Naomba ushauri wako nasaha juu ya kufikia malengo ya kuku elfu 5 ndani ya mwaka mmoja na miezi sita

Naomba ushauri wako nasaha juu ya kufikia malengo ya kuku elfu 5 ndani ya mwaka mmoja na miezi sita

Kwanza kuku chotara usinunue kwa wafugaji, kama kuroiler nunua moja kwa moja kwenye kampuni yao AKM Gliters, saso ile kampuni nimesahau jina au tanbro wa interchick, pia ukitaka mradi ukue haraka nunua incubator , tengeneza mabanda ya kulelea vifaranga ya kisasa ambayo vifaranga havitapata magonjwa kirahisi..
kwa kuku wa kienyeji nunua matetea ata mia mbili kidogo kidogo, wakiwa wanataga mayai unaweka kwenye incubator usiwaruhusu walalie wakitaka kulalia wanaweka kwenye maji ili zile dalili za kulalia zipotee baada ya wiki mbili anaanza kutaga tena .
wazo zuri.
 
Mimi hata sikuagwa nikiambiwa baada ya siku tatu kuku wamefungiwa Banda.

Ikabidi nimtume mtu akawahamushie Kwa Kwa jamaa yangu; niliemtuma nae akanipiga na kitu kizito; huko nako nilikopelekwa ikawa shida.

Nilianzw na kuku wa kienyeji 20 mpaka kijana anaondika walikuwa 170+ niliokuja kuambulia ni 15 tu
Pole mkuu.
 
Halafu kitu kingine kuhusu soko

Kuku chotara akishafika mkubwa hna soko sana kma broilers hawa kuku lbda utegee msimu wa skukuu ndo uuze iyo bei ya 30000 na kweli utpta pesa ila kma untka kuku wa biashara fuga broilers tu ambao ndani ya mwezi unauza

Kma utategea kipindi cha skukuu tu hao kuku utauza kweli kweli ila kma unavofikiria ww hawatokulipa niamini nakwambia haya sitaki uje kuuchukia ufugaji wa kuku mna umesema huna uzoefu nao
Asante kwa ushauri.
 
Kwa hali ya hewa ya Tanga ni joto na hayo mabanda yako umeyajenga mafupi mno hili litapelekea kuku kutopata hewa nzuri na hupelekea vifo kwa kuku

Kwaio mm ushauri wangu ni bora ungeyarefusha mabanda hyo na uweke madirisha makubwa ili hewa iingie vizuri

Nakushauri hivi bcz yashanikuta
Nimechukua ushauri wako kaka.
 
Ni kweli sababu mtu mwenye exposure kukuingizia hela ndefu halafu umlipe 140K ni ngumu. Utapigwa utachakaa
Mkuu kheri kufanya kisha ukifeli utanya tena kuliko kutofanya kabisa. Mimi ndio naanza nahitaji nijibane na angalau kila siku nne za wiki nipo Tanga kwa sasa mpaka 2027, kwahio ntakua na uangalizi mzuri tu.
 
Kwa mtindo huo utafanikiwa, sikuhizi biashara ya kumsindikiza mtu kwenye utajiri hakuna 😀!

Ni ama twende wote au niende mimi we ubakie nyuma. Ila sio mie nikupeleke wewe halafu nibakie pale pale. Kila mtu anataka maisha mazuri.

Kuna shemeji yangu ana mradi mkubwa sana wa almost kuku 20,000 kwa sasa sema yeye ni wa nyama wale. Ameajiri manager anamlipa 4M kila mwezi. Yeye ana tender interchick kuwazalishia kuku na wanapiga hela haswaa maana Meneja anafanya kazi kweli kweli.

Hivyo ndio jinsi ambavyo biashara inatakiwa kufanyika sio mambo ya wewe kukutengenezea million 30 kila mwezi halafu mie unipe laki na nusu. Hatuendi hivyo ila kwa percentage utafanikiwa.
Mkuu biashara kama unaianza huwezi mlipa mtu hivyo, kwanza unakua huna uhakika wa mambo mengi nsa vingi tunavyoweka kwenye mpango kazi ground hua tofauti.
 
We jamaa,una ndoto nzuri,ila nikuambie huwezi kufuga kuku chotara na kienyeji kwa idadi hiyo unayotaka bila kuwa na eneo kubwa kwa kifupi Shamba.Tena lisipungue heka 3.

Kufuga kuku Chotara na kienyeji utegemee kuwalisha kwa chakula cha dukani kwa muda wote ni hasara.Ni hasara kwa sababu hawakui kwa haraka kama broiler,

Na kwa vile unataka kuwafugia kwenye mabanda maana yake lazima uwanunulie chakula cha dukani kila mara

Shamba ni la nini?

Shamba hilo litakusaidia wewe kupunguza gharama za ulishaji kwa wewe kulima mazao ya kuwalisha kuku wako,.Mazao kama Mahindi,mtama uwele na Alizeti.Na pia utapanda majani na kutengeneza Azola pia Funza kwa ajili ya protein,

Pia Shamba hilo hilo litatumika kuwaachia kuku wako free waokote chakula mashambani kuliko kuwafungia ndani muda wote.

Kumbuka kuwa kwa idadi hiyo ya hao kuku maana yake utahitaji eneo la kutupia mbolea.So ukiwa na Shamba maana yake hutapata shida kwa kuhifadhi mbolea,na utalima bustani.

