Naomba ushauri wako juu ya kipi nifanye kwa hiki kilichotukumba kwenye ndoa

Yaan mkuu hii ishu yako ni kama yetu, hata mimi nilivurugwa kiasi cha kumuuliza hivyo wife like "au kuna mistake umefanya huko ndio maana unalia" hapa sasa nikachochea moto
 
Sawa sawa chief..kumbe hii ni experience ya watu wengi kidogo kwenye ndoa!!.. napata mwangaza sasa, na ninashukuru wadau kuniweka wazi maana inanitia moyo
 
Yaan mkuu hii ishu yako ni kama yetu, hata mimi nilivurugwa kiasi cha kumuuliza hivyo wife like "au kuna mistake umefanya huko ndio maana unalia" hapa sasa nikachochea moto
Inabidi muwe strong nyie bora mkubwa,mimi ndo kwanza alikuwa na miezi sita,nilipambana mtoto nikamnyonyesha huku na mimba yangu karibia najifungua ndo namuachisha baada ya kujifungua unasahau.
 
Inabidi muwe strong nyie bora mkubwa,mimi ndo kwanza alikuwa na miezi sita,nilipambana mtoto nikamnyonyesha huku na mimba yangu karibia najifungua ndo namuachisha baada ya kujifungua unasahau.
Dada angu kweli wewe ulipambana, mtoto wa miezi 6 naamin kabisa haikua rahisi.
Hapo huwa tunaumizwa na mitazamobya watu, kwamba watatuonaje hawa? Kwamba tunapemda sanaaa mpaka hatuzingatii masuala ya msingi?
 
Ushauri.
Mmoja au wote mfunge kizazi, au wife atumie zile njia za kuzuia uzazi.
Mungu alikupa mwanaume uwezo wa kumjaza mimba mwanamke hata ukiwa na miaka 90, lakini mwanamke 40 tu kupata mimba ni mbinde.

Halafu anakuja mtu anakushauri mwanaume eti kufunga kizazi. Never
 
Hebu naomba uni PM
 
Dada angu kweli wewe ulipambana, mtoto wa miezi 6 naamin kabisa haikua rahisi.
Hapo huwa tunaumizwa na mitazamobya watu, kwamba watatuonaje hawa? Kwamba tunapemda sanaaa mpaka hatuzingatii masuala ya msingi?
Ni kweli kila mtu anaongea lake ila unapotezea,alafu nyie umri wenu bado mdogo mi mtoto wa kwanza nilipata nikiwa na miaka 31
 
Kilichokukuta wewe ni kama ambacho kilinikuta mimi miaka 4 iliyopita. Mimi na mke wangu tumejaaliwa watoto 4 kwa sasa.

Plan ya kwanza ilikuwa tuwe na watoto wawili tu. Ila kwa bahati wote wawili walikuja wa kiume. Tukakubaliana tujaribu mara moja ya mwisho napo pia akapatikana wa kiume.

Tuliamua rasmi kuwa kuzaa basi tena. Mke wangu aliweka kitanzi lakini kikawa na madhara makubwa kwake kiafya, akaweka kijiti halkadhalika ikawa na matatizo, akaishia kwenye vidonge vya majira.

Kuna kipindi alipata blood infection kupelekea kutumia antibiotics ambazo kitaalam inasadikika huudhofisha nguvu ya vidonge vya majira. Baada ya muda ikawa hajielewi ikabidi kupima ujauzito na kukuta imo.
Hicho kipindi kilikuwa ni kigumu mno maana iilikuwa kipindi cha Covid, kipato kilitetereka na bado ujauzito umekuja.

Mungu anisamehe, nilimwambia mke wangu atoe ujauzito na mpaka kumfanyia booking ya abortion. Mwanzo alikubali lakini dakika ya mwisho kabisa akabadili mawazo yake na kukataa kabisa kutoa ile mimba. Hii ilileta mtafaruku mkubwa mno baina yetu katika ndoa. Kipindi chote cha mwanzo cha ujauzito hatukuwa sawa mpaka nililipoamua kukubaliana tu na hali halisi.

Baada ya miezi tisa mke wangu alijifungua mtoto wa kike. Mtoto ambae nilikuwa nikitamani kumpata kwa miaka.
mingi. Nafsi ilinisuta na wakati mwingine inanisuta mpaka leo.

Binadamu ni wazuri katika kupanga ya kwetu huku tukisahau kuna mamlaka yenye nguvu zaidi yetu na kila kitu hutokea kwa matakwa yake.
Binti yangu alizaliwa July, 2020, January 2021 mke wangu alipata message instagram toka kwa ad agency kupitia kwenye account ambayo alimfungulia mtoto kama wafanyavyo ma mama wengi. Walitaka kutumia picha za mwanangu kwenye matangazo ya vitu vya watoto.

Mwanzo nilidhani utani lakini baada ya kuangalia account ya huyo mtu ya instagram nikagundua ni ya kweli kutoka Kenya. Process iliyofuatwa ilikuwa ni mkataba wa miaka miwili ambao uliisha January 2023. Malipo hayakuwa makubwa sana ila kwa kipindi hicho ilitusaidia mno kusogeza maisha mbele.

Inawezekana mwanao asije kupata mikataba ya kazi akizaliwa tu kama wangu lakini kila jambo hutokea kwa sababu zake. Mpe moyo mke wako na chukulia kuwa huo ujauzito ni kama baraka kwenu. Mipango ya Mungu daima huwa haina dosari japo kama wanadamu huwa hatuoni mpaka jambo jema litokee mbeleni.

Kila heri mkuu.
 
Ni kweli kila mtu anaongea lake ila unapotezea,alafu nyie umri wenu bado mdogo mi mtoto wa kwanza nilipata nikiwa na miaka 31
HApo nimekuelewa vyema mkuu. Ahsante sana.
Mimi bwana ujana mwingi, mtot wa kwanza nimepata chuo niko na kama 21 yrs hiv πŸ˜‚πŸ˜‚.
 
Mkuu i really appreciate your sharing. Thanks alot
 
Kuna pahala umekosea.

Sisi tulikuwa tunafanya kazi ya kulipwa kwa performance, malipo ya ile kazi ilikuwa watu wakiwa wengi malipo kiduchu ila wakiwa wachache malipo makubwa, Guess What...Tulikuwa tunapiga vita mfanyazi kuongezeka ila endapo Bosa alimleta tu anakuwa mwenzetu hatumkatai tena maana ni mwenzetu maana ukimkataa tena hukatai kuongezwa mfanyakazi mpya bali unamkataa mtu SPECIFIC ambae ni JUMA, HAMIS au EMMA sawa na kutaka afukuzwe kazi...CONCEPT NINI ??

Kukataa mtoto kabla ajawa mimba ni sahihi maana huyo mtoto anakuwa bado hana IDENTITY maan hio ina belong kwa watoto wote ambao wajazaliwa bado Duniani ila kumlataa mtoto au kumsema baada ya kuwa mimba tiali hapo sasa unamsema mtoto SPECIFIC ambae yupo has na ni wako.

Namaanisha huyo mwanao ambae ni mimba tiali anauhai na ni wako, kuandika uzi kama huu tu na ulichoeleza maanake ujawa radii na huyo mtoto kifupi ushamkataa ila huna namna hii kama liana kwake.

Ulikuwa na haki kusema kwasasa sihitaji mtoyo mwengine ila una haki tena once mimba ishatungwa hapo STATEMENT IMEBADILIKA hukatai kuwa na mtoto mwengine tena bali unakataa mwanao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…