Leonard Robert
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 11,125
- 7,373
Vijana wanavizia mafao na mzee baba anavizia mafao..mpambano mkali Sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata mkifanikiwa kumtenganisha na huyo Uncle wa sasa wakaachana basi tambueni fika atakuja Uncle mwingine kufill the void.Mama ana tatizo kubwa aliloshindwa kulitatua mapema sasa linamuandama hadi uzeeni.
Poleni sana.
Hali hiyo ingewafanya mchakarike muwe na maisha yenu ya kujitegemea Sasa nyie mmebweteka kumchunguza mama na ki-serengeti chake.
Ushauri murua sana mkuu.Kwanza mkuu kaa ukijua mama yenu anawapenda sana...kitendo cha kukubali kuwalea,kuwasomesha na kuwapa huduma zote adi mmefikia umri huo bila kusumbuana na mzaze mwenza ni jambo lenye kuonyesha upendo wa hali ya juu.
Pili,nasikitka sana pale ninapo ona mwanamke yyte kuzalishwa na wanaume tofaut tofaut Mana najua huwa hao wanawake ni vigumu kudumu ktk ndoa hususani Kama hao wanaume anapita nao bila sheria ya dini kuwaunganisha (ndoa),inauma sna kwakweli Kama mtoto kuona umezalia nje ya ndoa...ndo Mana Kwenye utaratbu wa dini ya kiislamu mtoto wa sampuli hyo kuna baadh ya haki ananyimwa na kuitwa mtoto wa zinaa.
Tatu,bi mkubwa anafanya ayo yote kuna kitu kinampa jeuri either Mali yake au uzuri wake...msaada pekee kwake ni kumjenga kiimani...wala msimchukie,mpendeni muwe karbu nae mumpe maneno ya kiimani kulingana na dini yake...Kama anampenda huyo mwanaume mumshauri wafunge ndoa nae aitwe mke halali,kukata mzizi wa fitna Kwan mwanaume kuwa na wake 2 si tatzo
Mwisho kabsa mjitaidi mtoke apo nyumban mkatafute maisha Kisha muoe wake ambao watakuwa mfano wa kuigwa na mama yenu...Mana usikute mna mind mama yenu kumbe na nyinyi mnawaingza mabint za watu kweny nyumba ya mama yenu...
Hahahaha itakua wewe ni mmoja wa watoto wa huyo mama, poleni kwa mnayopitia.Ngoja nikuache na ubishi wako sijui nikushambulie PM
Au Basi tuchart
Sisi sote miaka yetu ni 24+ na Mama yetu ni 52 ,Jambo linalotusumbua ni kuwa" Mama
Nyie watu wazima what are you doing at your mum's home she has her own life leave her alone she sacrificed for you and educated you that's enough go away at 52 she still needs a man to entertain her.......nyie siwelewi kabisa wengine tumeanza maisha at 18 na timefanikiwa mkbali tu, hayo ya mama wenu
Sent using Jamii Forums mobile app
Haipo. Happy Mother's day.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kwa hyo mkuu hakuna saikolojia ya kuuzuia mkuyenge
Sent using Jamii Forums mobile app
HAPPY MOTHER'S DAY! Huyo Mama anapaswa kupongezwa kwa ujasiri aliouonyeshaUmeelezea vyema historia ya mama ya kimahusiano sioni haja ya kumlaumu sababu iyo ndo haiba yake, muacheni afurahie maisha yake, kidogo ningelaumu endapo anabadili wanaume kile siku, ilo tendo ni haki ya msingi kabisa ya binadamu, trust me kama mkimlazimisha kuacha ayo mambo utakuja hapa kuomba ushauri juu ya tatizo kubwa linalomsumbua mama kama ulevi kupindukia ama kichaa, muacheni mama aishi maisha yake.
Duuh huo UKAUZU sasapole mkuu, tatizo hili linawakumba wengi sana bt kikubwa nikukubaliana na hali mpaka mtakapokua tayari kujitegemea japo jambo hilo hushusha heshima sana hasa watoto wakiwa wakubwa
kuna mama jirani alikua akifanya hivo japo watoto hawakukubali, alichoamua akamuita mkubwa chumban kwake kama anashida nae then akamwambia amfanye sasa maana wanambana utadhani hana hisia ukweli ilikua aibu sana
tangu siku hiyo yule bwana aliacha tabia hiyo nakuamua kukeep busy na mishe zake
Habari zenu,
Nimekuja na ID mpya ili kuficha utambulisho wangu wa awali ni kuomba msaada wa ushauri.
Naombeni ushauri na njia za kutatua tatizo hili.Ipo hivi kwenye tumbo la Mama yetu tulikuwa watoto 7 hadi Leo hii tupo 4. Katika watoto 7 tumezaliwa na Baba tofautitofauti 4. Katika hao baba zetu kuna moja wao ndio tumekuliwa kwake toka tukiwa wadogo badaye miaka 6 iliyopita Mama alitengana Nate.
Mama ni mtumishi wa umma, hivyo alinunua kiwanja na kujenga nyumba ambapo watoto wote 4 tuliongozana nae na kwenda kuishi nae, maana haikuwezekana kukaa tena kwa huyo baba mlezi sababu katika wathili.4 tuliobaki kati yetu 1 tu ndio mwanae kwahiyo ikabidi wote sisi sote tuongozane na mama. Ikumbuke kuwa katika sisi watoto 4, mtoto 1 hamjui baba yake wengine 2 Baba yao alifariki na mtoto 1 baba take ndio huyo aliyetulea.
Sisi sote miaka yetu ni 24+ na Mama yetu ni 52, jambo linalotusumbua ni kuwa Mama yetu ana mwanaume mwingine ambaye ni mume wa mtu. Jamaa huyu huwa anakuja na kulala hapa nyumbani karibu kila siku; huwa anasitisha kuja pale ambapo kaka yetu mkubwa akija nyumbani.
Ndugu na marafiki wamejaribu kumshauri mama kuwa tayari umri umekwenda na ana vijana wakubwa anatakiwa kuacha mambo hayo pasipo mafanikio, haelezeki wala haambiwi chochote. Kwa sasa tumefunga chuo sababu ya hii CORONA nipo hapa home naona aibu kijiji kizima kinatuzungumza.
Kaka yangu mkubwa alijaribu kuongea na huyo bwana mwaka jana; kwa kweli jamaa alisitisha kama miezi 2 hivi pasipo kuonekana, badaye ratiba ikaanza kama kawaida nimemjulisha kaka atafute siku 3 nyumbani tusaidiane kutatua tatizo hili. Pia, kila tukimsuhi Mama kuacha hiyo tabia majibu anayotupa ni kuwa huu mji ni wake na hamna aliyemsaidia kujenga hivyo anafanya chochote atakacho.
Ndugu zangu wana JF, naombeni msaada wa mawazo namna ya kutatua tatizo hili.
Kwanza mkuu kaa ukijua mama yenu anawapenda sana...kitendo cha kukubali kuwalea,kuwasomesha na kuwapa huduma zote adi mmefikia umri huo bila kusumbuana na mzaze mwenza ni jambo lenye kuonyesha upendo wa hali ya juu.
Kama imani inaruhusu, si umesikia ni mume wa mtuKumshauri kuacha haitowezekana kabisa cha msingi mshaurini afunge ndoa na huyo Baba.