Cha mwisho hakikisha unaajiri Daktari wako kwa ajili ya kuwaangalia hao kuku kila siku
Ushauri mzur Sana huu
 
Mkuu kheri kufanya kisha ukifeli utanya tena kuliko kutofanya kabisa. Mimi ndio naanza nahitaji nijibane na angalau kila siku nne za wiki nipo Tanga kwa sasa mpaka 2027, kwahio ntakua na uangalizi mzuri tu.
Hapo utafanikiwa anza kusimamia mwenyewe tu
 
Ndio unatakiwa usimamie hadi uweze kulipa watu
Hao wenye elimu kubwa siwahitaji Kwa Sasa, nahitaji mtu alieishia form four tu na akafeli. Siku mambo yakiwa mazuri ntatafuta hao wanaohitaji mishahara mikubwa Sasa kulingana na namna mradi unavyozidi imarika.
 
EEEeeenHeeeee!
Ona huyu mlevi, sijui anatafuta kitu gani huku JF. Umeona wapi nikiuliza 'details' hizo unazodai wewe?

Sasa ushauri wako kwake ni nini, akalewe kama ulivyolewa wewe?

In fact, wewe siyo mlevi, wewe ni chizi.
Samahani lakini, Kwani wewe ni wakike?
 
The best thing ni kuanza. Anza,anza, anza.Umeanza na kuku wachache songa nao. Let them grow gradually while you are learning.
Aliekuambia eneo ni dogo mzingatie sana. Nimewahi ona you tube watu wanaofanya grazing, Yani unaziswaga tu kwenye eneo lako kubwa zinashiba it's a little bit crazy!
Andaa chakula chako, hasa mahindi yatapunguza gharama kwa robo nzima ya gharama ya chakula.
SASA sio waziri kwa maya, wanakula sana labda kwa ajili ya kuku wazazi tu.
Fuga ng'ombe wa maziwa walau 4tu, hawa huita wadudu na hasa kwa kuku wa kienyeji.
Farming is an art, every day you create new way to solve daily problems. Kufuga nayo ni hob,tayari unayo, hivyo furahia unachokifanya Mwanzoni hakilipi but it make you enjoy.
Mwisho, oa,oa is Kama hao mabinti ni watulivu chagua mmoja maana hobi zenu zitakuwa sawa yaani wafugaji. Miaka 32 si verma ukawa huna mke wala mtoto, hivyo vitu si muda mrefu vitahitaji sapoti ya mke na watoto. Utachelewa kufanya naturing kwa watoto na mke, ni muhimu Waone how you grow from zero to rich kuliko wazaliwe wakute wewe ni welloff.
 
Binafsi nimekusoma sana mkuu. Naiona comintment kubwa ndani yako. Shida ya Jf hasa jukwaa letu linakosa kabisa mrejesho sijui shida huwa ipo wapi. Mfano uzi maarufu wa nimeamua kulima mara ya pili hauna kabisa mrejesho zaidi ya miaka 10 sasa... nakutakia ufugaji mwema twende malawi tukatafute kuku next weak
 
Binafsi nimekusoma sana mkuu. Naiona comintment kubwa ndani yako. Shida ya Jf hasa jukwaa letu linakosa kabisa mrejesho sijui shida huwa ipo wapi. Mfano uzi maarufu wa nimeamua kulima mara ya pili hauna kabisa mrejesho zaidi ya miaka 10 sasa... nakutakia ufugaji mwema twende malawi tukatafute kuku next weak
Hatariii mkuu mapambano yanaendelea. Ingawa sio rahis lkn tunaendelea kupambana.
 

Attachments

  • VID-20240125-WA0004.mp4
    5.3 MB
EEeeenHeeeee!
Huo mstari wako wa mwisho umenifanya nicheke kabisa.

Hapana, hao wenye elimu ya namna hiyo wapo Tanzania pekee.

Nikutahadharishe tena; kama utatekeleza (kwanza siamini) ulivyoyaweka hapo kwenye mada yako mwanzoni, jihesabu kuwa hasara sehemu ya juhudi zako.
Kama wewe hujali hasara na kupoteza muda, basi endelea kama ulivyopanga mwenyewe.

Ningekuelewa kama ungekuja hapa katika mada hii na kusahihisha makosa yaliyo wazi katika mpango wako huo, hapo ningekuelewa kidogo na mada yako ingeleta maana.

Lakini kung'ang'ania hapa mpango usioweza kuleta ufanisi, ni kama huu wako na kujidai kuutekeleza, inaondoa kabisa maana ya wewe kuleta mada yako hapa.

Ni kama hakuna lolote unalojifunza, na huku wewe mwenyewe umeanza kwa kuomba ushauri.

Vuta pumzi, angalia upya uliyopanga, na sahihisha yaliyo wazi kusahihishwa katika mpango wako wa mwanzo; kama kweli wewe unayo nia ya kufuga kama unavyodai.

Mkuu bado mapambano yanaendelea ingawa kufikia malengo bado sana, lakini sihaba kunajapo hatua Moja imepigwa.
Mwalimu bado naendelea kujifunza kupitia ukosowaji wako. Lakini dhamira ni ile ile kuku 5000 lazima wafikiwe ingawa sikwamuda ule niliotarajia.
 
Back
Top Bottom