EEeeenHeeeee!
Huo mstari wako wa mwisho umenifanya nicheke kabisa.
Hapana, hao wenye elimu ya namna hiyo wapo Tanzania pekee.
Nikutahadharishe tena; kama utatekeleza (kwanza siamini) ulivyoyaweka hapo kwenye mada yako mwanzoni, jihesabu kuwa hasara sehemu ya juhudi zako.
Kama wewe hujali hasara na kupoteza muda, basi endelea kama ulivyopanga mwenyewe.
Ningekuelewa kama ungekuja hapa katika mada hii na kusahihisha makosa yaliyo wazi katika mpango wako huo, hapo ningekuelewa kidogo na mada yako ingeleta maana.
Lakini kung'ang'ania hapa mpango usioweza kuleta ufanisi, ni kama huu wako na kujidai kuutekeleza, inaondoa kabisa maana ya wewe kuleta mada yako hapa.
Ni kama hakuna lolote unalojifunza, na huku wewe mwenyewe umeanza kwa kuomba ushauri.
Vuta pumzi, angalia upya uliyopanga, na sahihisha yaliyo wazi kusahihishwa katika mpango wako wa mwanzo; kama kweli wewe unayo nia ya kufuga kama unavyodai.