Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HONGERA kwa kuweka kisa chako hapa! Naamini kabisa kwa kufanya hivyo utapata msaada utakaokufungua toka katika masahibu yako!Mimi ni mtu wa ibada nimekulia maisha hayo pia sina mambo mengi kwenye maisha nna vitu vichache nnavyo concentrate navyo.
Kama kuna dhambi inayosababisha haya labda ya kuzini ila sina baya la hivyo na hata wakati nna kipato mimi ni mtu wa kujitoa sana kwa wengine.
Asante sana kwa ujumbe wakoHONGERA kwa kuweka kisa chako hapa! Naamini kabisa kwa kufanya hivyo utapata msaada utakaokufungua toka katika masahibu yako!
Lakini pia Pole sana kwa unayopitia!
Inawezekana kabisa kujitoa kwako kwa wengine ndiyo kumekufikisha hapo! Unajua si kila unayempa utabarikiwa! Kuna mikono mingine ina roho ya kuua! Unampa mtu pesa inakurudishia majibu tofauti! Anaitumia pesa hiyo uliyompa kuvuta baraka zako kwake! Anatumia pesa hiyo kuiba nyota yako ya kifedha! Anaitumia pesa hiyo kuua kinachokuingizia kipato nk.
Cha kufanya ni kuzidisha maombi! Naona umekaribia kutoka kwenye huo mkwamo wa kiuchumi! Unachopaswa kufanya ni kutoa sadaka na kumuomba Mungu kupitia sadaka hiyo akakufanikishe katika mambo yako yote! Omba kwa nguvu, ikibidi funga na kemea kila roho ya mauti iliyoua kazi yako na uchumi wako ikuachie! Kata kamba za mauti zilizokufunga mikono, miguu na uchumi wako! Safisha mikono, miguu yako nk kwa damu ya Yesu naamini utarudi kwenye hali nzuri! Usikate tamaa wala USIJARIBU KWENDA KWA MGANGA! NARUDIA, USIENDE KWA MGANGA!
POLE SANA!