Naombeni mbinu za kuushinda umaskini

Naombeni mbinu za kuushinda umaskini

Kama ni Mungu nimemwomba sana lakini wapi? Sometimes mpaka nawaza bora nisingezaliwa. Maana kama huna hela huna msaada.
Usifikie kujilaumu kiasi hicho. Katika kutatua tatizo, hatua ya kwanza ni kutambua tatizo, baada ya hapo ni kutafuta njia sahihi na mbinu sahihi za kupambana nalo. Umekwishagundua tatizo, sasa upo kwenye hatua ya pili.

Ili tukupatie ushauri, sahihi, yabidi utupatie mwangaza zaidi juu ya yafuatayo;

1) Una umri gani?

2) Umekuwa unajishughulisha na nini?

3) Una elimu na ujuzi wowote?

5) Kama huna ujuzi, na labda elimu ya kawaida (primary - secondaru), una uwezo wa kufanya kazi ngumu za kujituma kama utalipwa vizuri?

6) Una mke na watoto?
 
Umaskini ni changamoto kubwa inayowakabili watu wengi duniani. Hapa kuna mbinu kadhaa za kuushinda umaskini:

1. Elimu:
- Kujifunza:
Kuongeza maarifa na ujuzi kupitia elimu rasmi na isiyo rasmi.
- Kufikia elimu bora:
Kuwa na fursa ya elimu bora kwa watoto ili kuwapa uwezo wa kujitegemea.

2. Kujiajiri:
- Kuanzisha biashara:
Watu wanaweza kuanzisha biashara ndogo ndogo zinazoweza kuwasaidia kujipatia kipato.
- Ujuzi wa ufundi:
Kujifunza ujuzi kama vile ushonaji, ujenzi, au upishi.

3. Mikopo na Fedha:
- Mikopo ya biashara:
Kutafuta mikopo kutoka taasisi za kifedha kwa ajili ya kuanzisha au kukuza biashara.
- Akiba,;
Kuwa na utamaduni wa kuweka akiba, hata kama ni kidogo kidogo.

4. Kilimo:
- Kilimo bora:
Kutumia mbinu za kisasa za kilimo ili kuongeza uzalishaji na kufikia masoko.
- Kujifunza masoko:
Kujua jinsi ya kuuza mazao na kupata bei nzuri.

5.Usawa wa Kijinsia:
- Kuwapa wanawake nafasi:
Kukuza ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi na uongozi.
- Elimu ya jinsia:
Kukuza elimu na uelewa kuhusu usawa wa kijinsia.

6. Mikakati ya Kijamii:
- Mikakati ya jamii:
Kuunda vikundi vya ushirikiano ambavyo vinaweza kusaidia kuboresha maisha ya wanajamii.
- Msaada wa kijamii:
Kuanzisha miradi ya kusaidia wenye uhitaji.

7. Afya na Lishe:
- Huduma za afya:
Kuweka mikakati ya kuhakikisha watu wanapata huduma za afya bora.
- Lishe bora;
Kutoa elimu kuhusu lishe ili kuhakikisha watu wanapata chakula cha kutosha na chenye virutubisho.

8. Teknolojia:
- Teknolojia ya habari:
Kutumia teknolojia kuimarisha biashara na kujifunza zaidi.
- Mafunzo ya kidijitali:
Kutoa mafunzo kuhusu matumizi ya teknolojia katika maisha ya kila siku.

9. Ushirikiano na Serikali:
- Sera za maendeleo:
Kushirikiana na serikali katika kutunga sera zinazosaidia kupunguza umaskini.
- Programu za kijamii:
Kusaidia katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya jamii.

Kupitia mbinu hizi, watu wanaweza kujenga maisha bora na kupunguza umaskini katika jamii zao.
Sawa Mkuu. Litakalowezekana litafanyika🙏🙏🙏
 
20240418_123833.jpg
 
Usifikie kujilaumu kiasi hicho. Katika kutatua tatizo, hatua ya kwanza ni kutambua tatizo, baada ya hapo ni kutafuta njia sahihi na mbinu sahihi za kupambana nalo. Umekwishagundua tatizo, sasa upo kwenye hatua ya pili.

Ili tukupatie ushauri, sahihi, yabidi utupatie mwangaza zaidi juu ya yafuatayo;

1) Una umri gani?

2) Umekuwa unajishughulisha na nini?

3) Una elimu na ujuzi wowote?

5) Kama huna ujuzi, na labda elimu ya kawaida (primary - secondaru), una uwezo wa kufanya kazi ngumu za kujituma kama utalipwa vizuri?

6) Una mke na watoto?
1)23yrs
2)Mi sichagui kazi Ndugu yangu. Kazi yoyote nafanya. Kwahiyo sina kazi maalum.
3) Sikubahatika kumaliza elimu ya chuo (DIPLOMA IN PHARMACEUTICAL SCIENCE)
5) Kazi ngumu nafanya.
6) Sina Mke wala Watoto.
 
Angalao kwa kuanzia, unafikiria ukiweza kupata kiasi gani kwa mwezi, maisha yako yatakuwa na unafuu na ya uhakika kuliko yalivyo sasa?

Naangalia uwezekano wa kuongea na jamaa zangu ili wakupe kibarua, angalao hata ukifanya kwa miaka miwili, unaweza kuwa umejikusanyia kiasi fulani cha kwenda kuanza nacho kama mtaji, kama utakuwa umefikiria kufanya hivyo.
 
At least 400k maana kwenye harakati zangu mara nyingi napata 15k au 20k kwa siku. Kazi zikiwepo, Japo kuna mda harakati zinakuwa adimu kwa kweli.
 
Soma thread hii,

DawayaUmaskini,madeni,ukata, mifukokutoboka,uhitaji,kufilisika,hiihapa-Rabbon
 
Angalao kwa kuanzia, unafikiria ukiweza kupata kiasi gani kwa mwezi, maisha yako yatakuwa na unafuu na ya uhakika kuliko yalivyo sasa?

Naangalia uwezekano wa kuongea na jamaa zangu ili wakupe kibarua, angalao hata ukifanya kwa miaka miwili, unaweza kuwa umejikusanyia kiasi fulani cha kwenda kuanza nacho kama mtaji, kama utakuwa umefikiria kufanya hivyo.
Japo hata chochote ila kisiwe cha kuumiza sana Ndugu.
 
1. Ondoka hapo ulipo (hama mkoa)
2. Usifikirie kuhudumia kwenu (jijenge kwanza, sio kwa ubaya ila hautaukimbia huo umasikini ukijivika hayo majukumu sahivi. Kama chakula ni kidogo ni bora akala mmoja akapata nguvu tukamtuma kwenda kuleta kingi kilicho mbali)
3. Fanyakazi kwa kiasi, pata muda wakupumzika ili uweze kujitafakari na kuitafakari kazi unaifanya.
4.Acha lawama, kwa watu na mazingira

Ongeza bidii kiongozi
 
Badili cycle ya marafiki zako...hapo automatic utabadili mifumo ya utafutaji na mitizamo juu ya mafanikio....mfano,,ukiwa na rafiki wengi wenye njaa na wewe umeshiba utaona kuwa umefanikiwa,,,lakini wakiwa wengi wamekuzidi mbali,tuliza wenge wakupe code...
 
Back
Top Bottom