Naombeni ushauri kuhusu hii fursa

Naombeni ushauri kuhusu hii fursa

Mingendeu

Senior Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
115
Reaction score
237
Nilifanya kazi kwenye kampuni moja ya kuuza vifaa vya ujenzi kwa miaka 5. Mwaka huu mwanzoni sikurenew mkataba kwasababu ya maslahi. Niliamua kupumzika.

Wiki hii katika pitapita yangu, nimekutana na kampuni mpya inayofanya shughuli zinazofanana na zile za kampuni niliyotoka Ila utofauti ni kwamba hii kampuni mpya haina wafanyakazi wazoefu.

Kurasa zao za mitandao ya kijamii hazipo active. Ukiwapigia simu na kuwauliza bidhaa, wanakujibu Kama sio watoa huduma, hawafanyi follow-up nk. Kiufupi wanamakosa mengi katika mauzo ( sekta hiyo mimi nilifanya kwa miaka 5 na kwa mafanikio Sana hapo awali), pia nnaconnection ya mawasiliano ya wateja wakubwa (dealers) nchi nzima.

Hiyo kampuni kwa kuifatilia tu, haijatangaza ajira. Ila mimi naiona fursa hapo kwao. Je njia ipi ni nzuri ya Mimi kuitumia ili niweze kupata ajira hapo?

Nahisi kwa CV yangu inaweza kunibeba kwa upande wa maslahi kiasi, maana kule kwa awali mshahara ulikuwa ni nauli, kodi, kula huwez kusave chochote.

Naomba wataalam mnishauri namna ya kuwasiliana nao ili niweze kupata nafasi hata tu ya Kama interview. Maana nnachokiogopa ni kwenda na kuacha CV reception bila kujua imefika au haijafika.
 
Nyie ndo mnaoharibia watu kula yao. Ww nenda kama unataka kazi kwenye hyo kampuni lakini achana na masuala ya aina ya huduma wanazotoa.

Nakushauri pia jua kwamba hao wafanyakazi waliopo kweny hyo kampuni unayotaka wana familia na watu wengine tegemezi kwahyo usiende kwa gia hizo za kuharibiana kibarua .

Nikukumbushe pia kwamba fahamu kuwa hao unaoona hawana huduma nzuri hawapo kwenye hyo kampuni kwa bahati mbaya kwahyo nenda taratibu mkuu,wamefeli wengi sana kuingilia vibarua vya watu kwa gia hyo.
Nikutakie siku njemaaa
 
Sijasema kuwa naenda kumuharibia mtu kazi wala siwez kutaja lolote linalohusiana na hilo, kitu kikubwa nilichokiona ni uzoefu so nikajipima nikaona kama fursa ndio maana nikaja jamvini kwa wajuvi ili waone ni kwa namna gani naweza kuitumia hiyo (uzoefu) kupenya hapo.
 
Jatibu kuomba appointment na bosi peekaboo barua ya EOI ukielezea mikakti yako na namna kampuni itakavyofanikisha kupitia wewe
 
Kama unajua ofisi zao zilipo, andaa CV yako halafu nenda physically.

Jitahidi sana either kwa appointment au kwa kuomba ukienda ofisini, hakikisha unakutana na bosi mwenyewe (kwa uliyo yaeleza hapo kama kweli unaweza kuyafanya na una hiyo Cv atakupa kazi siku hiyo hiyo) zingatia LAW OF POWER "Never outshine your master" ndiyo maana ni mhimu ukutane na bosi mwenyewe.

Kuna watu ukiwa umeshiba sana kichwani wanakuona ni threat kwao hivyo sometime wanakuwekea ukuta.

Ukikutana na Boss mfanyie SWOT analysis then mpe na experience yako na vitu ambavyo wewe unataka kuviimpliment kwenye hiyo kampuni yake/yao lazima upewe kazi mkuu.

NB.
Maelezo yako hakikisha hayamuattack mfanyakazi au mtu yeyote wa kampuni directly unapo onyesha maeneo ambayo unahisi wanaweza kuyaboresha na namna ya kuyaboresha (hiyo itakucost)
 
Asante mkuu nimeichukua hii
 
Sijasema kuwa naenda kumuharibia mtu kazi wala siwez kutaja lolote linalohusiana na hilo, kitu kikubwa nilichokiona ni uzoefu so nikajipima nikaona kama fursa ndio maana nikaja jamvini kwa wajuvi ili waone ni kwa namna gani naweza kuitumia hiyo (uzoefu) kupenya hapo.
Nani amekwambia siyo wazoefu?
 
Back
Top Bottom