Naomba ushauri wenu, nataka kwenda kwa mganga

Naomba ushauri wenu, nataka kwenda kwa mganga

Kwanza kama una nia ya kwenda kwa mganga kuwa makini na matapeli.
Mganga yoyote asikuambie umtie fedha kwanza ndo afanye huduma.
Jambo la pili ungesema uko mkoa ghn ili uelekezwe kwa mtaalamu wa karibu.
Nipo Dar es Salaam kiongozi
 
Kama ni kuomba na kufunga hilo ni rahisi hakuna mtu anaeshindwa kufunga na kuomba, Je ni sadaka gani unaitoa kwa Muumba wako, Ni tabia gani mbaya unazozificha ukafikiri kisiri siri kwamba Mungu hakuoni? Anza kufuatilia taarifa za maisha yako hatua kwa hatua, utaja gundua mahali baraka zako zinapotokomea.
Mimi ni mtu wa ibada nimekulia maisha hayo pia sina mambo mengi kwenye maisha nna vitu vichache nnavyo concentrate navyo.
Kama kuna dhambi inayosababisha haya labda ya kuzini ila sina baya la hivyo na hata wakati nna kipato mimi ni mtu wa kujitoa sana kwa wengine.
 
Pole mkuu ila jua Tu mtaa ndio ulivyo, nishaajiriwa na nikaacha kazi, nikaajiriwa tena na nikaacha na katika time zote sikuwahi kuona mambo ni rahisi kabisaaa.

Kama unaamini huko utapokwenda kutakupa wepesi kwa kuanzisha maagano na waganga, sisi ni nani tukupinge
Mkuu naomba connection kama hutojali
 
Soma kwanza avatar yako ndo uamue, lakin ni maisha tu , tafuta kazi za kutumia nguvu huwez kosa yaan utafute kazi kama ya kujenga , kupiga tofari utawaza kwa mganga
 
Pia wapi nitampata mtaalam sahihi wa kunisaidia asiwe mbabaishaji.

Nakuhakikisha...

M'baya wako wa kwanza ambaye hutakuja kumsahau hadi unaingia kaburini ni huyo atakayekuonyesha utakapompata huyo Mganga...

Hakuna mtu aliwahi kwenda kwa mganga mwenyewe,, lazima kuna mtu alimpeleka,,, na hao watu ndio madalali wa hao waganga..

Chunga sana,,,utapoteza hata hicho kidogo ulicho nacho...

Cc: Mshana Jr
 
Kwa mganga panahitaji pesa hakuna mganga atakutibia Bure,

wapo wa bure lakini kuwapata nauli itakatka pesa nzuri tu mpk kumfikia

Siwajui waganga mkuu,naongelea "hear say" so kama unauwezo wakulipa Mganga

akutibie kwann hiyo hela usijiongeze ukafanya biashara asee? Sikia nikwambie ndugu

Hata huko kwa waganga ni pagumu vile vile,malalamiko yako yameegemea zaidi ktk kupata

uhakika wa kesho,kula nk,kwann mkuu usijiajiri? kwann usifanye vibarua? mbona zipo kazi

vibarua vya elfu kumi,saba,tan,nk kwann usiende ukafanye? kote huko umekosa kazi kweli?

Au ku make ni shida kwako? siamini kama umekosa hata vbarua asee siamini mkuu,

Kuna biashara za mtaji ya 50k nyingi kuna za 100k nyingi,Kama upo Dar nina weza kuwa mganga wako

hatuto onana ila naweza kukupa kazi kwa mwezi 1 tu upate mtaji uanze Biashara,Ntakupa kazi ya mshahara wa 100,000 Naamini inakutosha kuanza biashara.

nataka Nikupe kazi ya kupata MTAJI mkuu,kwanini unakimbilia kwa waganga mkuu,unaona faida gani kujazwa chale mwilini mwako?

Hamna kitu inanikata stimu kama nikiona alama za chale mwilini mwa mtu,mkuu hvyo vialama vitajaa mwili wako wote,na hutopata la maana zaidi ya kuwekwa alama za kishenzi.

Kama kweli una nia ya kujiajiri karibu PM nikupe kazi ya kupata Mtaji kwa mwezi m1 tu,kula juu yangu,malazi juu yangu mwisho wa mwezi ntakupa 100k. (kama upo dar tu)

Kama haupo Dar,bado nakushauri kama ndugu yako,Kwa waganga unaenda yaongeza matatizo Amini nakuhakikishia. Heri utafute nauli Kama upo mkoni Uje Dar nikusaidie kwa namna nitakayo ona yafaa.

Shida yako ipo kwenye MWANZO tu,natamani kukusaidia kuanza huko kwngine ntakuacha ujiongeze,mKuu nipo Hapa Karibu uwe huru niambia matamanio yako ila kwa MGANGA hapana,sikusikilizi wala sikushauri.
 
Nipo kwenye miangaiko ya maisha kwa muda wa miaka miwili sasa baada ya kupoteza kazi.

Maisha yamekuwa magumu sana nimetumia akili, maarifa na kila ujanja lakini hali inazidi kuwa mbaya.

Kila kitu sasa nimekuwa nakipata kwa shida iwe kula iwe mahitaji yoyote ya kila siku.

