaza vijana tukaingia kwenye ndoa. Best thread ever
🙏🙏🙏🙏Mkuu i really appreciate your sharing. Thanks alot
Mbona mapema hiyo mkuu kuna wenzio huku 35 hana hata mtu wa maanaNi kweli kila mtu anaongea lake ila unapotezea,alafu nyie umri wenu bado mdogo mi mtoto wa kwanza nilipata nikiwa na miaka 31
Yeah,ila mimi nilikaa kwa relationship mda mrefu coz nilikuwa na mambo nakamilishaMbona mapema hiyo mkuu kuna wenzio huku 35 hana hata mtu wa maana