Naomba ushauri wenu, nataka kwenda kwa mganga

Naomba ushauri wenu, nataka kwenda kwa mganga

mimi mtakatifu

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2019
Posts
248
Reaction score
539
Nipo kwenye miangaiko ya maisha kwa muda wa miaka miwili sasa baada ya kupoteza kazi.

Maisha yamekuwa magumu sana nimetumia akili, maarifa na kila ujanja lakini hali inazidi kuwa mbaya.

Kila kitu sasa nimekuwa nakipata kwa shida iwe kula iwe mahitaji yoyote ya kila siku.

Mimi ni mkiristo na nimekuwa nikimuomba Mungu kila siku anitoe kwenye hii hali lakini imefika sasa naona giza mbele yangu yani nimekuwa wa kulala bila kujua kesho nikiamka nitapata wapi hela ya kula japo milo miwili ya siku.

Kwa muda mrefu watu kadhaa wamekuwa wakishauri niende kwa mganga wa kienyeji naweza kupata msaada uko. Mimi ni mgeni eneo ilo so nimekuwa nnasita pia kuna hofu fulani nnayo maana ni ulimwengu ambao uwa nausikia tu na kuna story za kuogopesha.

Ila nimekata shauri niende tu maana sina alternative kwa sasa......nachohitaji mganga wa kunisaidia kupata kazi na kufungua milango ya kuingia kwenye biashara.

Waliowai kupata kazi au deals za kimaisha baada ya kwenda kwa mganga, naombeni mnisaidie ushauri nini cha kufanya na nini cha kuepuka kufanya kupitia ulimwengu huu.

Pia wapi nitampata mtaalam sahihi wa kunisaidia asiwe mbabaishaji.
 
Pole mkuu ila jua Tu mtaa ndio ulivyo, nishaajiriwa na nikaacha kazi, nikaajiriwa tena na nikaacha na katika time zote sikuwahi kuona mambo ni rahisi kabisaaa.

Kama unaamini huko utapokwenda kutakupa wepesi kwa kuanzisha maagano na waganga, sisi ni nani tukupinge
 
Pole mkuu ila jua Tu mtaa ndio ulivyo, nishaajiriwa na nikaacha kazi, nikaajiriwa tena na nikaacha na katika time zote sikuwahi kuona mambo ni rahisi kabisaaa.
Kama unaamini huko utapokwenda kutakupa wepesi kwa kuanzisha maagano na waganga, sisi ni nani tukupinge
Nakazia
 
huko akuna unafuu kabsa ndugu naamn kwa kila kjana wa kitanzania upitia hard time kwa namna yake miaka miwil sio ming ya kukufanya upeleke kias cha pesa yako ambayo ingekusogeza sku kadhaa kumpelekea mtu ambae pia nae anawatoto apo kwake ambao hawana raman zaid ya kutwanga dawa.. Endelea kupga got na kumwomba mungu wako yawezekana anakufundisha ulpo kosea ukiwa kwenye ajira yako ya kwanza anakuondolea wale watu waliokua siosahii kwenye maisha yako ambao walkuthamn ukiwa na pesa na sasa iv hata smu hawashik ukiwapgia Pga moyo konde unavuka na kuandka hstoria kwa kipnd ulchoptia
 
"Hakuna jambo gumu linalodumu milele"

Haya maneno unifanya niamini hata leo nikilala njaa, kesho haitokuwa kama leo.

Na kweli, mambo hubadilika na kurudi kwenye mstari ingawa ni baada ya msoto na kutokwa jasho haswa.

Chochote unachokifanya/ kuamua kuna GHARAMA ya kulipia.

Kama upo tayari KUWAJIBIKA na kuwa tayari kwa kulipa gharama yoyote bila kumlaumu yeyote, fanya unachoona kitarejesha amani ya moyo wako.

Key point:

Utayari wa KUWAJIBIKA kwa namna yoyote ile pasipo kumlaumu mwingine.
 
Kama ni kuomba na kufunga hilo ni rahisi hakuna mtu anaeshindwa kufunga na kuomba, Je ni sadaka gani unaitoa kwa Muumba wako, Ni tabia gani mbaya unazozificha ukafikiri kisiri siri kwamba Mungu hakuoni? Anza kufuatilia taarifa za maisha yako hatua kwa hatua, utaja gundua mahali baraka zako zinapotokomea.
 
unataka kwenda kuomba kazi kwa mganga wa kienyeji ama mimi ndio sijakuelewa
 
Kwanza kama una nia ya kwenda kwa mganga kuwa makini na matapeli.
Mganga yoyote asikuambie umtie fedha kwanza ndo afanye huduma.
Jambo la pili ungesema uko mkoa ghn ili uelekezwe kwa mtaalamu wa karibu.
 
hakika watu tunaingia kwa waganga baada ya juhudi za kumtegemea MUNGU kwa muda mrefu bila majibu,ni vyema kutumia subira na kuongeza juhudi na maarifa ya kazi au kuhama eneo eneo kuliko kwa hao waganga hakuna jipya ,watakuingiza kwenye giza kamwe usione mwanga
 
Bro iyo kawaida uzuri umeshare ila jua watu wako na hali mbaya zaidi wengine waliacha kazi Kwa maradhi mpaka akiba ziliisha mtu unaumwa miaka 2 still una hope

Wengine sababu ya shida ndoa zimevunjika🥺🥺 maisha yanakuwa tight siku zinavyenda

Wengine Wana kila kitu lakini hawana furaha jaribu kujishikilia ulipo Kwa mganga utaishi Kwa mateso zaidi Yale una pesa lakini hauna furaha
 
Maisha yanachangamoto sana..tumia mbinu zote kupambana na hizo changamoto...sio mbaya kujaribu upande wowote unao amini utakusaidia.
Kikubwa ukitaka waganga nenda mikoani huko vijijini..achana na hawa waliojaza mabango kwenye nguzo za umeme na walioko fbk au wanatuma sms.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mtaani kwenu hakuna vile vibao vya mganga toka Nigeria?
 
Back
Top Bottom