Naombeni ushauri kabla hili halijaniua

Usimsamehe boss wangu.
 
Hapo Sasa ndo utaelewa Nemo "Kua uyaone"
Ukiweza kupambana na tuchangamoto huto basi ujue umeshakua Sasa..
Rahisi ni kwamba ukitaka kufa kwa stress hapa Dunia basi Mwamini mwanamke utaona unavokufa taratibu taratibu..
Wewe Kama huna moyo Wala hukutakiwa kurudi kuja kuthibitisha tatizo unamwamini ndo maana ukaona ngoja nikathibitishe..
Tumia busara tu maadamu hujamuona kwa macho yaani kumfuma basi panua kifua uyahifadhi atarudia tu then ndo unakuja mbwaga.
 
Jiulize haya maswali kabla hujafanya maamuzi.

1. Je, bado unampenda mke wako?

2. Je, unafikiri anaweza kubadilika kwa alichokifanya?

3. Je, uhusiano wenu unaweza kuwa kama zamani ukiamua kumsamehe?

4. Je, unafikiria kumwacha kwa sababu ya heshima yako au kwa sababu unajua huwezi kusahau au kusamehe?

Kama ukiamua kumsamehe fanya haya.

1. Weka sheria kwenye ndoa yenu.

2. Hakikisha unaongea na wife kwa uwazi kuhusu kilichotokea na namna mnaweza kusonga mbele.

Iwapo utaamua kuachana na wife.

1. Tafuta mwanasheria akusaidie kuweka sawa mambo yote, hasa kuhusu malezi ya mtoto.

Mkuu, kwavyovyote utakavyoamua hakikisha unajipenda wewe kwanza, unajiheshimu na usiruhusu jambo hili likuharibie maisha yako.

All the best brother.
 
Sasa mkuu hapa tukushauri nini?

Biblia inasema usimuache mkeo ispokuwa kwa Uasharati tu.

Majibu unayo
 
mkuu pole sana hii issue inaumiza sana tatizo huyo mkeo hajui anacho kifanya yani hajielewi utapigiwa sana, ila suluhisho hapa ni kumpa taraka na kumrudisha kwao vinginevyo utakuja kuuwa bure maana kama ni malaya lazima ataendelea kukusumbua mwisho wa siku utaishia jera
 
Hii habari sijaielewa vizuri,ama hujatueleza vizuri au huyo mkeo kuna kitu ambacho hakieleweki kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…