Naomba ushauri wenu, nataka kwenda kwa mganga

Naomba ushauri wenu, nataka kwenda kwa mganga

Bado ujamjua Mungu ukimjua huwezi kuwa masikini
 
Jaribu hii ikusaidie kuondoa umasikini.
Njia rahisi ya kuondokana na umasikini kwa mtu asiye na kipato.
Ardhi still bado ndio mtaji rahisi wa kutokea kimaisha.
Nje ya mji mapori tele yamejaa hata bure au kukodi unaweza pata safisha angalau si chini ya heka 10,panda mazao yasiyo na changamoto mfano kunde, alizeti, mtama, nk.
Chukua zao moja hili ni uhakika.
Baada ya kusafisha heka 10 au zaidi panda mmea wa nyonyo castro oil huu unavuna baada ya miezi 3 na utaendelea kuvuna kwa mda wa miaka 2.
Heka moja ya nyonyo utapata gunia 15 ukizikamua utapata lita 500 za mafuta, so heka 10 ni lita elf 5.
Jifunze kutengeneza sabuni za mche za mawingu
Lita moja ya mafuta utapata miche 2 mara lita elf 5 utapata miche elf 10.
Uza mche kwa sh 1500 mara elf 10 utapata milioni 15.
Jinsi ya kutengeneza mashine ya kukamua mbegu za mafuta tafuta bomba inchi nne tafuta Nondo mm 12 ikunje mfano wa spring ingiza ndani ya bomba mbele ya bomba ziba acha tundu dogo.Toboa toboa Bomba vitundu vidogo Ili mafuta yamwagike chini, weka mshikio wa kunyongea Ili ukamue mafuta.
Ukipata pesa kodi nyumba nenda viwandani kafunge bidhaa ambazo ni daily use kisha jaza kwenye nyumba uliyokodi kisha uwe tengeneza network na wauzaji wa dogo uwe unawasambazia bidhaa wanazoishiwa.
Kwa kufanya hivi ndani ya mwaka utakua mbali sana utaoa, utajenga, nk.
 
Yaani ni kwamba umeshindwa kabisa hata kununua chupa za maji ukajipanga pale Mbezi (kama upo Dar) jioni ukapata chochote...unachunga tu Mgambo wa Jiji, kikubwa uwe na mbio, wakija unatimua.

Hata hivyo mimi ni tofauti sana na Wengi wenu, huwa siamini kama Binaadamu Mwenzako anaweza kukurahisishia Maisha yako kwa miujiza...binaadamu tunatofautiana Karama tu, yaani kama wewe unajua sana kucheza Mpira basi Mwingine anajua sana kuchora n.k...lakini kamwe siwezi kumpa Binaadamu Mwenzangu cheo cha kufanya miujiza.

Hata hivyo sijui ni kwa nini umechagua kwa Waganga na si kwa kina Mwampesa, walau naamini kuwa wana mbinu tofauti...wakati kwa Mganga utaambiwa ukamuue Mwanao au Mzazi ili utajirike huko kwa kina Mwampesa utaambiwa ununue geleni la mafuta ya kupikia uogelee...walau hutomdhuru Mtu.

Nadhani ni bora kujaribu shughuli yoyote kwani kwa hali ya ukataji wa tamaa uliyoifikia wewe naona huna tena cha kupoteza..lakini kamwe hakuna Mtu wa kukusaidia kimiujiza kwa sababu hakuna miujiza...kama ni Mungu hata wewe ukimuomba atakusaidia huna haja ya kumfuata Mtu akusaidie kuomba.
 
Chukua zao moja hili ni uhakika.
Baada ya kusafisha heka 10 au zaidi panda mmea wa nyonyo castro oil huu unavuna baada ya miezi 3 na utaendelea kuvuna kwa mda wa miaka 2.
Heka moja ya nyonyo utapata gunia 15 ukizikamua utapata lita 500 za mafuta, so heka 10 ni lita elf 5.
Jifunze kutengeneza sabuni za mche za mawingu
Lita moja ya mafuta utapata miche 2 mara lita elf 5 utapata miche elf 10.
Uza mche kwa sh 1500 mara elf 10 utapata milioni 15.
Je bado unajishughulisha na kilimo?
 
