Naombeni msaada wa mawazo mwanangu hapendi Kula

Pole sana.
Mpeleke hosp. wamchunguze kama ana shida kooni, apatiwe na dawa za minyoo.

Pia, zingatia kwenye upishi wa chakula chake (Apikiwe chakula chake), kwa kuanzia mpikie vyakula rojorojo, asile chakula kikavu (Kama ni wali, ufanye rojo) Unaweza kumuongezea tui la nazi, maziwa ama karanga.

Jitahidi pia kumkorogea uji awe anakunywa asubuhi na jioni (katika kuandaa unga wa uji zingatia nafaka za makundi mawili/matatu). Katika ukorogaji wa uji unaweza pia kuongeza tui la nazi maziwa ama karanga.

Ukishaona anaanza kula vizuri sasa ndo utaanza kuvifanya vyakula vyake kuwa milo ya kati kabla ya milo mikuu mnayokula wote kama familia.
 
Sawa asante sana
 
Daah asante mdau
 
Mtoto ana miaka mitano lakini sio miezi mitano
 
Niliachiwa watoto na mke mtafuta Hela. Watoto hawakuwa wanapenda kula Hadi ufoke au tuwape zawadi ili wale. Njia niliyotumia
1. Kwanza wapatishe njaa no bites, no juice, no kutafuna chochote
2. Wape kazi Fulani ili walichokula kiyeyuke mfano wafagie, wang'oe majani au wakimbie riadha.
3. Kisha njaa ikiwapata vizuri na wamechoka hutatumia fimbo wape vyakula kama viazi, Dona yenye mboga nzuri ya uchu, anyway kulingana na umri wao. Watakula Hadi utashangaa.
4. Ukiweza wakati wa kula waarike na rafiki zao wa jirani mmoja wawili watatu hivi aseee watakula Hadi utafirahi na watapata afya Hadi raha.
 
Sawa kaka nmekupata vilivyo asante
 
KULA nini? Nyapi au
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…