Naombeni mawazo yenu kuhusu hii ramani ya nyumba yangu

Sawa nimekupata basi kwenye huo huo ukuta mwishoni karibu na upande wa kuta ya store weka dirisha mkuu kusaidia ventilation.
Alafu pia hapo kwenye entrance kati ya foyer na sitting room weka french doors. Hii ni kwa sababu ya ufaniai wa ac kama utaweka kwenye siting room.
 
Chumba cha metre 3×3 ni standard mkuu
 
Kuna hii kanuni ya kujifunza lay out ya kabati la nguo na kitanda vinapaswa kupangiliwaje ndani ya chumba ukizingatia dirisha/madirisha ya chumba. Hapo utaweza kujua ni wapi pa kuweka kiti na meza ya kusomea
 
1. hiyo laundry kuwa ndani ya jiko haijakaa vizuri
2. corridor ilivyokaa lazima itakuwa na giza itakulazim kuwasha taa hata mchana.
3. master bedroom umeificha nyuma mno ni vyema ukaona wanaoingia na kutoka ndani kwako
 
Sawa mkuu... Nitaongeza ukubwa wa vyumba. Kiwanja sio kikubwa sana, ni 473 sqm... so nafikiri maybe nitaongeza iwe 3.2 * 3.5 ( kutoka hiyo 3*3). Nini maoni yako juu ya hii size mpy

Sawa mkuu... Nitaongeza ukubwa wa vyumba. Kiwanja sio kikubwa sana, ni 473 sqm... so nafikiri maybe nitaongeza iwe 3.2 * 3.5 ( kutoka hiyo 3*3). Nini maoni yako juu ya hii size mpya?
Hiyo based on size ya kiwanja inatosha.
 
3. Public bathroom ni nyembamba sana na siyo sawa sana kuwa na shower katikati ya sink na choo, yaani mtu anavuka maji kufika chooni. Ukienda haja baada ya mtu aliyetoka kuoga na umevaa soksi....
💯🤝 nakuunga mkono hapo kwenye arragement ya shower na toilet kwenye choo cha public sio sahihi

Kikawaida ilitakiwa iwe kama alivyofanya kwenye master.

Plumbers (mafundi bomba) wengi bongo huwa wanafail hapa utakuta ukiingia kwenye choo ukifungua mlango unaanza na sink, shower halafu choo

Lakini layout inayotakiwa ni sink, choo then shower
 
Standard kwenye ordinary sio moden. Vinyumba vya nation housing enzi hizo. Huwezi hata kuweka kabati, kitanda, meza na kiti chumba kimejaa. Nyumba za kishamba kabisa. We ukiwa na eneo la kutosha kwanini ung'ang'ane na tuchumba tudogo.
Au kiwanja cha 20x20 400sqm cha kazi gani? Ndio maana nilikubaliana na Mabula kwenye kupiga marufuku huto tu viwanja... anyway kila mtu na standard zake pambana mwanaume. Ila binafsi out of 1200sqm and above sihangaiki napo.
Chumba cha metre 3×3 ni standard mkuu
 
4. Kama utaratibu uko vizuri, laundry na store vichanganye viwe chumba kimoja kiwe scullery ama Butler's pantry with laundry.
Modern laundry room inahitaji kuwa na iron board/table, sink, kabati la kuwekea nguo zilizonyooshwa temporarily na vifaa vingine na hangers za kutundikia nguo. Ili kuzuia purukushani za store zetu za kibongo ni bora kutenganisha






 
Hiyo corridor maeneo ya vyumbani itakuwa na giza sana...
 
Kweli kabisa mkuu. Ndiyo maana nikasema kama utaratibu uko vizuri aunganishe. Wazo langu lilikuwa Kwa combo ya namna hii zaidi...


Ila kama ni ngumu kumaintain ni Bora kutenganisha kama ulivyoshauri.

 
Hakikisha sebule ina madirisha si chini ya mawili lli kuweza kutembeza natural air and light kwa uhakika. Ogopa nyumba sebuleni inawashwa taa saa 7 mchana.
 
..Kwa nini master bedroom inakaa uwani? Yaani watoto wakae mbele wewe mwenye nyumba ujifiche uwani! Fanya uwezavyo chumba chako kikae mbele uwe na uwezo wa kuona chochote kinachotokea eneo la mbele la nyumba ikiwezekana uone na gate kubwa la mbele.
Wapita njia watakuwa wanasikia akiwa anapiga miti
 
Kuongeza ukubwa wa chochote ni kuongeza maradufu gharama ya ujenzi. Hata kama ungekuwa na kiwanja cha 400sqm kama budget yako haitoshi huwezi kufanya kitu. Ungeuliza kwanza kama mhusika ana "unlimites budget" ndio utoe ushauri wako huo.

Jamaa yangu tulianza nae ujenzi mwaka 2016 yeye akajenga mjengo mkubwa balaa (hiyo veranda mzunguko wake pekee ni hatari na inatakiwa kumiminwa) mimi nikajenga simple/standard family house, mwaka 2017 nikahamia kwangu. Yeye mpaka leo lile jumba lake halijaisha (tunakaribia kuliita gofu/pagale) na bado amepanga mpaka leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…