Naomba ushauri wenu juu ya haya magari ya kutumia Umeme yaliyoingia nchini, nimeyapenda kwa mazingira ya sasa

Inafaa uwe na betri 2
 
Nafikiri hiyo ndo future. Betri zitakuwepo tu na vituo vya kuzijaza zinapoisha. Ukiingia kwenye kituo unampa empty betry anakupa full betry. Huko mbeleni nadhani binadamu wataachana na magari ya mafuta.
Ulaya sasa hivi magari ya umeme yapo kila kona. Makampuni mengi ya magari sasa hivi wanatoa matoleo mapya mengi ya magari ya umeme. Kuna nchi zimeshajiwekea baada ya miaka 15 kutoka sasa magari yote yatakuwa ya umeme. Ila kwa Tanzania sihsauri mtu anunue gari ya umeme kwa sasa. Hasara ni kubwa kuliko faida.
 
Ukinunua uwe na backup car. D4 engine na hybird zenyewe bado zinaogopeka.
 
Magari mengi ya umeme betri zake ziko fixed na kuitoa ni shughuli. Haziwekwi kama betri za tochi!
Hio haifai bora wabuni mfumo wa betri 2 sawa na baadhi ya magari yenye tank 2 za diesel.

Pili...why hizo gari hazima mfumo wa otoneta ziwe zinajichaji ukiwa una drive?
 
Chukua la umeme na mafuta maana ishu iko kwenye battery.. Battery ikifa sio chini ya million mbili kwa moja..!
Ishu nyingine hapo ni converter nayo ikifa ni shida.. Yaani inayobadili umeme kwenda mafuta na kinyume chake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…