Naombeni ufafanuzi kuhusu posho za nje ya kituo cha kazi

Naombeni ufafanuzi kuhusu posho za nje ya kituo cha kazi

Joined
Apr 23, 2025
Posts
17
Reaction score
16
Salaam wakuu. Naomba msaada tajwa hapo juu kuhusu posho Kwa viongozi Hasa kuanzia ngazi ya wizara na juu yahapo.

Kinachonitatiza nikwamba,hivi kiongozi mwenye dhamana ya kushughulikia masuala yote ndani ya nchi(mikoa yote) ambaye ofisi Yake ipo Dar Kwa mfano, anaweza kulipwa posho akiwa mikoani nje ya Dar?

Tuchukulie waziri ambaye ofisi Yake ipo Dodoma, akiwa na ziara ya kikazi Kigoma analipwa posho ya nje ya kituo ilhali Bado yupo ndani ya eneo lake la utumishi?

Mfano huo ni sawa na wakurugenzi wa masharika ya umma yanayotoa huduma nchi nzima (TANESCO,TRA,TANAP, and so like),wanapewa posho wanapotembelea mikoani wakati kimsingi nao wapo ndani ya eneo lao la kiutumishi? Naombeni ufafanuzi jamani, posho ya nje ya kituo cha kazi huwa inatolewa katika mazingira gani Hasa?
 
Mawazo yote kwenye posho
, subiri vijana watakuja kulidadavua vizuri.
 
Back
Top Bottom