Kabla ya kwenda kwa mganga.
Anzia kwanza wodi za hospital Kama muhimbili omba uingie emergency room uone wagonjwa.
alafu ujiulize wale waliolala wamemkosea Nini Mungu.
Mimi tangu mwaka jana mwezi wa 3 tarehe 26.sina kazi lakini naishi.
Kulala njaa kawaida ila namshukuru mungu NIPO MZIMA.
 
Huna pesa huna Kazi ukienda kwa mganga nae anataka umpe pesa kwanza ndipo akupe pesa
 
Ukifika kwa mganga ndy maisha yatakuwa magumu zaidi.

Hakuna aliyekwenda kwa mganga akakutwa hajarogwa.

Maisha ya sasa ni ku take risk ili utoboe.

Wote walio kazini,
Biashara.
Wajasiria Mali.

Bila ku take risk hitoboi.

Tusidanganyane.
 
Nipo kwenye miangaiko ya maisha kwa muda wa miaka miwili sasa baada ya kupoteza kazi.

Maisha yamekuwa magumu sana nimetumia akili, maarifa na kila ujanja lakini hali inazidi kuwa mbaya.

Kila kitu sasa nimekuwa nakipata kwa shida iwe kula iwe mahitaji yoyote ya kila siku.

Mimi ni mkiristo na nimekuwa nikimuomba Mungu kila siku anitoe kwenye hii hali lakini imefika sasa naona giza mbele yangu yani nimekuwa wa kulala bila kujua kesho nikiamka nitapata wapi hela ya kula japo milo miwili ya siku.

Kwa muda mrefu watu kadhaa wamekuwa wakishauri niende kwa mganga wa kienyeji naweza kupata msaada uko. Mimi ni mgeni eneo ilo so nimekuwa nnasita pia kuna hofu fulani nnayo maana ni ulimwengu ambao uwa nausikia tu na kuna story za kuogopesha.

Ila nimekata shauri niende tu maana sina alternative kwa sasa......nachohitaji mganga wa kunisaidia kupata kazi na kufungua milango ya kuingia kwenye biashara.

Waliowai kupata kazi au deals za kimaisha baada ya kwenda kwa mganga, naombeni mnisaidie ushauri nini cha kufanya na nini cha kuepuka kufanya kupitia ulimwengu huu.

Pia wapi nitampata mtaalam sahihi wa kunisaidia asiwe mbabaishaji.

Astaghafilullah
 
Jaribu hii ikusaidie kuondoa umasikini.
Njia rahisi ya kuondokana na umasikini kwa mtu asiye na kipato.
Ardhi still bado ndio mtaji rahisi wa kutokea kimaisha.
Nje ya mji mapori tele yamejaa hata bure au kukodi unaweza pata safisha angalau si chini ya heka 10,panda mazao yasiyo na changamoto mfano kunde, alizeti, mtama, nk.
Chukua zao moja hili ni uhakika.
Baada ya kusafisha heka 10 au zaidi panda mmea wa nyonyo castro oil huu unavuna baada ya miezi 3 na utaendelea kuvuna kwa mda wa miaka 2.
Heka moja ya nyonyo utapata gunia 15 ukizikamua utapata lita 500 za mafuta, so heka 10 ni lita elf 5.
Jifunze kutengeneza sabuni za mche za mawingu
Lita moja ya mafuta utapata miche 2 mara lita elf 5 utapata miche elf 10.
Uza mche kwa sh 1500 mara elf 10 utapata milioni 15.
Jinsi ya kutengeneza mashine ya kukamua mbegu za mafuta tafuta bomba inchi nne tafuta Nondo mm 12 ikunje mfano wa spring ingiza ndani ya bomba mbele ya bomba ziba acha tundu dogo.Toboa toboa Bomba vitundu vidogo Ili mafuta yamwagike chini, weka mshikio wa kunyongea Ili ukamue mafuta.
Ukipata pesa kodi nyumba nenda viwandani kafunge bidhaa ambazo ni daily use kisha jaza kwenye nyumba uliyokodi kisha uwe tengeneza network na wauzaji wa dogo uwe unawasambazia bidhaa wanazoishiwa.
Kwa kufanya hivi ndani ya mwaka utakua mbali sana utaoa, utajenga, nk.
Kirahisi hivyo basi sawa..
 
Back
Top Bottom