Sigma na Alpha ni kitu gani?
Mimi Nifahamuvyo, kuna makundi manne ya temperament:
1. Sanguine
2. Melancholy
3. Choleric
4. Phlegmatic
Sanguine na Choleric zipo kwenye kundi la EXTROVERT, Melancholy na Phlegmatic zipo kwenye kundi la INTROVERT.
Lakini ifahamike pia kuwa hakuna mtu mwenye tabia za kundi moja kwa asilimia mia moja. Tafiti zinaonesha kuwa mtu mmoja anaweza kuwa na tabia za makundi mawili au hata matatu, ila ile inayoonekana kuwa "dominant" ndiyo hutumika kumtambulisha kuwa yeye ni wa kundi fulani.
Kwa mfano, mtu mwenye uwiano wa SANGUINE 70%, CHOLERIC 20% na PHLEGMATIC 10% atatambulika kama SANGUINE. Kwa huyo mtu, Temperament ya Sanguine ndiyo imekuwa "dominant".
Kwa maelezo yako, inaonekana upo kwenye kundi la MELANCHOLY. Vigezo nilivyovitumia kufikia hiyo hitimisho ni maelezo yako binafsi, kama:
1. MWONGEAJI UNAPOKUWA NA WATU ULIOZOEANA NAO
Melancholy anafahamika kuwa ni mkimya sana, lakini anao uwezo mkubwa wa kubadilika kulingana na mazingira. Akiamua kuongea, wasiofahamu huishia kumtambua kama mtu mwongeaji sana, lakini mtu uyo huyo wakimkuta kwenye mazingira mengine, wanaweza wakashangazwa kwa jinsi alivyo mkimya.
2. NDOTO KUBWA
Ni tabia mojawapo inayowatambulisha. Mara nyingi, hawapendi kuwa katikati. Wakiweka malengo, wanaweka makubwa sana ambayo wakati mwingine hushindwa kuyafikia.
3. KUTOKUPENDA MIKUSANYIKO
Kutokana na asili ya tabia zao, endapo atahudhuria sherehe uliyomwalika, ujue ni kwa sababu tu amekuheshimu, la sivyo, asingehudhuria.
Hata kazini, yeye angefurahia kukaa kwenye ofisi ya peke yake. Ni tofauti na mwenzake - Sanguine. Sanguine kukaa peke yake ni kama mateso vile.
4. KUWAKOPESHA WATU KIRAHISI
Katika temperament zote 4, mbili ndizo zinazoongoza kwa kuwa wepesi kuguswa hisia zao. Nazo ni SANGUINE na MELANCHOLY. Lakini hasa Melancholy, ana tabia ya kuwatanguliza sana wengine. Ana tabia ya huruma sana na kujitoa "sadaka" kwa ajili ya wengine.
5. MARAFIKI WACHACHE
Kwa kawadi, Melancholy hutengeneza marafiki kwa tahadhari sana lakini pia si rahisi kuwapoteza marafiki. Yeye, msimamo wake ni kuwa bora kuwa na marafiki wachache lakini walio bora. Anazongatia ubora na si idadi.
Kutokana na kutokuwa mwepesi kumridhia mtu kama rafiki yake, pia ni nadra sana kwa yeye kumpoteza rafiki. Isitoshe, katika makundi yote 4, ndilo kundi linaloongoza kwa kuaminiwa. Ndilo kundi pia linaloongoza kwa kuwa waaminifu.
Kwa kuongezea tu, hizi ni baadhi ya tabia zingine za Melancholy:
A. Ni watu wa kufikiria sana. Kama analifikiria jambo linalogusa hisia, anaweza akfikiria mpaka akaanza kutokwa na machozi, ingawa jambo lenyewe ni la kufikirika tu.
B. Ndilo kundi linaloongoza kwa kuwa na vipaji vingi, ingawa wana changamoto ya kutokujiamini
C. Si wepesi kufanya maamuzi ingawa pia wakishaamua ni vigumu kubadili misimamo yao
D. Wako very organized. Kama ni mwanaume, kwa mfano, anaporudi tu kutoka kazini, si ajabu anaweza akaanza kuhoji sababu ya vyombo kutokupangiliwa katika mpangilio stahiki.
E. Perfectionist. Wao ni bora wachelewe kukamilisha jambo lakini walifanye katika kiwango wanachoamini kuwa ni cha ubora unaoridhisha
F. Hawapendi umaarufu. Yeye anaridhika kukaa "viti" vya nyuma, tofauti na Sanguine ambaye yeye anataka anapokuwa mahali fulani kila mtu autambue uwepo wake. Inasemekana, kama Sanguine akiwa na nusu ya uwezo wa Melancholy, angekuwa maarufu haraka sana.
G. Wakati mwingine huwaona Sanguine kama watu wasiokuwa na akili kutokana na udhaifu wa Sanguine kuongea bila kufikiria.
H. Ni wasiri sana, hivyo wanaaminika sana katika ushauri. Wana vifua vya kutunza siri za watu. Ni tofauti na Sanguine ambaye yeye akishajua mambo ya siri ya mtu, anaweza akashindwa kuvumilia na kuishia kusema kwa mtu anayemwamini akifikiri naye hataenda kuyavujisha kama yeye alivyoyavujisha.
Hizo ni baadhi tu, lakini pia, si lazima mtu awe nazo zote.
Kwa hiyo, inavyoonekana, wewe unaweza ukawa na temperament ya Melancholy.