Mkuu ondoa hiyo misconception kichwani mwako eti MediaTek nj mbaya, sio kweli. MediaTek wana processor nzuri ambazo zinazidi hata baadhi ya processor kali za Snapdragon kama Qualcomm Snapdragon 8 Gen 2.
Kwa laki 5 tafuta AliExpress kule utapata "Xiaomi Redmi Note 13 Pro 5G" au "Xiaomi Poco X6". Hizo mbili ni simu moja ileile isipokuwa Redmi Note 13 Pro 5G ina kamera nzuri zaidi, ila almost everything else ni sawa ila sana sana tafuta hiyo Redmi kwa sababu itapokea 4 years major Android updates na 5 years security patches wakati hiyo Poco inapokea 3 na 4years updates respectively. Redmi Note 13 Pro 5G na Poco X6 zinatumia processor ya Qualcomm Snapdragon 7s Gen 2, 67W fast charger in box, stereo speaker, high quality 120Hz AMOLED display na vitu vingi vizuri
Kwa Tanzania options ni chache. Unaweza kutoa 450K ukanunua Redmi Note 13 4G yenye 8GB RAM 256GB ROM. Nayo ni nzuri na inakuja na Qualcomm Snapdragon 685, 108MP, underdisplay fingerprint scanner, stereo speakers, etc.
Au okoa pesa kwa 350K upate Samsung Galaxy A15 4G ambayo ina MediaTek Helio G99 na ndio simu bora zaidi kwa bei hii. Samsung Galaxy A24 kwa 350K pia sio mbaya. Kwa 450K unaweza pata Samsung Galaxy A15 4G yenye 8GB RAM.
Option ndio hizo ila acha kuchukia MediaTek. Cha msingi angalia sanasana uwezo wa processor kuliko jina lake
Tofauti na Snapdragon na MediaTek kwa bei hii kuna processor za Samsung Exynos na UniSoC ambazo hazitupi simu nyingi nzuri za kuchagua kwa bei hii