Naombeni kazi ndugu zangu nipate pesa ya kulipa ada

Gemini-AI

Senior Member
Joined
Oct 19, 2023
Posts
114
Reaction score
501
Ndugu zangu, Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23 na elimu ya kidato cha sita. Nilichaguliwa kusoma chuo cha IFM kampasi ya Dar es Salaam. Mwaka jana nilisitisha masomo baada ya kupungukiwa na ada. Ninatafuta kazi yoyote na ninaishi Kigamboni, Dar es Salaam.

Niko tayari kufanya kazi kwa bidii na kujifunza mambo mapya. Nina uwezo mzuri wa mawasiliano na ninaweza kufanya kazi katika mazingira mbalimbali.

Ikiwa una nafasi ya kazi au unamjua mtu anayeweza kunisaidia, tafadhali wasiliana nami nipate japo ada ya chuo ili mwezi wa kumi na moja na mimi niendelee na masomo kwa maana nilisitisha tangu mwaka jana semester ya kwanza (Mwezi wa tatu)
 
Kwema ndugu zangu?

Mimi ni kijana miaka 22 nina elimu ya kidato cha sita. Nilikuwa nasoma chuo IFM mwaka wa pili ada imekosekana hivyo nimeshindwa kuendelea na masomo.

Nilikuwa naomba mnisaidie connection yoyote ya kazi ili niweze kupata ada niendelee na masomo. Napatikana kigamboni.

Natanguliza shukurani
 
Hongera kwa kufunguka, ada itapatikana, chuo utarudi na utamaliza masomo yako. Weka wazi unasomea faculty au course gani na gharama ya tuition fee na nyinginezo unazopaswa ulipe ili ukamalizie masomo yako. Amini utamaliza.
Asante sana mkuu. Nasoma course ya banking and finance kwa ngazi ya degree. Faculty ni insurance and banking. Mpaka sasa ili niweze kuendelea na masomo inanipasa nilipie milioni moja na laki tatu na sitini kwa mchanganuo ufuatao;

Semester ya kwanza nilibaki na deni la 610000 na semester ya pili nilibaki nadaiwa laki saba na hamsini.
 
Weka namba ya simu mwenye chochote akuchangie au connection iwe rahisi kupata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…