Naombeni ushauri kuhusu nyumba yangu niliyoijenga Maramba Mawili

Naombeni ushauri kuhusu nyumba yangu niliyoijenga Maramba Mawili

Pridah

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
1,495
Reaction score
3,453
Hi JF.

Ndugu zangu naomba mawazo yenu.

Ni hivi, kuna nyumba iko hapo Mbezi Maramba mawili naona kama nilipoteza muda na hela zangu bure coz haina faida yeyote kwangu tokea nimeijenga.

Ilipokamilika nilimpa uncle wangu na wife wake wakae. Baada ya miaka 3 ndugu akajiongoza akaenda panga 2 rooms then akaleta mpangaji kwa 200K kwa mwezi. Ikawa ile kodi anatumia kulipia zile 2 rooms inayobaki anatumia.

Ikaenda hivyo for two years nikiwa sijui kitu coz baada ya kuwakabidhi sikuwahi tena kwenda huko hadi siku jirani mmoja kunipigia akilalamika kuhusu wapangaji wangu.Nikashangaa ikabidi niende kwa lengo lakuwatimua hao waliopangishwa bila idhini yangu.

Kufika Maramba, nilijicheka kumebadilika, kumejengwa hata njia ya kufika kwangu nimeisahau😁😁 ila nilifika nikakuta nyumba imechoka baadhi ya vioo vimevunjwa, vitasa hakuna, rangi ndo usiseme ila wapangaji walinipokea vizuri na walikua watu wastaarabu sana.

Nikajitambulisha na wakashangaa coz kwa 2 yrs wanajua ndugu yangu ndo mama mwenye nyumba wao wakaanza kulalamika kutapeliwa.

Nikawaambia hakijaharibika kitu endeleeni kukaa ila nikawaomba wanipe 300k kwa mwezi sababu nyumba imechoka coz 200K ni ndogo sana.

Hiyo 300K kwa mwezi walilipa miezi 6 tu then Covid 19 ikaja wakaomba 200k coz Covid imempozea baba kazi, nikakubali nikiwa naplan nikaikarabati then niweke mpangaji atakayenipa hela yakuridhika.

Cha ajabu nina hiyo plan tokea enzi za Covid ila kila nikifikiria kwenda Maramba kufanya huo mchakato naona uvivu na mind you marekebisho makubwa hapo ni rangi tu na toka nilipoenda kujitambulisha sijarudi tena Maramba so mpaka leo wananipa 200K kwa mwezi ila nahisi ni ndogo sana.

Ninawaza niiuze hiyo nyumba then nikajenge kwenye moja ya plots zangu zilizoko Mtoni Kijichi.Kijichi kuna kodi nzuri.

Au niikarabati then niongeze kodi ila hapa nashindwa kuamua coz sijui soko la nyumba za kupanga likoje hapo Maramba Mawili.

So majirani zangu wa Maramba Mawili hebu niambieni eti kajumba ka 3 bedrooms,big living room,dinning,jiko,choo cha master na public,alluminium window,tiles,umeme ikiwa kwenye hali nzuri halali yake kwa mwezi ni bei gani kupangisha kwa sasa?Enzi hizo kabla wakati nampatia uncle wangu alipatikana mpangaji wa 350K kwa mwezi kwa kila miezi 4.

Na je nikisema niuze nitapata kiasi gani eti majirani zangu wapendwa(Kwa kukadiria)

Natanguliza shukrani zangu Majirani zangu wapendwa.Sisi ni ndugu tusaidiane🙏🙏
 
Hi JF.

Ndugu zangu naomba mawazo yenu.

Ni hivi,kuna nyumba iko hapo mbezi Maramba mawili naona kama nilipoteza muda na hela zangu bure coz haina faida yeyote kwangu tokea nimeijenga...
hot-cuppa.gif
 
Usiuze wewe karabati tu then weka mtu... maramba ni moja ya maeneo ambayo yanaenda kuwa ghari sana so kama huna shida yoyote ifanyie ukarabati weka wapangaji... kodi ni makubaliano na wewe ndio unatakiwa upange kwa kushirikiana na dalali.
 
Maelezo mbona yanajichanganya? Mara uncle wako alikuwa anapokea 200k Kwa mwezi mara 350k kwa mwezi..

Mimi sio wa maramba 2 lkn ninakushauri uache tamaa.
Ilivyoisha nikawapa madalali ndo akapatikana mtu yuko tyr lutoa 350K ila nikaghairi kuipangisha baada ya kuona mazingira uncle wangu anaishi so nikampa anko akae ila badae akaipangisha ikiwa imechoka sana na mpangaji waliyemuweka ndo analipa hiyo 200K.
 
Wananikosea mwenzao nahitaji kushauriwa😭
Pole dada ,irekebishe waeleze kuwa Kodi Sasa imepanda wakikataa ,hakika utapata wapangaji wengine Ila usiwagusie suala la kupanda Kodi bila kufanya walau marekebisho fulani .

Watu wa huko Makamba hawana cha kukishauri kwakuwa Bei ya nyumba inategema na quality ya nyumba na malengo yako wewe Kama mama mwenye nyumba mfano unakuta wewe unayoisema ni nyumba Sasa unahisi wenye vibanda watakushauri nini zaidi ya kuleta zogo tu hapa
 
Ni Maramba sehemu gani, kama ni karibu na njia kuu pana hela. Maramba ni karibu na Mbezi Luis hivyo kodi inapanda kila siku, shida yake napo pamejengwa kiholela tu kama maeneo mengi ya Daslam.
 
Back
Top Bottom