Just Distinctions
JF-Expert Member
- May 5, 2016
- 3,230
- 6,742
Fanya unachopenda na kila kitu ni sawa na kinaweza kuleta matunda makubwa ila usisahau majuto ni mjukuuMimi ni baba wa watoto watatu Na mke mmoja Nina miaka 34.
Mtoto wa Kwanza ni kwa mwanamke wa Kwanza na Hawa wawili ni kwa mke niliyenae sasa ambaye naishi nae hapa nyumbani.
Nimezaliwa Na kukulia mkoa X, nimekuja Dar kutafuta Maisha lakini mji huu unahitaji uwekezaji Na connection Za biashara.
Nina nyumba yenye uwanja mkubwa, nimeijenga baada ya kwenda South Africa lakini Kwa sasa Maisha ni magumu Sana South Africa kwahiyo nikachukuwa jukumu la kurudi nyumbani.
Nilianzisha biashara ya Duka la spear za pikipiki mkoa niliozaliwa lakini Ile biashara ilikuja kufa kabisa nikaamua kuuza ili nipate Kodi ya kuja kuanza Maisha Dar es salaam.
Nimepata rafiki ambaye yeye anauza magari yake kwahiyo Mimi nikaanza Kazi ya udalali WA kuuza magari lakini Sina uzoefu hii Kazi ya udalali WA magari.
Maamuzi yangu Ni kuuza nyumba Na kuondoka mkoa X kabisa na pesa ambayo nitaipata natumia hili tobo la huyu rafiki yangu kwajili ya kununua MAGARI japani Na kuuza hapa nyumbani.
Naombe ushauri wenu wadau maamuzi ya kuuza nyumba Ni mazuri kweli ama hapana.?
Na ndio maana wahenga walisema heri kenda shika kuliko kumi nenda uje
Sasa wewe uza kila ulichonacho halafu anza upya ndio utajua ya kuwa kwanini mabeberu walisema Roma haikujengwa siku moja