Naombeni mawazo yenu kuhusu hii ramani ya nyumba yangu

Wsitting room mbona dirisha upande mmoja tuu?
Masterbedroom ukiwa unaendelea na mizagamuano upande wa pili wanakusikia. Choo cha master ndio ungekipachika katikati ya hivyo vyumba viwili.
Masterbedroom inapaswa kuwa na madirisha pande mbili
 
Point zako 6 za nguvu nimezichukua mkuu, nazifanyia kazi
 
Sawa mkuu, Acha niliangalie hilo
 
Mkuu, hebu fafanua ili kunipa mwangaza...

Unasema ramani haijazingatia matumizi makubwa ya ardhi...kivipi?
 
Point zako 6 za nguvu nimezichukua mkuu, nazifanyia kazi
Karibu sana.

Kama ungependa, acha pia nikuonyeshe post niliyoanzisha hivi karibuni ya jinsi ninavyodesign . Kuna vitu utaweza kupata hapa pia.

 
Mkuu, hebu fafanua ili kunipa mwangaza...

Unasema ramani haijazingatia matumizi makubwa ya ardhi...kivipi?
Kiwanja chako ni SqM ngapi..? (Upana mita ngapi na urefu mita ngapi..?)
Raman yako upana ni mkubwa itabana nafasi kama kiwanja chako chini ya sqm 600. Jitahidi nyumba iache mita 3.5 au 4 kulia na kushoto.
 
Mkuu asante kwa inputs:

1. Foyer/entryway ni vitu ambavyo wabongo hatuwekagi/hatuvijuagi... ila huko mambele more than 90% ya nyumba zao huwa na entryway.(nimekuwa inspired kutoka kwao). Entryway ina functionality zake, ambazo naona kwangu ni muhimu.

Ili kuongeza mwanga, nafikiria kuondoa huo ukuta unaoelekea dining ili kuwe na space na mwanga.

2. Kuhusu kuweka meza ya ofisi sebuleni, kwa mimi it's a turn-off. Kuchanganya makochi na meza ya ofisi naona haijanikalia vizuri kwa usmart ninaotaka kuuweka kwenye hiyo nyumba.
Mimi napenda vitu viwe EXTRA smart. Napenda sebule iwe sebule, minimal and carefully designed.

Ushauri wako wa kule juu wa kuweka master mbele ya nyumba nimeuchukua kwa 100% na nitaufanyia kazi.

Nashukuru sana mkuu
 
Nahitaji pia maoni wakuu, kwa ramani hii
Brother hii raman yako utaichukia nyumba ukiimaliza, wageni ili waingie ndani Veranda/Kibalaza kipo Master Bedroom sio vzuri haipendez... Ihamishe ikae upande wa dining...
Mwisho wa siku uzuri au ubaya wa kitu upo machoni pa mtu, kwa maana kilamtu ana namn yake ya kupenda au kuchukia kitu... All in all raman ya nyumba unapaswa kuzingatia vitu vitatu 1. Privacy ya M/bedroom 2. Ukubwa wa raman una determine gharama za ujenzi 3. Ukubwa wa eneo lako
 
Nahitaji pia maoni wakuu, kwa ramani hii
Kuna mjumbe kashasema Baraza mbele ya master bedroom siyo poa. Bora hata iwe upande wa dining.
Toilets za 1.5*1.6 siyo mbaya, ila zipangiliwe vizuri. Mwambie mchoraji akuwekee wc, shower tray na basin na ikibidi akupe na vipimo vyake.
Jiko dogo ila kuna milango/njia tatu. Sioni likiwa practical. Mchoraji akuwekee design ya jiko- sink litakaa wapi, fridge, cooker nk. Kumbuka unahitaji prep area pia Kwa kuandaa vya kupika na pakuepulia vilivyoiva.

Vyoo na jiko huwa vinasahaulika kupangwa na wachoraji wengi. Usipokee plan isiyoonyesha mpangilio wa ndani wa vitu hivi. Bedrooms pia ni muhimu ujue kitanda na kabati au meza vitakaaje.

Mlango wa master bedroom unaweza kurudishwa nyuma kwenye hicho kicorridor chake.
 
Sawa Engineer
 
Sawa Mkuu
 
Ongeza room moja ua hyo ofisi isiyo na dirisha
Nashukuru mkuu kwa wazo.
Room 4 itakuwa too much kwa familia yangu ndogo ya watoto wadogo...
Ofisi ndogo ya nyumbani ni muhimu kwangu(ina dirisha ila kwenye ramani amesahau kuliweka)
 
Nahitaji pia maoni wakuu, kwa ramani hii

Kuna vitu viwili havijakaa sawa...

1. Kutoka jikoni kwenda vyumbani inalazimu mtu apite kwanza dinning room, then sitting room kisha aende vyumbani...

2. Kingine, position ya master naona kama ajabu kukaa mbele kiasi cha kupakana na front porch/front verandah. Mfano ikitokea unafanya mambo yetu yale nyakati za mchana hautakuwa huru sana...
 
Mkuu hao watoto SI wanakua, kinatosha kama utaweka kitandaa pekee bila kabati
Sawa mkuu... Nitaongeza ukubwa wa vyumba. Kiwanja sio kikubwa sana, ni 473 sqm... so nafikiri maybe nitaongeza iwe 3.2 * 3.5 ( kutoka hiyo 3*3). Nini maoni yako juu ya hii size mpya?
 
Wsitting room mbona dirisha upande mmoja tuu?
Masterbedroom ukiwa unaendelea na mizagamuano upande wa pili wanakusikia. Choo cha master ndio ungekipachika katikati ya hivyo vyumba viwili.
Masterbedroom inapaswa kuwa na madirisha pande mbili
Mzee wa mizagamuo mzabzab ... Asante kwa mawazo mazuri.

Nimeweka dirisha moja Sebuleni kwa sababu huwa napenda kwenye sitting room sehemu ya "Entertainment area" (ie upande wa Tv) usiwe na dirisha wala mlango, uwe plain na itawaliwe na TV, sound system, game etc peke yake. Unaonaje wazo hili kwa hii ramani?

Wazo la dirisha mbili Master bedroom nimelichukua, na nitarekebisha hapo.
 
Asante mkuu, naipitia hiyo post yako... naona iko njema sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…