Aiseee this time nahitaji simu ambayo haina ishu za overheating, huwa nacreate content kwa simu sasa niliikimbia sd888 maana nilitaka kuchukua note 20 ultra ila nikakimbia ishu za overheating. 8 gen 1 sikujua pia kama ina hizo ishu,
Nikataka kuhamia kwenye Google pixel 6 pro na yenyewe nikasikia ina ishu za overheating, hapa sijui kama nilifanganywa au lah, mwisho nikadondokea Bionic A14 ila Nimeanza kuregret maana simu inaoverheat na hili ndio nilikuwa nalikimbia.
Nishauri kama kuna soc yenye thermal efficiency nzuri.
Mkuu inategemea bei yako ni ipi ila chipset zenye thermal management nzuri zipo nyingi sana
*Kuna Qualcomm Snapdragon 7+ Gen 2 kwenye Redmi Note 12 Turbo/ Poco F5 (laki 6 bei AliExpress)
*Kuna MediaTek Dimensity 9200 kwenye Xiaomi 13T Pro (milioni 1 na laki 2 AliExpress)
*Kuna MediaTek Dimensity 8200 kwenye Xiaomi 13T (Laki 8 na nusu AliExpress)
*Kuna Samsung Exynos 1480 kwenye Samsung Galaxy A55 (Milioni 1 kwa hapa Tanzania)
*Kuna Qualcomm Snapdragon 7s Gen 2 ya kwenye Redmi Note 13 Pro 5G na Xiaomi Poco X6 (laki 5 na nusu AliExpress)
*Kuna Qualcomm Snapdragon 8+ Gen 1 kwenye Nothing Phone 1, Xiaomi 12S Ultra, Motorola Edge S30 Ultra, Poco F5 Pro, etc.
*Qualcomm Snapdragon 8 Gen 3 kwenye vivo X100 Ultra na Samsung Galaxy S24 Ultra (Ila Snapdragon 8 Gen 3 ina overheat kwenye baadhi ya simu mfano Xiaomi 14 Ultra na Oppo Find X7 Ultra)
*Kuna Apple A16 Bionic ya kwenye iPhone 15
Zipo nyingi kwa bei tofauti tofauti kwa hiyo unapochagua chipset angalia bei uliyo nayo na simu zinazotumia hizo SoC zina manage vipi heat.
Huku kwenye flagship hakueleweki, unaweza kuta simu mbili zinatumia chipset moja ila hii ina overheat nyingine hai overheat. Mfano Google Tensor G3 hai overheat kwenye Google Pixel 8 na 8Pro ila ina overheat kwenye Google Pixel 8A na ni chipset moja ileile. Cha msingi kuwa makini wakati wa kuchagua, simu ipi ina oveheat ipi hai overheat.
Soma na reviews za gsmarena kwenye Performance section zitakusaidia kukupa vitu vingi unavyotaka kujua