Biashara ya kuku wa mayai sio mbaya katika uwekezaji, ila ushauri wangu Anza na kuku wachache kwanza hata kama una mtaji mkubwa, Hawa sio kuku wa nyama kuwalisha Hawa viumbe mpaka waanze kutaga inachukua miezi mpaka 6, Hawa wajomba hawalali kazi Yao kubwa iliyowaleta hapa duniani ni kupiga msosi, na gharama za vyakula vyao na vitamin na dawa za kuwachanganyia kwenye maji zimepanda pia.... Kwa hiyo unaweza kukimbilia kuwafuga wengi badae ikawa mtihani katika kuwafuga.
Nimeona watu wengi wakiwauza kabla hawajataga baada ya kushindwa kuwahudumia mpaka mwisho.
Tahadhari nyingine tafuta sehem au namna umeme uwe wa uhakika Hawa kuku umeme ukikatika ni wajinga sana watatafuta Kona Moja watarundikana na kulaliana kesho unaweza Kuta hata 50 wamekufa kwa kulaliwa na wenzao, sehemu iwe tulivu, kwenye paa lao akitokea hata mtoto mtundu akarusha jiwe watalaliana sehemu Moja kwa hofu na watakufa wengine.
Uwe na roho ngumu kidogo, kuna kaupepo ka ugonjwa kakipita wao kufa hata 30 Kila siku sio jambo la ajabu sana, lakini Mungu akisaidia inalipa maana wakianza kutaga unaongeza na mke wa pili kabisa😃😃
Nimeona nikupe baadhi ya changamoto chache wengine wataleta mengine