Naomba ushauri wenu juu ya haya magari ya kutumia Umeme yaliyoingia nchini, nimeyapenda kwa mazingira ya sasa

Naomba ushauri wenu juu ya haya magari ya kutumia Umeme yaliyoingia nchini, nimeyapenda kwa mazingira ya sasa

Yaani watembea km 200 tu betri imeisha, kisha uchaji betri kwa karibu saa 10! Duh, kwa hiyo hayo masaa 10 unakuwa umepaki wasubiria betri lijae au unakuwa upo kwenye mwendo betri lajichaji automatically?!

Pengine labda itabidi uwe na betri zaidi ya moja (angalau tatu hivi) ukizingatia na umeme wetu wa kuunga unga
Hizo battery sio n200 😀😀😀😀😀😀😀. Kwa utafiti wangu gari za umeme, battery ni pana inacover sehemu ya viti vinne vya gari na inakuwa upande chini wa gari.
1657533084972.png
 
Nimeyakagua pale maonesho ya Sabasaba

La Mwanza ni Nissan saloon linatumia umeme 100%
Ni mtumba
Betri ikiwa full unatembea km 200
Betry inachajiwa kwa saa 8 hadi 15

Ya pili ni Toyota
Inatumia Umeme na Petrol
Lita moja ya Petrol unatembea km 25

Hawapo barabarani hayana muungurumo zaidi ya kupiga honi tu

Bei yake moja

Ushauri tafadhali lipi litafaa zaidi katika mazingira ya Tanzania

Natanguliza shukrani
Mie nina ungo, hauhitaji chaji wala mafuta!
Kufika Bariadi sekunde tu.
 
Cost za mafuta kwa kuendesha hizo 2OOkm ni juu kuliko gharama ya umeme. Huenda ukatumia umeme wa elfu kumi tu kuzimaliza hizo km zake ila
petrol ingekugharimu mafuta si chini ya elfu 5O,OOO
 
Cost za mafuta kwa kuendesha hizo 2OOkm ni juu kuliko gharama ya umeme. Huenda ukatumia umeme wa elfu kumi tu kuzimaliza hizo km zake ila
petrol ingekugharimu mafuta si chini ya elfu 5O,OOO
Future ipo kwenye EVs, makampuni makubwa ya magari pamoja na makampuni makubwa ya vifaa vya umeme (Sony, Apple) wanawekeza nguvu huko. Ni suala la muda tu, improvement kwenye ubora wa battery na charging utaboreshwa huko mbeleni. Naimani kuna watakao vuka 1000km per single charge.
 
Hio ikifika kuwa industrial standard basi ICE cars ndio zitakuwa zimeumaliza mwendo. Wese litabakia kwenye kuendesha mitambo tu.

Kwa sasa mchina ndio ana lead kufyetua vitu vya umeme kuna kagari kake kana clock 8OOkms ila haijathibitishwa japo in real life watu wanasema kataishia around 639kms
 
Hio ya kuchajia nyumbani ndio ya kuchukua masaa 8-10. Ila dedicated charging plant ya fast charge ni ndani ya lisaa ishajaza
Inategemea pia na aina ya gari. All in all kwa Tanzania ukinunua gari la umeme inatakiwa ''ujue unachokifanya'' siyo kujinunulia tu.
 
Mzigo unawasha umeme wa nyumba kabisa.
Kwangu natumia unit moja kwa siku nzima nikizid sana ni 1.4kwh hapa kama friji na jagi limetumika sana... Huo umeme ninaotumia kwenye gari hukifikish kilometa kumi

Imagine battery pack ya tesla yenye 100kwh huo ni umeme kwangu wa miezi miwili kabisa
 
Yes, nilikuwa napitia review ya ford f-150, EV version au Ford lightining wanasema umeme ukikatika wa manyumbani inakuwa back up ya umeme wa Nyumba vizuri.
1657553018138.png
 
Gari za umeme betri iko fixed. Kuitoa mpaka upeleke kwa fundi na ni shughuli hivyo ondoa wazo la kusema utatembea na betri za akiba kama tochi. Nchi zilizoendelea wanachofanya ni kuweka vituo vya kuchajia vingi njiani. Kwa mfano utoke Mwanza kuja Dar unakuta kuna vituo vingi njiani.
hii sasa ni fursa kubwa sana kwa shirika letu pendwa la Tanesco,muda huu ndio wangetumia kutuma wataalamu wake kwenda nje kujifunza jinsi mfumo huo utakavyokuwa wa kuchaji magari ya Umemena wao kuanza kuweka stand za kuchajia,tena hii fursa wakiitumia vizuri ndio litakuwa shirika lenye pesa nyingi kuliko taasisi nyingine
 
Ila tujiandae tu, magari ya umeme hayatakuwa nafuu kwenye upande wa tozo na kodi za kila mwezi au mwaka, kwa sababu yanaenda kupunguza mapato ya serikali kwenye mafuta. Hivyo mbadala wake ni kuongeza au kubuni kodi kwenye magari ya umeme ambayo itakuwa mbadala wa mapato yatakayopotea kutokana na kupungua kwa utumiaji na uaguizaji wa mafuta kwa ajili ya magari.

Naona ndio kipindi serikali itaweza kupunguza au kuondoa kabisa kodi kwenye uagizaji wa magari ya mafuta na kuongeza kodi kwenye uagizaji wa magari ya EV ili kuhakikisha inapata watumiaji wa mafuta na wachache wa EVs.
 
Magari ya umeme hayafai safari ndefu mkuu labda tesla ambayo ukichaj unaenda hadi 600kms. Ila haya mengine ukiondoka asubuhi kwenda kazini ukirudi unalaza chaj usiku
 
Ile ya Umeme na Petrol betry inajichaji automatically

La Umeme tupu ni lazima ulichaji ukiwa umepaki
Sasa masaa nane 8 ndio inakuwaje aisee?! Yaani nakaa kusubiria gari ijae masaa nane then hiyo safari itembee 200km mmmmmmhmn?! Hapo tayari wamefeli kufikia malengo ya ubora.
 
Nafikiri hiyo ndo future. Betri zitakuwepo tu na vituo vya kuzijaza zinapoisha. Ukiingia kwenye kituo unampa empty betry anakupa full betry. Huko mbeleni nadhani binadamu wataachana na magari ya mafuta.
Me hapana ziwezi kuyaacha. Nishazoea purukushani za sheli.
 
Back
Top Bottom