Mimi ni mkiristo na nimekuwa nikimuomba Mungu kila siku anitoe kwenye hii hali lakini imefika sasa naona giza mbele yangu yani nimekuwa wa kulala bila kujua kesho nikiamka nitapata wapi hela ya kula japo milo miwili ya siku.

Kwa muda mrefu watu kadhaa wamekuwa wakishauri niende kwa mganga wa kienyeji naweza kupata msaada uko. Mimi ni mgeni eneo ilo so nimekuwa nnasita pia kuna hofu fulani nnayo maana ni ulimwengu ambao uwa nausikia tu na kuna story za kuogopesha.

Ila nimekata shauri niende tu maana sina alternative kwa sasa......nachohitaji mganga wa kunisaidia kupata kazi na kufungua milango ya kuingia kwenye biashara.

Waliowai kupata kazi au deals za kimaisha baada ya kwenda kwa mganga, naombeni mnisaidie ushauri nini cha kufanya na nini cha kuepuka kufanya kupitia ulimwengu huu.

Pia wapi nitampata mtaalam sahihi wa kunisaidia asiwe mbabaishaji.
Umejiandaa kudanganywa?
 
Namba za mganga hizo mwenzio nimetumiwa leo [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Screenshot_20220414-215231.jpg
 
Kama ni kuomba na kufunga hilo ni rahisi hakuna mtu anaeshindwa kufunga na kuomba, Je ni sadaka gani unaitoa kwa Muumba wako, Ni tabia gani mbaya unazozificha ukafikiri kisiri siri kwamba Mungu hakuoni? Anza kufuatilia taarifa za maisha yako hatua kwa hatua, utaja gundua mahali baraka zako zinapotokomea.
Je, wote watoao sadaka, wenye tabia mbaya siku zote mambo yao uwa yamenyooka tu? Muumini akipitia changamoto kubwa za maisha utasikia waumini wengine wakisema ili dhahabu iwe safi lazima ipitishwe kwenye moto mkali. Muumini akiishi maisha marefu itasemwa kabarikiwa na Muumba na ikitokea akafa katika umri mdogo watasema Mungu kampenda zaidi hivyo kamchukua mapema kumwepusha na mabalaa ya duniani.
 
Mganga hatoi kazi nayeye ana ganga njaa ndio maana anasubiri wateja ili apate hela ya kuishi
 
Kama Rc nenda kafanye toba ya kweli na ujue namna ya kuomba then nenda kaabudu Ekaristi Takatifu majibu utapata sahihi.
 
Nasikia kaharufu ka utapeli hapa au wenzangu mnamafua?[emoji846]
 
Naona waganga sasa hivi waanze utaratibu wa kuwapasulia wateja mayai ili mkome kwenda!
 
Kwa mganga panahitaji pesa hakuna mganga atakutibia Bure,

wapo wa bure lakini kuwapata nauli itakatka pesa nzuri tu mpk kumfikia

Siwajui waganga mkuu,naongelea "hear say" so kama unauwezo wakulipa Mganga

akutibie kwann hiyo hela usijiongeze ukafanya biashara asee? Sikia nikwambie ndugu

Hata huko kwa waganga ni pagumu vile vile,malalamiko yako yameegemea zaidi ktk kupata

uhakika wa kesho,kula nk,kwann mkuu usijiajiri? kwann usifanye vibarua? mbona zipo kazi

vibarua vya elfu kumi,saba,tan,nk kwann usiende ukafanye? kote huko umekosa kazi kweli?

Au ku make ni shida kwako? siamini kama umekosa hata vbarua asee siamini mkuu,

Kuna biashara za mtaji ya 50k nyingi kuna za 100k nyingi,Kama upo Dar nina weza kuwa mganga wako

hatuto onana ila naweza kukupa kazi kwa mwezi 1 tu upate mtaji uanze Biashara,Ntakupa kazi ya mshahara wa 100,000 Naamini inakutosha kuanza biashara.

nataka Nikupe kazi ya kupata MTAJI mkuu,kwanini unakimbilia kwa waganga mkuu,unaona faida gani kujazwa chale mwilini mwako?

Hamna kitu inanikata stimu kama nikiona alama za chale mwilini mwa mtu,mkuu hvyo vialama vitajaa mwili wako wote,na hutopata la maana zaidi ya kuwekwa alama za kishenzi.

Kama kweli una nia ya kujiajiri karibu PM nikupe kazi ya kupata Mtaji kwa mwezi m1 tu,kula juu yangu,malazi juu yangu mwisho wa mwezi ntakupa 100k. (kama upo dar tu)

Kama haupo Dar,bado nakushauri kama ndugu yako,Kwa waganga unaenda yaongeza matatizo Amini nakuhakikishia. Heri utafute nauli Kama upo mkoni Uje Dar nikusaidie kwa namna nitakayo ona yafaa.

Shida yako ipo kwenye MWANZO tu,natamani kukusaidia kuanza huko kwngine ntakuacha ujiongeze,mKuu nipo Hapa Karibu uwe huru niambia matamanio yako ila kwa MGANGA hapana,sikusikilizi wala sikushauri.
Sawa mkuu nitakuPM
 
Mungu wako na huyo Mganga, nani anaweza kukupa kazi?... But kumbuka Imani ya mtu hujaribiwa na unapaswa kuishinda.. Imani yako I wapi? Rudi kasome kitabu cha Ayubu..
 
Back
Top Bottom