BABA LEA WATOTO
JF-Expert Member
- May 6, 2017
- 352
- 782
Hali hiyo ingewafanya mchakarike muwe na maisha yenu ya kujitegemea Sasa nyie mmebweteka kumchunguza mama na ki-serengeti chake.Poleni,wanaowasimanga hapa hawajapitia mnayopitia. Duh mmetangishwa sana tangu utoton inaonekana maza hajatulia kabisaa. Hali hio muizoee tu
Kuna wamama/wababa hawashuriki,mapenzi ni upofu.
anaweza kusemea mke wa mtu akasema afadhali mumewe kampata mwalimu kuliko vibinti vya mtaani vichunaji.Umesema huyo jamaa ni mume wa mtu. Fanya roho mbaya kamsemee kwa mkewe 😂. Ila haitosolve tatizo la mama yako. Atatafuta mwingine tu.
Huyo Baba yenu mpya anaweza kuwa na Kama miaka mingapi ?Habari zenu,
Naombeni ushauri na njia za kutatua tatizo hili.Ipo hivi kwenye tumbo la Mama yetu tulikuwa watoto 7 hadi Leo hii tupo 4. Katika watoto 7 tumezaliwa na Baba tofautitofauti 4. Katika hao baba zetu kuna moja wao ndio tumekuliwa kwake toka tukiwa wadogo badaye miaka 6 iliyopita Mama alitengana Nate.
Mama ni mtumishi wa umma, hivyo alinunua kiwanja na kujenga nyumba ambapo watoto wote 4 tuliongozana nae na kwenda kuishi nae, maana haikuwezekana kukaa tena kwa huyo baba mlezi sababu katika wathili.4 tuliobaki kati yetu 1 tu ndio mwanae kwahiyo ikabidi wote sisi sote tuongozane na mama. Ikumbuke kuwa katika sisi watoto 4, mtoto 1 hamjui baba yake wengine 2 Baba yao alifariki na mtoto 1 baba take ndio huyo aliyetulea.
Sisi sote miaka yetu ni 24+ na Mama yetu ni 52, jambo linalotusumbua ni kuwa Mama yetu ana mwanaume mwingine ambaye ni mume wa mtu. Jamaa huyu huwa anakuja na kulala hapa nyumbani karibu kila siku; huwa anasitisha kuja pale ambapo kaka yetu mkubwa akija nyumbani.
Ndugu na marafiki wamejaribu kumshauri mama kuwa tayari umri umekwenda na ana vijana wakubwa anatakiwa kuacha mambo hayo pasipo mafanikio, haelezeki wala haambiwi chochote. Kwa sasa tumefunga chuo sababu ya hii CORONA nipo hapa home naona aibu kijiji kizima kinatuzungumza.
Kaka yangu mkubwa alijaribu kuongea na muyo bwana mwaka jana; kwa kweli jamaa alisitisha kama miezi 2 hivi pasipo kuonekana, badaye ratiba ikaanza kama kawaida nimemjulisha kaka atafute siku 3 nyumbani tusaidiane kutatua tatizo hili. Pia, kila tukimsuhi Mama kuacha hiyo tabia majibu anayotupa ni kuwa huu mji ni wake na hamna aliyemsaidia kujenga hivyo anafanya chochote atakacho.
Ndugu zangu wana JF, naombeni msaada wa mawazo namna ya kutatua tatizo hili.
Jamaa aweke picha ya Mama na Ankali hapa tujaribu kusuluhisha.Poleni,wanaowasimanga hapa hawajapitia mnayopitia. Duh mmetangishwa sana tangu utoton inaonekana maza hajatulia kabisaa. Hali hio muizoee tu
Kuna wamama/wababa hawashuriki,mapenzi ni upofu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kwani makonda hawezi kuingilia kati?
Mama acha kumnanga mwenzako, wewe mbona ulitoka na kijana mdogo wa JF?Mwacheni, hapo tu karibia kila mtoto ana baba yake.
Maradhi yatamfundisha so soon, na kuuguza jiandaeni
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe sio mmojawapo!Ngoja waje mkuu
Sidhani kama kutaka utamu ni tatizo, tatizo ni kukosa stara.Jael 52bado mlito...sema anatakiwa kuwa na stara fulan..angekuwa anakitana na men wake hukoo...! Lakini kimahusiano wamwache kbs! Kisa cha kufana utamu wako nini?
Lakini wana miaka 24 hata kama unasoma huyu ni mtu mzima huwezi kuingilia maisha ya mzazi wako eti tunasemwa kijijini kwahiyo kuwazaa tu nyie ndo mmpagie maisha
Naona waongee na uncle kwa kuwa kujiachia Ni Jambo huru ambalo hawapaswi kumuingilia lakini kwa Hali hii lazima waingilie maana mwanaume Ni mume wa mtu then anaweza akawaletea magonjwa mzigo ukabaki kwa watoto"jambo linalotusumbua ni kuwa Mama yetu ana mwanaume mwingine ambaye ni mume wa mtu"
Hili Ndio tatizo haswa,maana sidhani kama mnatatizo laiti kama mama yenu angelikuwa ameolewa au anaishi na mwanaume mwingine ambaye si mume wa mtu,kwa umri wake kuwa mchepuko ni fedheha na ndio maana hata jamii inamshangaa na kumsema.
Lakini kwa kuwa mlishajaribu kuzungumza naye na hakukubaliana nanyi basi hamna budi kutafuta miji yenu na kiwa mbalinae maana ninyi ni vijana wakubwa.
Maana mnaoona aibu ni nyinyi yeye anajionea sawa tu,na ndio maana anfanya hata mbele yenu.