Ninacho amini kutoka kwako; ni kweli wewe ni kijana mdogo usiyekuwa na uzoefu wowote katika maswala haya ya ufugaji. Sina hakika sana na hizo biashara zako nyingine ulizozitaja hapo mwanzo.
Mategemeo yangu ni kwamba, hata uzoefu tu wa hizo biashara unazodai zinazalisha pato, zingeweza kukupa mwanga tofauti kabisa na haya unayotaka kuyafanya kwenye ufugaji wa kuku.
Kwa mfano: huwezi kwenda kuanza biashara na kufanya utafiti hapo hapo kwa mambo ambayo wengine walishayafanya siku nyingi na taarifa zake zipo wazi.
Wewe hutakuwa mtu wa kwanza kufanya biashara ya hawa kuku, ya nini upoteze muda na upate hasara kwa jambo ambalo tayari linajulikana?
Hili ndilo linalonipa mashaka kuhusu ukweli wa habari yako ya hii biashara na mada nzima kama ulivyoileta hapa.
Nadhani umeamua tu, kuleta andiko, watu wajifurahishe kujibu vyovyote wanavyoona wao.
You're not serious.