Naomba ushauri wako nasaha juu ya kufikia malengo ya kuku elfu 5 ndani ya mwaka mmoja na miezi sita

Asantee mkuu.
natamani kukufundisha mengi juu ya huo ufugaji lakini ni mambo mengi na nikianza hapa kumaliza ni ngumu kupitia reply moja kikubwa ukitaka kufuga kwanza ni vyema kujua namna ya kuwakinga mifugo yako na magonjwa,wadudu udumavu na ubora wa kile unacho kifuga
kuna vitu huwezi vipata kupitia vitabu bali ni kupitia pale unapofanya
nakushauri anza kumsoma kuku kwanza,hakika hutoyumbishwa nakwambia hivyo kwani na utalamu juu ya hayo mambo kwa zaidi ya miaka 25 nimemsoma kuku kunzia niko kidato cha kwanza, adv katika somo la AGRI sahivi nafikiri limefutwa pale galanos

piga hesabu za ulishaji jua njia za kukata gharama bila kuharibu production, soko lipo endapo kuku wako mtu akiwaona wanavutia.na kwa hiyo idadi kubwa unayotaka kuwa nayo hakikisha unapesa ya kuwalisha hao kuku kwa miezi mitatu mbele hii itakusaidia kutoyumbishwa sokoni
 
Dah..unaweza pata ugonjwa wa moyo..pole sana
 
EEeeenHeeeee!
Huo mstari wako wa mwisho umenifanya nicheke kabisa.

Hapana, hao wenye elimu ya namna hiyo wapo Tanzania pekee.

Nikutahadharishe tena; kama utatekeleza (kwanza siamini) ulivyoyaweka hapo kwenye mada yako mwanzoni, jihesabu kuwa hasara sehemu ya juhudi zako.
Kama wewe hujali hasara na kupoteza muda, basi endelea kama ulivyopanga mwenyewe.

Ningekuelewa kama ungekuja hapa katika mada hii na kusahihisha makosa yaliyo wazi katika mpango wako huo, hapo ningekuelewa kidogo na mada yako ingeleta maana.

Lakini kung'ang'ania hapa mpango usioweza kuleta ufanisi, ni kama huu wako na kujidai kuutekeleza, inaondoa kabisa maana ya wewe kuleta mada yako hapa.

Ni kama hakuna lolote unalojifunza, na huku wewe mwenyewe umeanza kwa kuomba ushauri.

Vuta pumzi, angalia upya uliyopanga, na sahihisha yaliyo wazi kusahihishwa katika mpango wako wa mwanzo; kama kweli wewe unayo nia ya kufuga kama unavyodai.
 
Ndio maana Mimi najaribu Kwa mara nyingine ila Kwa makubaliano ya kungawia 40% ya faida
LOOooh!

Jameni, ufugaji huu unawezekana kweli?

Unao kuku wangapi mkuu 'Fursakibao'?

Hata kama kuku hao wangetaga kimiujiza, sasa utapewa taarifa kwamba kuku wamepunguza kutaga; kumbe nusu ya mayai yanayotagwa yanawekwa pembeni.
Sasa hiyo faida sijui itatoka wapi?

Ndiyo maana nasema, kwenye hizi mada hapa JF ni za kujifurahisha tu!

Kwenye mada hii hii kwa mfano, sijasoma mchango wowote ambao ninaweza kusema umekaribiana na hali halisi ya ufugaji unaoweza kuingiza faida katika kazi hiyo.

Nitaonekana kama ninakatisha watu tamaa wasitekeleze ndoto zao hata kama ndoto hizo ni za kusadikika tu, kama ilivyo letwa mada hii tunayoijadili sasa.
 
Ndio maana Mimi najaribu Kwa mara nyingine ila Kwa makubaliano ya kungawia 40% ya faida
Kwa mtindo huo utafanikiwa, sikuhizi biashara ya kumsindikiza mtu kwenye utajiri hakuna 😀!

Ni ama twende wote au niende mimi we ubakie nyuma. Ila sio mie nikupeleke wewe halafu nibakie pale pale. Kila mtu anataka maisha mazuri.

Kuna shemeji yangu ana mradi mkubwa sana wa almost kuku 20,000 kwa sasa sema yeye ni wa nyama wale. Ameajiri manager anamlipa 4M kila mwezi. Yeye ana tender interchick kuwazalishia kuku na wanapiga hela haswaa maana Meneja anafanya kazi kweli kweli.

