Jamani....
Naombeni mbinu za kuwa mchumi,,,,,nisitumie pesa hivyo,Hali hii inanitesa Sana.
Natafuta pesa kwa taabu mnoo....yaani kuipata Ile 20,000 NI kazi Sana lakini nikiwa na pesa matumizi yangu ni mabya mnoo
Yaani mwezi December Hadi February nafikir nimetumia zaidi ya 1M
Juzi Jana na leo nishatumia 170,000,
Sina kazi Wala kutegea uchumi chochote, Ila na haso huku na huko kutafuta
Alafu nikiombwa pesa kusema Sina siwezi,Kama ninayo lazima nitatoa tuuuu [emoji22][emoji22]
Tatizo linanitesa Sana, kwasababu nitakapokwama Sina MTU YEYOTE wa kunipatia hata 5000 nikiwawatizama ndugu na marafiki wanaonizunguka sioni wa kunisaidia nikikwama.
Nisaidieni niwe bahili, na mchumi niache matumizi mabaya ya pesa ninayoitafuta kwa taabu na nguvu nyingi.........
Nimewaona watu wakishinda na njaa huku Wana pesa mfukoni ....yaani nataka kuwa bahili Kama hivyo