Naomba watanzania tumsaidie Ray C tumchangie

Kuna wagonjwa kibao wanahitaji mchango wako wa hali na mali ili wapelekwe nje ya nchi kutibiwa, umeshawachangia wangapi, mpaka utake kumchangia mtu alojipachika ugonjwa?
Kamchangie Beatrice, yule dada wa kisarawe, mwenye mguu mkubwa hata kunyanyua hawezi, anahitaji Usd 27,000 ili akatibiwe india, mchango wako mdogo will make a big difference.
 
JF inabidi muwe waelewa. Huyu Ray C kwao wanajiweza sana tu kuweza kumuhudumia, kinachofanyika hapa ni mashauzi classic yakujifanya na mimi au na sisi tulimchangiaga Ray C. Vituo vile havina gharama kubwa yeyote, tena vipo radhi kukusaidia free endapo unataka kuacha Unga. Wacheni ujinga wakusema watu hawana huruma. Hizi ni Shobomshoboko ambazo wa tz haswa maredio ya kise nge yanaleta, haswa pale m2 anapoumwa. Wao hawaangalii hata kama huyo m2 kwao wanajiweza wao wanatafuta sifa. Ray c anahitaji ushauri kwanza wa kuacha unga, then aanze kupewa ARVs.
 
Mateja wenzake wapo weng sn so pitisha bakul huko co hapa jf au na hapa mateja wapo???Watanzania weng sn wanamagonjwa from god co hayo ya kjitakia,mwache avune alichopanda
 
Kwani gharama ya kuacha madawa ya kulevya ni sh.ngapi zaidi ya kujicommit sober houses na kula vizuri. Mbona Langa ameacha madawa bila kuchangiwa.Isitoshe ray c anandugu wenye uwezo.Kama kuna gharama fulani hawawezi kushindwa.Nafkiri kuna watu wanatafuta sifa za kimjini. watz tumedhalilishwa kwa hili ss sio watu wa kuchangia ujinga.Kama unataka kusaidia mateja nenda kawasaidie kiujumla wao kwenye vituo vyao na sio kufata umaarufu wa mtu
 

Nakubaliana na hitimisho lako na kwa msingi huo sasa, mimi na wewe tunaongea lugha moja.

Ila tunatofautiana pale ambapo wewe unahisi kama vile kuwananga akina Ray C, eti kwa kuwa wamepata shida ni haki yatu. Na kwamba wanastahili adhabu ya namna hiyo!!

Nadhani kama wewe ni mfuatiliaji wa mijadala ya MMU, utakuwa umekutana na uzi uliozungumzia wanawake kuwapokea na kuwauguza waume zao ambao walitelekeza wakati mambo yalipokuwa mazuri.....Naamini mifano iliyotolea inafaa hata kwenye hii case, kwani hata siku moja, hatuwezi kuwa sahihi na hatuna haki ya tuwakebehi na kuwatukana watu wenye matatizo kwa kuwa huko nyuma walifanya madudu!!

Tukifanya hayo, hata sisi hatutakuwa tofauti nao.....kwani bado kuna watu wanatuona na sisi tunaringa au tunafanya mambo ya ajabu pia!

Babu DC!!
 

Ndugu yangu ukisoma heading vizuri, na hata maelezo ya mleta mada, utakuta tayari umetoa mchango mkubwa sana isipokuwa pale ulipopotoka na kumwaga mitusi....

Hivi kuna mahali mleta mada kasema lazima tutoe pesa???

Babu DC!!
 
Jaman tuseme huyu Ray C hana marafiki jaman wenye uwezo wa kchangia mpaka aombe watanzania, mtu aliekua maarufu namna ile jaman, wasanii wenzake alofanya nao kolabo, clouds fm mameneja na maproducer wa mhzik wake wote hao wameshinwa kumchangiatu wao, kuna watu wengine ambao hawana hata mtu wanafahiana nae mwenye uwezo hao ndio wanahitaj msaada wa watanzania
 
Nadhani wanaowaza kumchangia mtovu wa akili na maadili huyu wakapimwe!hivi mnawafahamu watanzania wenzenu wenye matatizo? isitoshe familia ya wasanii ni kubwa wanaweza kuchangiana sie tushawachangia zamani kwa kununua kazi zao!
 
Hivi wale waliokuwa wanapata huduma za kiuno bila mfupa kwenye sita kwa sita wamekwenda wapi?
 

Anao Marafiki kuna Barnaba Boy, Mwisho Mwampamba, Rodzy Eyes hata Na yule Mzenji HT huyu Ray c Nadhani atakuwa na Uhusiano na Yle Mkuu wa koa sijui au Wilaya Mama Betty Chalamila ak.a Betty Mkwasa anaweza kumsaidia kwa njia ya kiserikali kwenye vitupo vya waathirika wa Madawa ... nimesikia kuna mtu ame comment Ray C atumie RV mmmh! kwani ana Ngoma?
 
Betty Chalamila Mkwasa na Rehema Chalamila Ray C siyo ndugu, udugu wao ni wa Kiutanzania zaidi lakini siyo wadamu kutokana na majina yao, ingawaje wote wanatokea Kumnofu.
 
ray c ana ngoma na ARV za bongo ni feki sijui tuchange ili iweje? uume ni lethal injection ikimbieni zinaa kina dada,
 

kikwete
 
Kama mna hela za kuchezea namna hiyo na mimi naombeni mnichangie nikatishe mbege pale Moshi. Kipindi hiki cha mwisho wa mwaka biashara ya mbege pale Moshi huwa inatoka sana.
 
Dah! Nimesikitika sana, namshukuru mleta uzi na wana JF wote kwa michango yenu kimawazo. Mm nashauri kitu, kwamba hii dunia ipo, tuliikuta na tutaiacha. Unapofanikiwa kwa hatua 1 usidhani kwenda haraka mara 10 ya vile ulivyo ulivyopata 1 basi utafanikiwa mara kumi yake, na hp ndio wengi huumia. Au unapokimbia basi hakikisha huzidi uwezo wa miguu yako kuchanganya au lah utadondoka. Na pili usisahau ulikotoka!
Hiki ndicho alichokosea ndg yetu Ray C, omba na uwe na hekima sana upoona kuna mafanikio na usiwaache watu wako uliokuwa nao coz hawa huwa regulator pale unapokosea, Kwasasa Mungu mwenyewe atende.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…