Habari wana jamii wote,ni mara yangu ya kwanza kuingia huku kwenye forum hii
Naomba sana mnipe ushauri wenu kwa haya nitakayoyaeleza hapa
Mimi nimeolewa nina miaka 13 katika ndoa, nina mtoto mmoja wa kiume mwenye miaka 12, mume wangu ana mtoto wa kike mwenye miaka 10 aliezaa na mwanamke mwingine.
tatizo langu ni kuwa miaka mitatu iliyopita niligundua kuwa nimeathirika na sasa natumia dawa za kupunguza makali(ARV)
Nilishindwa kumweleza mume wangu kuhusu hali yangu kwa kuwa kila nilipomshauri kuhusu kupima afya alikuwa hataki akidai kuwa siku akigundua kuwa ameathirika atakufa. Ila mimi nilipogundua kuwa nimeathirika nikawa sikubali kufanya mapenzi bila kutumia kinga, ingawa wakati mwingine alikuwa analazimisha lakini sikuwa tayari.
Hivi karibuni akanieleza kuwa amegundua kuhusu hali yangu baada ya kuona kadi yangu ya clinic, na yeye ameenda kupima na amesema yeye hajaathirika, hivyo kasema tuendelee kuishi bila watu kujua.
Mimi nikampa option kuwa kwa kuwa yeye ni mzima basi nisimbane kama atahitaji awe na mwenza mwingine basi tunaweza kuachana na yeye akaanza maisha mapya, lakini kasema kuwa haiwezekani tuachane kwa kuwa tumeishi muda mrefu na tumesaidiana mengi.
sasa naomba ushauri wenu je hili linawezekana? Au mna ushauri gani?
Ahasanteni
pole sana kwa yaliyokukuta dada,
hiyo ni sehemu ya maisha tu, ningependa kukwambia kuwa kwa maisha haya ya sasa,
watu wengi tu kwenye ndoa wanaishi katika hali hiyo,
unakuta baba au mama mmoja wapo ni mgonjwa,
na maisha yanasonga kama kawaida,
usihofu, huyo ni mumeo na kumbuka kuwa
utaishi nae katika raha, shida, magonjwa na kila aina ya mapito!
Ni vema kwakuwa yeye hata baada ya kugundua kuwa wewe umeathirika,
basi amependa muendelee pamoja,
"what husband"
Tena ukithubutu kumwacha na kwenda kuishi kivyako basi na mungu anaweza akakupa adhabu mbaya sana,
wewe ni mtu unaehitaji faraj, upendo na ukaribu kutoka kwa mumeo!
hebu tulia muendelee kuwakuza hao watoto!
Mungu awape nguvu!