Hivyo ndio jinsi ambavyo biashara inatakiwa kufanyika sio mambo ya wewe kukutengenezea million 30 kila mwezi halafu mie unipe laki na nusu. Hatuendi hivyo ila kwa percentage utafanikiwa.
 
Ukiwaza sana utakata tamaa kabisa.
 
Ni dm aisee, maana kwenye miradi ya kuku kuna mengi sana na lazima machache uyajue. Kufika kuku 5k ndan ya mwana mmoja sio shiida ila ni kipato chako tuu japo hao kuku n wengi sana sana hivo waza gharama za chakula, wafanyakaz na materials mengine kwaajili ya hilo shamba lako.
 
Wew unataka ujue Ela aliyonayo bank ili iweje kama sio Uchawi na chuki
Personal details za biashara zake zingine zinakuhusu Nini !?
Wabongo kama ninyi wajinga sana
 
Kuku 100 watakuchelewesha;Anza na mia 300 angalau. Bajeti ulioitaja hapo inatosha Hadi kuku 500 Kwa mwezi.

Usitake kujifunza utaumia. Tumia wataalamu hakikisha vifaranga vinapata chanjo zote nitakuwekua list hapa ya chanjo na mda wa kuchanja
Mwaga nondo hapa
 
Hio bei ya kuku ni ya wapi hio? Fanya utafiti ili usije lia baadae.

Sikiliza Soko zuri la kuku chotara na hao wa Kienyeji ni kuwauzia watu individual hawa wanunua kwa sh 20, 000/ wala sio hio 35, 000/ na pia hawa ni mmoja mmoja mmoja yaani ni mtu mmoja mmoja.

Soko kubwa ni la kuuza kwa mkupuoa sasa bei ya mkupuoa ni sh 10, 000/ hata chini ya hapo, hao ndio wanaweza chukua kuku hata 50 au 100.

Hakuna mtu wa mkupuo atanunua kuku kwa sh 20, 000/ au 35, 000/

Mayai yenye soko ni mahai ya kuku wa kisasa, fanya utafiti Dar hapo, mayai ya kienyeji ni ya familt level napo ni mmoja mmoja mteja.

Kuku wa Kienyeji ili uwafuge unapaswa kuwa na shamba kubwa na uwaachie humu na usiwe unawawazia yaani kwamba ndio unawategemea watoto wale hapo itakula kwako.

Kuku wa Biashara ni Layers na Broilers basi
 
Wew unataka ujue Ela aliyonayo bank ili iweje kama sio Uchawi na chuki
Personal details za biashara zake zingine zinakuhusu Nini !?
Wabongo kama ninyi wajinga sana
EEEeeenHeeeee!
Ona huyu mlevi, sijui anatafuta kitu gani huku JF. Umeona wapi nikiuliza 'details' hizo unazodai wewe?

Sasa ushauri wako kwake ni nini, akalewe kama ulivyolewa wewe?

In fact, wewe siyo mlevi, wewe ni chizi.
 
Wewe ni mzungu wa roho , haki na ibaki kwako daima
Pole kwakuwa hii ni Africa watu kaliba yako wanaitwa wenye roho mbaya na chuki binafsi ila hongera sana .NIMEPENDA
 
EEEeeenHeeeee!
Ona huyu mlevi, sijui anatafuta kitu gani huku JF. Umeona wapi nikiuliza 'details' hizo unazodai wewe?

Sasa ushauri wako kwake ni nini, akalewe kama ulivyolewa wewe?

In fact, wewe siyo mlevi, wewe ni chizi.
Huna mchango kwa Taifa kaa pembeni
 
Kwa hali ya hewa ya Tanga ni joto na hayo mabanda yako umeyajenga mafupi mno hili litapelekea kuku kutopata hewa nzuri na hupelekea vifo kwa kuku

Kwaio mm ushauri wangu ni bora ungeyarefusha mabanda hyo na uweke madirisha makubwa ili hewa iingie vizuri

Nakushauri hivi bcz yashanikuta
 
Halafu kitu kingine kuhusu soko

Kuku chotara akishafika mkubwa hna soko sana kma broilers hawa kuku lbda utegee msimu wa skukuu ndo uuze iyo bei ya 30000 na kweli utpta pesa ila kma untka kuku wa biashara fuga broilers tu ambao ndani ya mwezi unauza

Kma utategea kipindi cha skukuu tu hao kuku utauza kweli kweli ila kma unavofikiria ww hawatokulipa niamini nakwambia haya sitaki uje kuuchukia ufugaji wa kuku mna umesema huna uzoefu nao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…